Sera ya Vidakuzi ya Spotify
Itatumika kuanzia tarehe 25 Februari 2026
3. Chaguo za kudhibiti vidakuzi na matangazo yanayotokana na mambo yanayokuvutia
Sera hii inafafanua jinsi Spotify inavyotumia vidakuzi na teknolojia zinazofanana (kwa pamoja, "vidakuzi"). Kuanzia sasa, tutaiita 'Sera'. Madhumuni ya Sera hii ni kukupa maelezo dhahiri kuhusu matumizi ya vidakuzi na teknolojia zinazofanana na Spotify. Inatumika kwa mtu yeyote anayetumia huduma au tovuti za Spotify (pamoja zinaitwa 'Huduma'). Sera hii pia inafafanua chaguo ulizo nazo za kudhibiti mipangilio yako ya vidakuzi.
1. Vidakuzi ni nini?
Vidakuzi na teknolojia zinazofanana, kama vile lebo za pikseli, ni faili ndogo zinazopakuliwa kwenye kifaa chako. Katika sera hii, tutavirejelea kwa pamoja kama "vidakuzi". Faili hizi huwekwa kwenye kifaa chako unapotumia vipengele vya Spotify. Kwa mfano, hili linaweza kufanyika unapotembelea tovuti yetu, unapotumia programu yetu, unapotumia mojawapo ya matangazo yetu au unapofungua barua pepe kutoka kwetu. Vidakuzi ni muhimu kwa sababu huruhusu Spotify na washirika wetu kutambua kifaa chako kwa kipekee. Vinasaidia pia katika mwendelezo wa hali yako ya matumizi. Kwa mfano, vidakuzi vinaweza kutusaidia kuelewa mapendeleo yako au kukumbuka vitendo vyako vya awali. Unaweza kupata maelezo ya jumla kuhusu vidakuzi katika: www.allaboutcookies.org.
2. Tunatumiaje vidakuzi?
Vidakuzi hutekeleza kazi nyingi tofauti. Vinakuruhusu kusogeza kati ya kurasa kwa ufanisi zaidi. Vinakumbuka pia mapendeleo yako na husaidia kuboresha hali yako ya matumizi. Vinaweza pia kuhakikisha kuwa matangazo unayoonyeshwa mtandaoni yanakufaa zaidi na yanaendana na mambo yanayokuvutia.
Spotify hutumia aina mbili kuu za vidakuzi: (1) vidakuzi ambavyo ni sharti vitumike; na (2) vidakuzi visivyo vya lazima:
- *Vidakuzi ambavyo ni Sharti Vitumike
Vidakuzi hivi huwekwa na Spotify au mhusika mwingine kwa niaba yetu. Ni muhimu ili kukuwezesha kutumia vipengele vya Huduma zetu. Vinakuruhusu kufanya mambo kama vile kutazama maudhui, kuweka chaguo zako za faragha, kuingia katika akaunti, kulipia huduma au kujaza fomu. Bila vidakuzi hivi, huwezi kutumia Huduma zetu na hivyo hupaswi kuvikataa.
- *Vidakuzi visivyo vya Lazima
Vidakuzi visivyo vya lazima vinaweza kuwa 'vidakuzi vinavyohifadhiwa kwenye tovuti unayotembelea' au 'vidakuzi vya wahusika wengine tofauti na tovuti unayotembelea'. Vidakuzi vinavyohifadhiwa kwenye tovuti unazotembelea huwekwa moja kwa moja na Spotify au na mhusika mwingine kwa ombi letu. Vidakuzi vya wahusika wengine tofauti na tovuti unazotembelea huwekwa moja kwa moja na wahusika wengine au na Spotify kwa ombi la mhusika mwingine, kama vile watoa huduma wetu wa takwimu au utangazaji. Unaweza kuona orodha ya washirika hawa katika kiungo hiki. Spotify, au washirika wetu, hutumia vidakuzi visivyo vya lazima katika njia zifuatazo:
|
Aina ya Kidakuzi |
Madhumuni |
|---|---|
|
Vidakuzi ambavyo ni Sharti Vitumike |
Vidakuzi hivi ni muhimu ili kukuwezesha utumie vipengele vya Huduma zetu, kama vile kuwasilisha maudhui kiufundi, kuweka mapendeleo yako ya mipangilio, kuingia katika akaunti, kufanya malipo au kujaza fomu. Bila vidakuzi hivi, Huduma zetu haziwezi kutolewa na hivyo huwezi kuzikataa. |
|
Vidakuzi vya Utendaji |
Vidakuzi hivi hukusanya maelezo kuhusu jinsi watumiaji wanavyotumia Huduma zetu. Kwa mfano, vidakuzi hivi huturuhusu kuhesabu idadi ya watu wanaotembelea tovuti yetu na kuelewa jinsi wanaotembelea tovuti yetu walivyoipata. Takwimu za mtandaoni zinazotumia vidakuzi kukusanya data ili kuimarisha utendaji wa tovuti huwekwa katika aina hii. Kwa mfano, zinaweza kutumika kufanya majaribio ya usanifu na kuhakikisha mwonekano thabiti unadumishwa kwa ajili ya mtumiaji. Tunaweza pia kupata maelezo kutoka kwenye majarida yetu ya barua pepe au mawasiliano mengine tunayokutumia, ikiwa ni pamoja na iwapo ulifungua au kusambaza jarida au kubofya maudhui yake yoyote. Maelezo haya hutueleza kuhusu ufanisi wa majarida na kukusaidia kuhakikisha kuwa tunakupa maelezo yanayokuvutia. Aina hii haijumuishi vidakuzi vinavyotumika kwa ajili ya mitandao ya utangazaji unaolenga mambo yanayowavutia/tabia za wanaolengwa. |
|
Kiutendaji |
Vidakuzi hivi huruhusu Huduma zetu kukumbuka chaguo unazofanya kama vile jina lako la mtumiaji, lugha au eneo uliko na kutoa maudhui na vipengele vilivyoimarishwa, vinavyokufaa zaidi. Kwa mfano, vidakuzi hivi vinaweza kutumika kukumbuka mabadiliko uliyofanya kwenye sehemu za kurasa za wavuti unazowekea mapendeleo. Vidakuzi hivi hukumbuka chaguo ulizofanya ili kuboresha hali yako ya utumiaji. Usiporuhusu vidakuzi hivi, basi baadhi ya chaguo ulizofanya ulipotembelea Huduma zetu awali hazitahifadhiwa. |
|
Vidakuzi vya utangazaji au vilivyowekewa mapendeleo |
Vidakuzi hivi hukusanya maelezo kuhusu tabia zako za kuvinjari ili kukuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi na kuelewa mambo yanayokuvutia. Vitatumika pia kudhibiti mara ambazo unaonyeshwa tangazo na vile vile kusaidia kupima ufanisi wa matangazo yanayoshirikiwa na Spotify. Vidakuzi hivi huweka kumbukumbu kuwa umetembelea tovuti na maelezo haya yanaweza kushirikiwa na mashirika mengine kama vile watangazaji. Vile vile, Spotify inaweza kushiriki data chache na mifumo mingine ili kutangaza ofa, vipengele au matoleo mapya ya Spotify kwenye mifumo hiyo mingine. Usiporuhusu vidakuzi hivi bado utaonyeshwa matangazo lakini hayatawekewa mapendeleo mengi ili yakufae zaidi. |
3. Chaguo za kudhibiti vidakuzi na matangazo yanayotokana na mambo yanayokuvutia
Mipangilio ya Kivinjari cha Wavuti
Unaweza kutumia mipangiio ya kivinjari chako cha wavuti kukubali, kukataa au kufuta vidakuzi. Ili ufanye hivi, fuata maelekezo yanayotolewa na kivinjari chako (kwa kawaida yanapatikana katika mipangilio ya 'Usaidizi', 'Zana' au 'Badilisha').
Tafadhali kumbuka kuwa ukiweka mipangilio ya kivinjari chako ikatae vidakuzi, huenda usiweze kutumia vipengele vyote vya tovuti ya Spotify. Ili upate maelezo zaidi, unaweza kutembelea www.allaboutcookies.org.
Vitambulishi vya Vifaa vya Mkononi
Huenda mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako cha mkononi ukakuruhusu kujiondoa kwenye matangazo ya kulenga au kubadilisha 'vitambulishi vyako vya simu'. Kwa mfano, unaweza kutumia mipangilio ya 'Ruhusu Programu Zitume Ombi ili Zifuatilie' kwenye vifaa vya iOS au mipangilio ya 'Jiondoe kwenye Matangazo Yanayolingana na Mambo Yanayokuvutia' kwenye vifaa vya Android. Mipangilio hii hukuruhusu kudhibiti matumizi ya maelezo kuhusu unavyotumia programu zako kwa madhumuni ya kukuonyesha matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia.
Kuwasha au Kuzima Matangazo Ya Kulenga
Katika Huduma ya Spotify, unaweza kujiondoa ili usipokee matangazo ya kulenga. Ili ufanye hivyo, zima kipengele cha matangazo ya kulenga katika ukurasa wa Faragha ya Akaunti kwenye Akaunti yako ya Spotify. Ukizima kipengele cha matangazo ya kulenga, Spotify itaacha kushiriki maelezo yako na washirika wengine wa matangazo. Spotify pia itaacha kutumia maelezo yake kukuonyesha matangazo ya kulenga. Huenda bado ukaona matangazo katika Huduma kulingana na maelezo yako ya usajili kwenye Spotify na jinsi unavyotumia Spotify katika wakati halisi. Hata hivyo, huenda matangazo haya yasikufae sana.
Baadhi ya matangazo ya kulenga yanayoonyeshwa na Spotify, au na mtoa huduma kwa niaba yetu, yanaweza kuwa ni pamoja na aikoni ya 'Ad Choices'. Aikoni hii, au zana inayofanana nayo, hukuruhusu kujiondoa ili usipokee matangazo ya kulenga. Unaweza kubofya aikoni ya Adchoices au utembelee www.aboutads.info ili:
- upate maelezo kuhusu ukusanyaji na matumizi ya maelezo kuhusu shughuli zako za mtandaoni kwa matangazo ya kulenga; au
- ujiondoe ili data yako isitumike kwa matangazo ya kulenga na kampuni zinazoshiriki katika Digital Advertising Alliance (DAA).
4. Masasisho ya Sera hii
Huenda tukafanya mabadiliko katika Sera hii mara kwa mara.
Tunapofanya mabadiliko ya msingi kwenye Sera hii, tutakupa taarifa. Aina ya taarifa itategemea njia inayofaa katika mazingira halisi. Kwa mfano, tunaweza kuonyesha taarifa dhahiri ndani ya Huduma ya Spotify au kukutumia barua pepe au arifa kwenye kifaa.
5. Jinsi ya kuwasiliana nasi
Asante kwa kusoma Sera hii. Kwa maswali au hoja zozote kuhusu Sera hii, wasiliana na Afisa wetu wa Ulinzi wa Data kupitia mojawapo ya njia hizi:
- barua pepe privacy@spotify.com
- tuandikie kupitia: Spotify AB, Regeringsgatan 19, 111 53 Stockholm, Uswidi
Tunatumai unafurahia Spotify!
© Spotify AB.