Spotify® Premium for Students

Sheria na Masharti

Ilianza kutumika tarehe 23/02/2021

TAFADHALI SOMA MASHARTI HAYA KWA MAKINI NA KIKAMILIFU. YANA MASHARTI NA VIKWAZO FULANI KUHUSU UPATIKANAJI WA USAJILI WA SPOTIFY PREMIUM FOR STUDENTS NA PIA TAARIFA KUHUSU KITAKACHOTENDEKA BAADA YA USAJILI WAKO WA SPOTIFY PREMIUM FOR STUDENTS KUKAMILIKA.

1. Utangulizi.

Usajili wako wa Spotify Premium for Students ("Usajili wa Premium for Students") unafanywa kupatikana na Spotify (kama ilivyofafanuliwa katika Sheria na Masharti ya Spotify), kulingana na sheria na masharti haya ("Masharti ya Usajili wa Premium for Students"). Usajili wa Premium for Students huwezesha Wanafunzi Wanaostahiki (kama ilivofafanuliwa hapa chini) kujisajili kwa Spotify Premium - aina ya Usajili wa Kulipiwa, kama ilivyofafanuliwa katika Sheria na Masharti ya Spotify, ("Spotify Premium Service") - kwa bei ya kila mwezi yenye punguzo iliyotangazwa.

2. Ustahiki.

  1. Matumizi ya Usajili wa Premium for Students uko wazi tu kwa wanafunzi walio kwenye taasisi za elimu ya juu zilizoidhinishwa ambao wanatimiza ustahiki wa ziada ulioelezwa hapa chini ("Wanafunzi Wanaostahiki").
  2. Utahitajika kuwasilisha taarifa fulani inayotutosha kuthibitisha kuwa wewe ni Mwanafunzi Anayestahiki. Hii ni pamoja na jina lako, taasisi halali ya elimu, anwani ya barua pepe, tarehe ya kuzaliwa na/au nyaraka nyingine ("Taarifa ya Kustahiki"), na pia maelezo yako ya malipo.
  3. Tutatumia huduma za SheerID, Inc. ("SheerID"), mhusika mwingine ili kusaidia kuthibitisha Taarifa yako ya Kustahiki. SheerID itachakata Taarifa yako ya Kustahiki, kwa mujibu wa sera ya faragha ya SheerID na kututhibitishia hali yako ya mwanafunzi. Spotify pia inaweza kupokea Taarifa yako ya Kustahiki na kushiriki taarifa hiyo na SheerID. Tuna haki ya kuamua ikiwa wewe ni Mwanafunzi Anayestahiki kwa busara yetu binafsi. Spotify itahifadhi jina lako, jina la taasisi ya elimu, anwani ya barua pepe na tarehe ya kuzaliwa.
  4. Kwa kutuma ombi la Usajili wa Premium for Students na kuwasilisha Taarifa ya Kustahiki, unaelewa kwamba taarifa yoyote ya binafsi tunayoweza kukusanya na kuchakata chini ya Usajili wako wa Premium for Students itafanywa kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Spotify. Hii itajumuisha kukusanya, kuhifadhi na kushiriki na wahusika wengine jina, jina la taasisi ya elimu, anwani ya barua pepe na tarehe yako ya kuzaliwa kwa madhumuni ya kutathmini ustahiki wako wa Usajili wa Premium for Students.

3. Kufikia Usajili wa Premium for Students.

  1. Endapo tutakuchagua kuwa Mwanafunzi Anayestahiki, kwa kuendelea kujisajili kwenye Usajili wa Premium for Students, unakiri na kukubali Sheria na Masharti ya Spotify na Masharti haya ya Usajili wa Premium for Students.
  2. Ikiwa tayari umejisajili kwa Spotify Premium Service wakati unapokamilisha uthibitishaji wako kama Mwanafunzi Anayestahiki na mchakato wa usajili, Mwezi wa kwanza wa Punguzo (jinsi ilivyofafanuliwa hapa chini) utaanza baada ya kuisha kwa kipindi cha Spotify Premium Service au Unlimited Service (jinsi ilivyofafanuliwa katika Sheria na Masharti ya Utumiaji wa Spotify) ambao umeshalipia tayari. Ikiwa wewe ni mtumiaji wa Bila malipo au mpya wa Spotify, Mwezi wa Punguzo utaanza baada ya wewe kuamilisha ufikiaji wako kwenye Usajili wa Premium for Students. Unaweza pekee kusajiliwa kwenye Usajili wa Premium for Students chini ya akaunti moja ya Spotify.

4. Muda na kughairi.

  1. Wanafunzi Wanaostahiki wanaweza kupokea usajili wa kila mwezi uliopunguzwa na uliotangaza kwa Spotify Premium Service kwa kila mwezi (kila "Mwezi wa Punguzo") hadi kipindi cha miezi kumi na miwili (12) inayofuatana ("Kipindi cha Punguzo"). Wanafunzi Wanaostahiki wanaweza kuamilisha hadi Vipindi vitatu (3) vya ziada vya Punguzo kwao wenyewe kwa kuwasilisha tena Taarifa zao za Kuhitimu kwa ajili ya kuthibitishwa tena.
  2. Wanafunzi Wanaostahiki ambao wamefikisha kiwango cha juu cha muda kwenye Usajili wa Premium for Students jinsi ilivyofafanuliwa katika sehemu ya 4A, hapo juu, watahamishwa moja kwa moja hadi kwenye usajili wa Spotify Premium Service kwa msingi wa kila mwezi unaorudiarudia, kwa gharama kamili ya saa hizo, baada ya kuisha kwa Kipindi cha Punguzo cha wakati huo. Ikiwa hutaki usajili wako kuhamishwa hadi kwa Spotify Premium Service mwishoni mwa Kipindi cha Punguzo, unaweza kughairi usajili wako wakati wowote kabla ya Kipindi cha Punguzo kufika mwisho kwa kufuata hatua zilizoorodheshwa hapa chini.
  3. Unaweza kughairi usajili wako kwenye Usajili wa Premium for Students wakati wowote kwa kuingia katika akaunti yako ya Spotify account na kufuata maagizo kwenye ukurasa wa Akaunti, au kwa kubofya hapa na kufuata maagizo. Kughairi kutaanza kufanya kazi wakati wa kuisha kwa Mwezi wa Punguzo wa wakati huo.
  4. Ikiwa unaghairi usajili wako kwenye Usajili wa Premium for Students kwa saa yoyote wakati wa Kipindi cha Punguzo, unaweza kuamilisha tena usajili wako katika wakati wa Kipindi hicho hicho cha Punguzo. Baada ya kuamilisha tena utapokea idadi iyo hiyo ya Miezi ya Punguzo inayosalia katika Kipindi hicho cha Punguzo jinsi ambavyo ungepata, ikiwa usingeghairi usajili wako. Kipindi chako cha Punguzo cha wakati huo kila mara kitakwisha miezi kumi na miwili mtawalia baada ya wakati ulipojisajili au mara ya mwisho ulipothibitisha, jinsi hali ilivyo. Vipindi vya Punguzo haviwezi kurefushwa kwa sababu yoyote. Kwa mfano, ikiwa Usajili wako wa Premium for Students unaanza katika mwanzo wa Januari, utakuwa umeamilisha Kipindi cha Punguzo kwa miezi kumi na miwili (12) mtawalia hadi mwisho wa Desemba. Ukighairi usajili wako mnamo mwezi wa Machi wa mwaka huo na kuuamilisha tena mnamo mwezi wa Agosti, Kipindi cha Punguzo kitasalia vivyo hivyo na kuisha mwishoni mwa mwezi wa Desemba mwaka uo huo.
  5. Pia unaweza kufuta akaunti yako ya Spotify wakati wowote kwa kuingia katika akaunti yako ya Spotify na kufuata maagizo kwenye ukurasa wa Akaunti au bofya hapa na kufuata maagizo.

5. Upatikanaji wa Usajili wa Premium for Students.

Spotify ina haki ya kukatiza, kuboresha au kusimamisha Usajili wa Premium for Students kikamilifu au kisehemu wakati wowote na kwa sababu yoyote. Baada ya muda kama huo, Spotify haitawajibika kuruhusu usajili wowote wa ziada kwenye Usajili wa Premium for Students.

6. Malipo.

Ikiwa Spotify inaongeza ada yake ya kila mwezi kwenye Usajili wa Premium for Students mbeleni, tutatoa notisi na nafasi ya kughairi. Ikiwa ada haighairiwi, mabadiliko ya bei yataanza kufanya kazi katika mwanzo wa Mwezi wa Punguzo unafuata tarehe ya mabadiliko ya bei. Unaweza kughairi usajili wako kwenye Usajili wa Premium for Students wakati wowote kabla ya mwanzo wa mzunguko mpya wa malipo. Kwa kukosa kughairi na kuendelea kutumia huduma ya Spotify baada ya mabadiliko ya bei kuanza, unakubali kulipishwa bei mpya.

Si kadi za kulipia kabla wala kadi za zawadi za Spotify zinaweza kutumika kama njia halali ya malipo kwa ofa hii.

Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501