Kituo cha Ufikivu

Ubunifu, ufikivu na msukumo kwa wote.

Mchakato wa maoni

Watu wanaweza kutoa maoni kupitia njia zifuatazo:

  • Fomu ya Maoni kuhusu Ufikivu: Kituo cha Ufikivu
  • Usaidizi kwa Wateja: Tembelea tovuti yetu ya usaidizi kwa maswali ya jumla au hitilafu za kiufundi.
  • Be My Eyes (BME): Spotify inashirikiana na Be My Eyes kusaidia watu wasioona na wasioona vizuri kupitia simu za video mubashara kwa usaidizi wa kuona.

Maelezo ya mchakato

Watu wana chaguo la kutoa maoni bila kujitambulisha, au kuwasilisha maelezo ya mawasiliano ili kuwezesha Spotify kufuatilia na kutoa taarifa.

Baada ya kupokea maoni ya ufikivu, Spotify inajitolea:

  1. Kuthibitisha kuwa wamepokea maoni mara moja.
  2. Kukagua na kuchunguza maoni katika mchakato wa ndani ya kampuni.
  3. Kutekeleza vitendo vinavyofaa au kutoa ufafanuzi ikiwa mabadiliko ya haraka hayawezekani.
  4. Kutoa taarifa kwa watu waliowasilisha maoni, ikiwa maelezo ya mawasiliano yametolewa

Uhakikisho wa faragha

Spotify huhakikisha kuwa maelezo ya binafsi yanayotolewa kupitia njia za maoni yanashughulikiwa kulingana na mwongozo wa msingi wa usiri wa data, sera za kuhifadhi na Sera yetu ya Faragha. Taarifa iliyowasilishwa itatumika tu kwa ajili ya kuchunguza maoni yako, kuwasiliana nawe (ikihitajika) na kuboresha ufikivu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejelea Sera ya Faragha.