Kituo cha Ufikivu

Ubunifu, ufikivu na msukumo kwa wote.

Taarifa ya ahadi

Katika Spotify, tunasherehekea ubunifu wa binadamu na kujitahidi ili mfumo wetu utumike na watu wote. Kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu na kuwaajiri watu wenye uzoefu wa masuala ya ufikivu, tunafanya kazi kuhakikisha bidhaa zetu zote zinazingatia ufikivu. Kwa pamoja, tunalenga kuwezesha kila mtu kuunda, kugundua na kuhamasishwa.

Mfumo wetu ni wa kila mtu, kama ilivyo mahali petu pa kazi. Unakaribishwa jinsi ulivyo, bila kujali unatoka wapi, unaonekanaje, au kinachocheza kwenye vifaa vyako vya sauti vya kichwani.

Hivi ndivyo tunavyojitolea kufikia malengo ya ufikivu katika mahali pa kazi, mfumo na watumiaji:

Wafanyakazi wetu: Kadiri tunavyowakilisha na kukuza mitazamo zaidi ndani ya kumbi za Spotify, ndivyo sote tutakavyochangia zaidi, kustawi na kuwa mahiri. Tumejitolea kuzingatia ufikivu katika kila kitu tunachofanya kwa watu wetu ulimwenguni kote. Tutaendelea kukuza mpango wetu wa kimataifa wa afya ya akili, Moyo na Nafsi na tumejitolea kufanya maeneo katika ofisi zetu za kimataifa kufikiwa kikamilifu.

Wasikilizaji: Spotify ni sehemu ya maisha ya mamilioni ya watu duniani kote, na kuhakikisha mfumo wetu ni fikivu kwa kila mtu ni jambo la kipaumbele.

Wasanii na watayarishi: Mfumo wetu una nguvu, na tunautumia kukuza sauti, hadithi na tamaduni za jumuiya ulimwenguni kote. Tutaendelea kuboresha usaidizi wetu kwa wasanii na watayarishi wenye ulemavu na kutumia mfumo wetu kushiriki vipaji vyao.

Hakuna njia bora ya kukuza zaidi mawazo haya kuliko kutoa mpango mahususi na unaoweza kupimika ili tuutumie katika utekelezaji na uwajibikaji.