Sera ya Faragha ya Spotify
Kutumika Kuanzia 30 Septemba 2021
- Kuhusu Sera hii
- Haki na udhibiti wa data yako ya binafsi
- Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu
- Madhumuni yetu ya kutumia data yako ya binafsi
- Kushiriki data yako ya binafsi
- Uzuiaji na ufutaji wa data
- Uhamisho hadi nchi nyingine
- Kulinda data yako binafsi
- Watoto
- Mabadiliko kwenye Sera hii
- Jinsi ya kuwasiliana nasi
1. Kuhusu Sera hii
Sera hii inaelezea jinsi tunavyochakata data yako binafsi kwenye Spotify AB
Inatumika kwenye matumizi yako ya:
- huduma zote za utiririshaji za Spotify kama mtumiaji. Hii ni pamoja na matumizi ya huduma hizi chini ya machaguo yetu ya bila malipo au ya malipo (kila "Chaguo la Huduma"); na
- Huduma nyingine za Spotify zinazojumuisha kiungo cha Sera hii ya Faragha (mfano, tovuti za Spotify, Usaidizi kwa Wateja na Tovuti ya Jamii).
Kutoka sasa na kuendelea, tutaziita hizi "Huduma za Spotify".
Mara kwa mara, tunaweza kuanzisha huduma mpya au za ziada. Pia zitazingatia Sera hii, isipokuwa ibainishwe vinginevyo wakati tunapozianzisha.
Sera hii si...
- Sheria na Masharti ya Spotify. Huo ni waraka tofauti, unaoangazia mkataba wa kisheria kati yako na Spotify wa kutumia Huduma za Spotify. Pia inaelezea kanuni za Spotify na haki zako za mtumiaji.
- Ya kuhusu matumizi yako ya huduma nyingine za Spotify zilizo na sera yazo binafsi ya faragha, kama vile Anchor, Soundtrap, Megaphone na Greenroom.
2. Haki na udhibiti wa data yako ya binafsi
Sheria za Faragha, ikiwemo Sheria ya Ulinzi wa Data wa Jumla ("GDPR"), zinawapa watu binafsi haki za data yao ya binafsi.
Tazama haki zako na fafanuzi zake katika jedwali hili.
Ni haki yako... | |
---|---|
Kufikia |
Kufahamishwa kuhusu data ya binafsi tunayochakata kukuhusu na kuomba kuifikia |
Urekebishaji |
Kuomba turekebishe au kusasisha data yako ya binafsi mahali ambapo si sahihi au haijakamilika |
Ufutaji |
Kuomba tufute sehemu fulani ya data yako ya binafsi |
Vikwazo |
Kuomba kwamba tuache kuchakata baadhi ya data yako binafsi au yote kwa muda mfupi au kwa kudumu |
Kukataa |
Kutukataza kuchakata data yako ya binafsi wakati wowote, kwa misingi inayohusiana na hali yako Kukataa data yako ya binafsi kuchakatwa kwa madhumuni ya uuzaji wa moja kwa moja |
Uhamishaji wa data |
Kuomba nakala ya data yako ya binafsi katika muundo wa elektroniki na haki ya kuipitisha data hiyo ya binafsi kwa matumizi ya huduma ya mtu mwingine |
Kutohusika katika utoaji maamuzi ya kiotomatiki |
Kutohusika kwenye uamuzi kulingana na utoaji maamuzi kiotomatiki (maamuzi bila binadamu kushirikishwa), ikiwemo kutolewa mfano, ambapo uamuzi utakuwa na athari ya kisheria kwako au kutoa athari kubwa kama hiyo. |
Jinsi ya kutumia haki zako kwenye Spotify
Fikia: Ili kuomba nakala ya data yako ya binafsi kutoka Spotify, tembelea akaunti yako ya Mipangilio ya Faragha. Hapo unaweza kupakua kiotomatiki data zako nyingi za binafsi na ujue jinsi ya kuomba taarifa zaidi.
Urekebishaji: Unaweza kuhariri Data yako ya Mtumiaji chini ya "Hariri wasifu" katika akaunti yako.
Ufutaji:
- Unaweza kuondoa maudhui ya sauti kwenye wasifu wako kwa kuteua maudhui yanayofaa na kuchagua kuyaondoa. Kwa mfano, unaweza kuondoa orodha za kucheza kwenye wasifu wako, au kuondoa wimbo kwenye orodha yako ya kucheza.
- Ili kuomba ufutaji wa data yako nyingine ya binafsi kwenye Spotify (mfano, Data yako ya Mtumiaji, Data ya Matumizi na data nyingine zilizoorodheshwa katika Sehemu ya 3 'Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu' hapa chini), tazama ukurasa wetu wa usaidizi.
Haki zako nyingine: Unaweza kuwasiliana na Spotify moja kwa moja ili kutumia haki zako wakati wowote (tazama Sehemu ya 11 'Jinsi ya kuwasiliana nasi').
Zaidi ya hayo, hizi hapa rasilimali na vidhibiti vya faragha:
- Kituo cha Faragha - taarifa zaidi kuhusu jinsi Spotify hutumia data yako ya binafsi, haki zako na jinsi ya kutumia aki hizo.
- Mipangilio ya Faragha - dhibiti uchakataji wa data fulani za binafsi, ikiwemo Tailored Ads.
- Mipangilio ya Arifa - jifunze jinsi ya kuweka mawasiliano gani ya uuzaji ambayo unapokea kutoka Spotify.
- Mipangilio (Kompyuta ya Mezani na Simu ya Mkononi) - dhibiti vipengele fulani vya Huduma za Spotify kama vile "Jamii" na "Maudhui ya Kingono".
- Sera ya Vidakuzi - taarifa kuhusu jinsi tunavyotumia vidakuzi na jinsi ya kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi VIdakuzi ni faili zilizohifadhiwa kwenye simu, kompyuta kibao au kompyuta yako ya mezani unapotembelea tovuti.
Pia una haki ya kuwasiliana na Mamlaka ya Uswidi ya Ulinzi wa Faragha au mamlaka yako ya karibu ya ulinzi wa data kuhusu maswali au masuala yoyote.
3. Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu
Majedwali haya yamebainisha kategoria za data binafsi tunazokusanya na kutumia.
Hukusanywa wakati unajisajili kwa Huduma za Spotify au wakati unasasisha akaunti yako | |
---|---|
Kategoria |
Ufafanuzi |
Data ya Mtumiaji |
Data ya binafsi tunayohitaji ili kufungua akaunti yako ya Spotify na kukuwezesha kutumia Huduma za Spotify. Aina ya data inayokusanywa inategemea na aina ya Chaguo la Huduma ulilo nalo, jinsi ya kufungua akaunti yako, nchi unayokaa sasa na ikiwa unatumia huduma nyingine kuingia kwenye akaunti. Hii inaweza kujumuisha:
Tunapokea baadhi ya data hii kutoka kwako mfano, kutoka kwenye fomu ya usajili au ukurasa wa akaunti. Pia tunakusanya baadhi ya data hii kutoka kwenye kifaa chako mfano, nchi. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya nchi, tazama “Eneo lako la jumla (liliso halisi)”. |
Data ya Anwani ya Barabara |
Huenda tukaomba anwani yako ya barabaa kwa sababu zifuatazo:
Katika hali fulani, tunaweza kutumia programu nyingine ya ramani (kama vile Ramani za Google) ili kukusaidia kuthibitisha anwani yako. |
Hukusanywa kupitia matumizi yako ya Huduma za Spotify | |
---|---|
Kategoria |
Ufafanuzi |
Data ya Utumiaji |
Data ya binafsi inayokusanywa kukuhusu wakati unapofikia na/au kutumia Huduma za Spotify. Kuna aina chache za taarifa ambazo hizi zinajumuisha, zimeelezwa kwa kina katika sehemu zifuatazo. Taarifa kuhusu jinsi unavyotumia Spotify Mifano ni pamoja na:
Data yako ya kiufundi Mifano ni pamoja na:
Eneo lako la jumla (lisilo halisi) Hii inaweza kueleweka kutoka data ya kiufundi (mfano, anwani yako ya IP, mipangilio ya lugha ya kifaa chako, au sarafu ya malipo). Tunahitaji hii ili kutimiza matakwa ya kijiografia katika makubaliano yetu na wamiliki wa maudhui kwenye Huduma za Spotify na kutoa maudhui na matangazo yanayokufaa. Data ya sensa ya kifaa chako Data ya sensa ya kifaa cha mkononi iliyozalishwa kwa mwendo au maelekezo (mfano, accelerometer au gyroscope) ikiwa inahitajika ili kutoa vipengele vya Huduma za Spotify zinazohitaji data hii. |
Data ya ziada unayoweza kutupa | |
---|---|
Kategoria |
Ufafanuzi |
Data ya Sauti |
Ikiwa vipengele vya sauti vinapatikana katika soko lako na mahali ulipotoa idhini, tunakusanya data ya sauti (klipu za sauti yako). Hii inatuwezesha kutoa na kuboresha vipengele vya sauti vya Spotify. Kwa taarifa zaidi angalia Sera yetu ya Kudhibiti Sauti. |
Data ya Malipo na Ununuzi |
Ukifanya ununuzi wowote kutoka Spotify (ikiwemo Chaguo la Huduma za kulipia) au ukijisajili kwa jaribio, tutahitaji kuchakata data yako ya malipo. Data halisi ya binafsi inayokusanywa inatofautiana kutegemea mbinu ya malipo, lakini itajumuisha taarifa kama vile:
|
Mashindano, Utafiti na Data ya Bahati nasibu |
Wakati unapokamilisha fomu zozote, kujibu utafiti au dodoso, au kushiriki kwenye mashindano au bahati nasibu, tunakusanya data ya binafsi unayotoa. |
Iliyokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya vingine (‘mhusika mwingine’) | |
---|---|
Kategoria za wahusika wengine |
Ufafanuzi |
Wabia wa uthibitishaji |
Ukijisajili kwa ajili ya au ukiingia kwenye huduma zetu ukitumia huduma nyingine, tutapokea taarifa zako kutoka kwazo ili kusaidia kufungua akaunti nasi. |
Programu, huduma na vifaa vingine unavyounganisha kwenye akaunti yako ya Spotify |
Ukiunganisha akaunti yako ya Spotify kwenye programu, huduma na/au vifaa vingine, tunaweza kukusanya taarifa fulani kutoka kwavyo ili kuwezesha ujumuishaji. Programu, huduma au vifaa hivyo vingine vinaweza kujumuisha:
Tutaomba idhini yako kabla hatujakusanya taarifa zako kutoka kwa wahusika fulani. |
Wabia wa huduma ya kiufundi |
Tunashirikiana na wabia wa huduma ya kiufundi ambao wanatupa data fulani, kama vile anwani za IP za ramani za data ya eneo lisilo halisi (mfano, jiji, jimbo). Hii inawezesha Spotify kutoa Huduma za Spotify, maudhui na vipengele. |
Wabia wa malipo |
Ukichagua kulipa Spotify kwa ankara, tunaweza kupata data kutoka kwa wabia wetu wa malipo. Hii inaturuhusu:
|
Wabia wa kutangaza na kutafuta soko |
Tunaweza kupata data kukuhusu kutoka kwa wabia fulani wa kutangaza na kutafuta soko. Hii inaweza kujumuisha:
Hii inaturuhusu kutoa matangazo yanayofaa zaidi na utafutaji soko. |
4. Madhumuni yetu ya kutumia data yako ya binafsi
Jedwali lililo hapa chini linabainisha:
- madhumuni yetu ya kuchakata data yako ya binafsi
- uthibitishaji wetu wa kisheria (kila moja inayoitwa "msingi wa kisheria") chini ya sheria ya ulinzi wa data, kwa kila madhumuni
- Kategoria za data binafsi tunayotumia kwa kila madhumuni (tazama zaidi kuhusu kategoria hizi katika Sehemu ya 3 'Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu')
Huu hapa ufafanuzi wa kila "msingi wa sheria" ili kukusaidia kuelewa jedwali:
- Utendaji wa Mkataba: Wakati inahitajika kwa Spotify (au mhusika mwingine) kuchakata data yako ya binafsi:
- kutii majukumu chini ya mkataba nawe, mfano, majukumu ya Spotify chini ya Sheria na Masharti ya kukupa Huduma za Spotify
- au kuthibitisha taarifa kabla ya mkataba mpya nawe kuanza.
- Haja Halali: Wakati Spotify (au mhusika mwingine) ana haja ya kutumia data yako ya binafsi kwa njia fulani, ambayo inahitajika na imethibitishwa kwa kuzingatia hatari yoyote inayowezekana kwako na watumiaji wengine wa Spotify. Kwa mfano, kutumia Data yako ya Mtumiaji ili kuboresha Huduma za Spotify kwa watumiaji wote. Wasiliana nasi ikiwa unataka kuelewa uthibitishaji mahususi.
- Idhini: Wakati Spotify inakuomba kubainisha makubaliano yako kwa Spotify kutumia data yako ya binafsi kwa madhumuni fulani.
- Kutii Majukumu ya Kisheria: Wakati lazima Spotify ichakate data yako ya binafsi kutii sheria.
Madhumuni ya kuchakata data yako | Msingi wa kisheria unaoruhusu madhumuni | Kategoria za data ya binafsi inayotumiwa kwa madhumuni |
---|---|---|
Ili kutoa Huduma za Spotify zilizoboreshwa. |
|
|
Kuelewa, kugundua, kusuluhisha, na kurekebisha masuala ya Huduma ya Spotify. |
|
|
Kutathmini na kukuza vipengele vipya, teknolojia, na maboresho ya Huduma ya Spotify. |
|
|
Kwa madhumuni ya uuzaji, uendelezaji, na matangazo. |
|
|
Kuzingatia majukumu ya kisheria na maombi ya utekelezaji wa sheria. |
|
|
Ili:
|
|
|
Kuanzisha, kutekeleza, au kutetea madai ya kisheria. |
|
|
Kufanya mipango ya biashara, kuripoti, na kutabiri. |
|
|
Kushughulikia malipo yako. |
|
|
Kugundua na kuzuia ulaghai, pamoja na malipo ya ulaghai na utumiaji mbaya wa Huduma za Spotify. |
|
|
Kufanya uchunguzi, mashindano, tafiti na bahati nasibu. |
|
|
Katika mamlaka ambapo maslahi halali hayatambuliki kuwa msingi wa kisheria, tunategemea hitaji au idhini ya mkataba.
5. Kushiriki data yako ya binafsi
Sehemu hii inabainisha kategoria za wapokeaji wa data ya binafsi iliyokusanywa au inayotokana na matumizi yako ya Huduma ya Spotify.
Taarifa inayopatikana kwa umma
Data ya binafsi ifuatayo hupatikana hadharani kwenye Huduma za Spotify:
- Jina lako la wasifu
- Picha ya wasifu wako
- Orodha zako za kucheza za umma
- Unayemfuata kwenye Huduma za Spotify
- Anayekufuata kwenye Huduma za Spotify (unaweza kuondoa wafuasi)
Data ya binafsi unayoweza kuchagua kushiriki
Tutashiriki tu data ya binafis ifuatayo na wale waliobainishwa katika jedwali hapa chini:
- Pale ambapo data fulani ya binafsi inahitajika kwa matumizi ya kipengele cha Huduma za Spotify, au programu ya mhusika mwingine, huduma au kifaa, ambacho umechagua kutumia; au
- vinginevyo ukitupa ruhusa yako kushiriki data ya binafsi, k.v. kwa kuchagua mpangilio unaofaa katika Huduma za Spotify au kutoa idhini yako
Kategoria za wapokeaji | Sababu ya kushiriki |
---|---|
Programu na vifaa vingine unavyounganisha kwenye Akaunti yako ya Spotify |
Ili kuunganisha akaunti yako ya Spotify na/au kukuruhusu kutumia Huduma za Spotify kuhusiana na programu, huduma au vifaa vingine. Mifano ya programu, huduma na vifaa vingine kama hivyo ni pamoja na: programu za mitandao ya jamii, vifaa vya spika, runinga, mifumo ya magari, au visaidizi vya sauti, vinavyotumia Huduma za Spotify. Unaweza kuona na kuondoa miunganisho mingi ya wahusika wengine chini ya “Programu” katika akaunti yako. |
Jumuia ya usaidizi |
Ili kukuwezesha kutumia huduma ya Jumuia ya Usaidizi wa Spotify. Unapojisajili kwa akaunti kwenye Jumuia ya Usaidizi wa Spotify, tutakuomba ubainishe jina la wasifu. Hii itaonyeshwa hadharani kwa yeyote anayetumia Jumuia ya Usaidizi wa Spotify. Pia tutaonyesha maswali au maoni yoyote unayochapisha. |
Watumiaji wengine wa Spotify |
Ili kushiriki taarifa kuhusu matumizi yako ya Huduma za Spotify na watumiaji wengine wa Spotify, ikiwemo ‘Wafuasi wako wa Spotify’. Kwa mfano, chini ya mipangilio ya “Jamii” unaweza kuchagua ikiwa utashiriki wasanii wako waliochezwa hivi majuzi na orodha zako za kucheza kwenye wasifu wako. |
Wasanii na lebo za rekodi |
Ili kupokea habari au ofa za matangazo moja kwa moja kutoka kwa wasanii, rekodi lebo au wabia wengine. Unaweza kuchagua kushiriki data ya binafsi (kwa mfano, anwani yako ya barua pepe) kwa madhumuni haya. Utakuwa na chaguo la kubadilisha nia yako kila wakati na utoe idhini yako wakati wowote. |
Taarifa tunazoweza kushiriki
Tazama jedwali kwa maelezo kuhusu yule tunayeshiriki kwake na sababu.
Kategoria za wapokeaji | Sababu ya kushiriki |
---|---|
Watoa huduma |
Ili waweze kutoa huduma zao kwa Spotify. Huduma hizi zinaweza kujumuisha wale tunaowaajiri ili:
|
Wachakataji wa malipo |
Ili waweze kuchakata malipo yako, na kwa madhumuni ya kupambana na ulaghai. |
Wabia wa matangazo |
Ili wabia wetu waweze kutusaidia kukupa matangazo yanayokufaa zaidi kwenye Huduma za Spotify. Kwa mfano, wabia wetu wa matangazo hutusaidia kuwezesha matangazo yanayokufaa:
|
Wabia wa Utafitaji Soko |
Ili kutangaza Spotify na wabia wetu. Tunashiriki data ya binafsi na wabia hawa pale inapohitajika ili:
Mifano ya wabia ni pamoja na:
Wabia wetu pia wanaweza kuchanganya data ya binafsi tunayoshiriki nao na data nyingine wanayokusanya kukuhusu (mfano, matumizi yako ya huduma zao). Sisi na wabia wetu tunaweza kutumia taarifa hizi kukupa ofa, promoshoni au shughuli nyingine za utafutaji soko tunazoamini zitakufaa. |
Kushiriki kwingine na wabia |
Tunaweza kushiriki data ya binafsi na wabia ili kutusaidia kuelewa na kuboresha utendaji wa bidhaa zetu na ubia wetu. Unaweza kuona na kuondoa miunganisho mingi ya mbia chini ya “Programu” katika akaunti yako. |
Watafiti wa elimu |
Kwa ajili ya shughuli kama vile uchanganuzi wa takwimu na elimu lakini katika muundo wa jina bandia pekee. Data ya jina bandia ni wakati data yako inatambuliwa kwa msimbo badala ya jina lako au taarifa nyingine zinazokutambulisha moja kwa moja. |
Kampuni nyingine tanzu za Spotify |
Kule tuliko na ofisi, ili kufanya shughuli zetu za kila siku na ili tudumishe na kukupa Huduma za Spotify. |
Mamlaka ya utekelezaji sheria na mengine |
Tunapoamini kwa nia njema ni muhimu kwetu kufanya hivyo, kwa mfano:
|
Wanunuzi wa biashara yetu |
Pale tunapouza au kukubaliana kuuza biashara yetu kwa mnunuzi au mnunuzi mtarajiwa. Katika hali hii, Spotify itaendelea kuhakikisha data yako ya binafsi inawekwa siri. Tutakupa notisi kabla ya data yako ya binafsi kuhamishwa kwa mnunuzi au sera ya faragha tofauti kuanza kutumika. |
6. Uhifadhi na Ufutaji wa data
Uhifadhi
Tunaweka data yako ya binafsi tu kwa muda unaohitajika ili kukupa Huduma za Spotify na kwa madhumuni ya biashara halali na muhimu ya Spotify, kama vile:
- kudumisha utendaji wa Huduma za Spotify
- kufanya maamuzi ya biashara yanayoongozwa na data kuhusu vipengele vipya na ofa
- kutii majukumu yetu ya kisheria
- kusuluhisha mabishano
Ufutaji
Ukifunga au kuomba kwamba tufunge akaunti yako, tutafuta au kuondoa utambulisho data yako ya binafsi ili isikutambulishe tena, isipokuwa tuhitajike kuweka kitu au bado tunahitaji kuitumia kwa sababu inayothibitishwa kisheria.
Hii hapa mifano ya hali ambapo tunaruhusiwa au kuhitajika kisheria kuhifadhi baadhi ya data yako ya binafsi:
- ikiwa kuna suala ambalo halijasuluhishwa kuhusiana na akaunti yako, kama vile mkopo ambao haujalipwa au dai au mabishano ambayo hayajasuluhishwa
- kwa majukumu yetu ya kisheria, kodi, ukaguzi na uhasibu.
- Kwa maslahi yetu ya biashara halali kama vile kuzuia udanganyifu au kudumisha usalama.
7. Uhamisho hadi nchi nyingine
Unapofanya shughuli zilizoelezwa katika Sera hii, Spotify hushiriki data yako ya binafsi ndani na kampuni za Spotify, wakandarasi na wabia ili kukupa Huduma za Spotify. Wanaweza kuchakata data yako katika nchi ambazo sheria zake za ulinzi wa data zinasemekana si thabiti kama sheria za Umoja wa Ulaya wala zile za nchi yako, mfano, huenda wasikupe haki sawa za data yako.
Kila tunapohamisha data ya binafsi ndani, tunatumia zana:
- kuhakikisha kuwa uhamisho unatii sheria inayotumika
- kusaidia kuipa data yako kiwango sawa cha ulinzi kama iliyo nao Umoja wa Ulaya
Tunafanya hili kwa kutumia ulinzi mbalimbali, inavyofaa kwa kila uhamisho wa data. Kwa mfano, tunatumia:
- Vifungu vya Mkataba vya Wastani (au chombo mbadala cha kisheria) kuhitaji mhusika mwingine kulinda data yako na kukupa haki na ulinzi wa kiwango cha Umoja wa Ulaya
- ulinzi wa kiufundi, kama vile usimbaji fiche na utumiaji wa jina bandia
- sera na michakato ya kupinga kutolingana au maombi ya mamlaka ya serikali ya kinyume cha sheria
Unaweza kutumia hak zako chini ya Vifungu vya Mkataba wa Wastani kwa kuwasiliana nasi au mhusika mwingine anayechakata data yako ya binafsi.
8. Kulinda data yako ya binafsi
Tumeahidi kulinda data binafsi ya watumiaji wetu. Tunatekeleza hatua za kiufundi na shirika zinazofaa ili kusaidia kulinda usalama wa data yako ya binafsi. Hata hivyo, fahamu kuwa hakuna mfumo ulio salama kikamilifu.
Tumetekeleza kinga mbalimbali ikiwemo uandikaji wa jina bandia, usimbaji kwa njia fiche, ufikiaji na sera za uzuiaji ili kukinga dhidi ya ufikiaji usiodhinishwa na uzuiaji usiohitajika wa data binafsi katika mifumo yetu.
Ili kulinda akaunti yako ya mtumiaji, tunakuhimiza:
- utumie nenosiri thabiti ambalo ni la kipekee kwenye akaunti yako ya Spotify
- usiwahi kushiriki nenosiri lako na yeyote
- punguza ufikiaji wa kompyuta na kivinjari chako
- toka pindi unapokamilisha kutumia Huduma za Spotify kwenye kifaa kinachoshirikiwa
- soma maelezo zaidi kuhusu kulinda akaunti yako
Unaweza kutoka kwenye Spotify katika sehemu mbalimbali mara moja kwa kutumia kipengele cha "Toka kila mahali" kwenye ukurasa wa akaunti yako.
Ikiwa watu wengine wana uwezo wa kufikia akaunti yako ya Spotify (kwa mfano ikiwa umewapa ruhusa ya kutumia akaunti yako kwenye kifaa kinachoshirikiwa), basi wanaweza kufikia data ya binafsi, udhibiti na Huduma za Spotify zinazopatikana katika akaunti yako.
Ni jukumu lako kuwapa tu watu ruhusa ya kutumia akaunti yako unaporidhika kushiriki nao data hii ya binafsi. Mtu mwingine kutumia akaunti yako ya Spotify kunaweza kuathiri mapendekezo yako yaliyoboreshwa na kujumuishwa katika upakuaji wa data yako.
9. Watoto
Fahamu: Sera hii haitumiki kwa Spotify Kids, isipokuwa Sera ya Faragha ya Spotify Kids iseme hivyo. Spotify Kids ni programu tofauti ya Spotify.
Huduma za Spotify ina "Kikomo cha Umri" cha chini zaidi katika kila nchi. Huduma za Spotify hazielekezwi kwa watoto ambao umri wao:
- ni chini ya miaka 13
- au, inaharamisha kuchakata data yao ya binafsi
- au, inahitaji idhini ya mzazi kuchakata data yao ya binafsi
Hatukusanyi data binafsi kwa kujua kutoka kwa watoto chini ya Kikomo cha Umri kinachotumika. Ikiwa uko chini ya Kikomo cha Umri, tafadhali usitumie Huduma za Spotify na usitupe data yoyote ya binafsi. Badala yake, tunapendekeza kutumia akaunti ya Spotify Kids.
Ikiwa wewe ni mzazi wa mtoto aliye chini ya Kikomo cha Umri na ufahamu kuwa mtoto wako ameipa Spotify data ya binafsi, tafadhali wasiliana nasi.
Tukifahamu kuwa tumekusanya data ya binafsi ya mtoto chini ya Kikomo cha Umri, tutachukua hatua zinazofaa kuifuta data ya binafsi. Hii inaweza kutuhitaji kufuta akaunti ya Spotify ya mtoto huyo.
Unapotumia kifaa kinachoshirikiwa kwenye Huduma za Spotify, unapaswa kutahadhari kuhusu kucheza au kupendekeza maudhui yoyote kwa watu walio chini ya miaka 18 jambo linaloweza kuwa la kutofaa kwao.
10. Mabadiliko kwenye Sera hii
Tunaweza kufanya mabadiliko kwenye Sera hii mara mojamoja.
Tunapofanya mabadiliko kwenye Sera hii, tutakupa notisi inavyofaa chini ya hali husika. Kwa mfano, tunaweza kuonyesha ilani maarufu ndani ya Huduma za Spotify au kukutumia arifa ya barua pepe au kifaa.
11. Jinsi ya kuwasiliana nasi
Kwa swali au suala lolote kuhusu Sera hii, wasiliana na Afisa wa Ulinzi wa Data kwa njia yoyote kati ya hizi:
- Tumia fomu yetu ya mawasiliano ya faragha
- Barua pepe privacy@spotify.com
- Tutumie barua kwenye: Spotify AB, Regeringsgatan 19, 111 53 Stockholm, Sweden
Pia unaweza kutembelea Kituo chetu cha Faragha kwa ufafanuzi wa Sera hii.
Spotify AB ni mdhibiti wa data wa data binafsi inayochakatwa chini ya Sera hii.
© Spotify AB