Katika Spotify, tunasherehekea ubunifu wa binadamu na tunajitahidi kuhakikisha mfumo wetu unatumika na watu wote, ikiwa ni pamoja na mamilioni ya wasanii na mabilioni ya wasikilizaji. Kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu na kuwaajiri watu wenye uzoefu wa masuala ya ufikivu, tunafanya kazi kuhakikisha bidhaa zetu zote zinazingatia ufikivu. Kwa pamoja, tunalenga kuwezesha kila mtu kuunda, kugundua na kuhamasishwa.