"Hamna Chochote Kutuhusu Bila Sisi" ni imani ya kimsingi ya Harakati ya Haki za Walemavu, inayoelezea haja ya ushiriki kamili wa watu wenye ulemavu katika kazi na uvumbuzi wowote kwa niaba yao. Mojawapo ya njia tunazotekeleza muundo huu ni kupitia ushirikiano wetu na Fable, mfumo wa ufikivu unaoendeshwa na watu wenye ulemavu. Timu ya Fable, pamoja na jumuiya yetu ya ndani ya #able, kikundi cha wafanyakazi wenye ulemavu au wenye akili inayofanya kazi tofauti na ilivyo kawaida, walishirikishwa katika kila hatua ya Mpango huu.
Kwa usaidizi wa Fable, Spotify ilifanya utafiti wa zaidi ya watu 100 wenye ulemavu kuhusu mahitaji na mapendeleo yao yanayohusiana na ufikivu. Majibu yalijumuisha mitazamo kutoka kwa watu wanaotumia teknolojia ya usaidizi kwa ajili ya kuona, kusikia, utambuzi, kunena na/au kwenda. Utafiti ulishughulikia mada mbalimbali kama vile huduma kwa wateja, mawasiliano, kuajiri, maeneo halisi, bidhaa za kidijitali na mazingira. Fable pia iliendesha kipindi cha kikundi cha mtandaoni na watu wanne walio na mahitaji mbalimbali ya ufikivu ili kuzama zaidi katika mada sawa. Maarifa haya yalitumiwa katika uundaji wa Mpango wa Ufikivu wa Spotify.
Baada ya Mpango kutayarishwa, kundi la nyongeza lenye washiriki watano wenye ulemavu lilipitia rasimu na kutoa maoni juu yake. Mbinu hii ya kurudiarudia inayohusisha watu wenye ulemavu katika uundaji wa Mpango ilisaidia kufichua maeneo ya kuboresha na kuleta imani katika mwelekeo wa juhudi za ufikivu za Spotify katika miaka mitatu ijayo.
Kama mfano wa jinsi mashauriano yetu yalivyopelekea uundaji wa Mpango huu, wahojiwa wa utafiti walisema mtu anayejibu maswali ya huduma kwa wateja anapaswa kufahamu teknolojia ya usaidizi na ufikivu. Kutokana na maoni haya, katika sehemu ya "Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)" ya Mpango huu, Spotify imejitolea kupanua timu yetu iliyopo kwa maarifa, ujuzi na zana zilizoimarishwa za kuwasaidia watu wenye ulemavu.