Kuna hatua mbalimbali ambazo Spotify huchukua kuhusiana na maudhui yanayokiuka Kanuni za Mfumo, sheria husika au ambayo huenda yana mada nyeti. Hatua hizi ni pamoja na kuondoa maudhui, kudhibiti uwezo wa maudhui kutambulika, kudhibiti uwezo wa maudhui kuchuma mapato na/au kuwekea maudhui angalizo la ushauri.
Tunazingatia vigezo mbalimbali tunapobaini hatua za kuchukua, kama vile muktadha wa mada mahususi au tukio la sasa na kiwango na/au mara ambazo ukiukaji umejirudia tuliobaini kama sehemu ya mchakato wetu wa ukaguzi. Tunatumia mbinu mbalimbali za utambuzi wa binadamu na wa kialgoriti ili kusaidia kutambua maudhui ambayo yanahitaji kuchukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na ripoti za watumiaji. Matumizi yoyote mabaya ya michakato yetu, ikiwa ni pamoja na kuripoti kunakolenga maudhui au mtumiaji yule yule, kunaweza kupunguza uwezo wako wa kuwasilisha maombi katika siku zijazo.
Ikiwa maudhui yanakiuka Kanuni zetu za Mfumo, huenda yakaondolewa kwenye Spotify.
Ukiukaji wa mara kwa mara au uliokithiri wa Kanuni za Mfumo unaweza kusababisha akaunti isimamishwe au ifungwe kabisa. Kumbuka kuwa hatua hii pia inaweza kujumuisha akaunti zote zinazohusiana na zinazoshirikiana na Spotify.
Katika hali ambazo maudhui yanakaribia kukiuka lakini hayakidhi vigezo vya kuondolewa kwa mujibu wa Kanuni zetu za Mfumo, tunaweza kuchukua hatua za kudhibiti uwezo kufikiwa na hadhira. Ingawa maudhui yataendelea kupatikana kwenye Spotify, yanaweza:
Katika nyakati za hatari zaidi mara nyingi kuna tishio kubwa la maudhui hatari mtandaoni, kwa mfano, wakati wa uchaguzi, migogoro ya vurugu au matukio ya vifo vingi. Kwa kutambua hili, Spotify inaweza kuchukua hatua za ziada wakati wa matukio kama hayo, kama vile kudhibiti ufikiaji wa aina fulani za maudhui na/au kuangazia nyenzo zinazoaminika na kwa wakati unaofaa.
Si maudhui yote yanastahiki kuchuma mapato kwenye Spotify. Pamoja na Kanuni za Mfumo, maudhui ambayo ungependa kuyatumia kuchuma mapato yatakaguliwa kulingana na Sera zetu za Uchumaji Mapato.
Katika hali ambazo muktadha zaidi huenda ukahitajika kuhusu mada husika, angalizo la ushauri kuhusu maudhui huenda likawekwa ili kuongeza maelezo yanayofaa na/au kuelekeza watumiaji kwenye nyenzo zinazoaminika na kwa wakati unaofaa.
Spotify ni jumuiya ya kimataifa na inaheshimu sheria za nchi tunakotoa huduma. Ni sharti watumiaji watii sheria na kanuni zinazotumika. Maudhui ambayo hayakiuki Kanuni zetu za Mfumo yanaweza bado yakawekewa vizuizi katika nchi au eneo mahususi ambako maudhui yamekiuka sheria husika.
Chaguo za kukatia rufaa maamuzi ya maudhui hutofautiana kulingana na eneo, na tutaendelea kupanua uwezo wetu.
Ikiwa hukubaliani na uamuzi wa utekelezaji uliochukuliwa dhidi ya maudhui yako au kutokana na ripoti yako, unaweza kuwasilisha rufaa. Ili ufanye hivi, tafadhali fuata maelekezo katika arifa uliyopokea kutoka Spotify.