Sheria na Masharti ya Spotify

 1. Utangulizi

 2. Huduma ya Spotify Tunayotoa.

 3. Matumizi Yako ya Huduma ya Spotify

 4. Maudhui na Hakibunifu

 5. Usaidizi, Maelezo, Maswali na Malalamishi ya Mteja

 6. Matatizo na Migogoro

 7. Kuhusu Masharti haya

1. Utangulizi

Tafadhali soma Sheria na Masharti haya ("Masharti" haya) kwa makini kwa kuwa yanaongoza matumizi yako ya (ambayo yanajumuisha ufikiaji wa) huduma za Spotify zilizoboreshwa kwa ajili ya kutiririsha muziki na maudhui mengine, ikiwemo tovuti zetu zote na programu zinazojumuisha au zinazounganisha Masharti haya (kwa pamoja, "Huduma ya Spotify") na muziki, video, podikasti zozote, au nyenzo nyingine ambazo zinapatikana kupitia Huduma ya Spotify ("Maudhui").

Matumizi ya Huduma ya Spotify yanaweza kuzingatia sheria na masharti yanayowasilishwa na Spotify, ambayo yamejumuishwa na rejeo hili ndani ya masharti haya.

Kwa kujisajili kwa, au vinginevyo kutumia Huduma ya Spotify, unakubali Masharti haya. Usipokubali Masharti haya, basi hupaswi kutumia Huduma ya Spotify wala kufikia Maudhui yoyote.

Mtoa Huduma

Masharti haya ni kati yako na Spotify AB, Regeringsgatan 19, 111 53, Stockholm, Sweden.

Matakwa ya umri na ustahiki

Ili kutumia Huduma ya Spotify na kufikia Maudhui yoyote, unahitaji (1) kuwa na umri wa miaka 13 (au umri wa chini zaidi unaokubalika katika nchi yako) au zaidi, (2) kuwa na idhini ya mzazi au mlezi ikiwa wewe ni mtoto katika nchi yako; (3) uwe na mamlaka ya kuingia kwenye mkataba wa kubana nasi na huzuiwi kufanya hivyo chini ya sheria husika, na (4) uwe unakaa katika nchi ambayo Huduma inapatkana. Pia unaahidi kuwa maelezo yoyote ya usajili unayowasilisha kwa Spotify ni ya kweli, sahihi na kamili na unakubali kuyahifadhi hivyo nyakati zote. Ikiwa wewe ni mtoto katika nchi yako, mzazi au mlezi wako atahitaji kuingia kwenye Masharti haya kwa niaba yako. Unaweza kupata maelezo ya ziada kuhusu matakwa ya umri wa chini zaidi katika mchakato wa usajili. Usipotimiza matakwa ya umri wa chini zaidi basi Spotify haitaweza kukusajili kama mtumiaji.

2. Huduma ya Spotify Tunayotoa.

Machaguo ya Huduma ya Spotify

Tunatoa machaguo mbalimbali ya Huduma ya Spotify. Machaguo fulani ya Huduma ya Spotify yanatolewa bila malipo, huku mengine yakihitaji malipo kabla hayajafikiwa ("Usajili wa Kulipiwa"). Pia tunaweza kutoa mipango maalum ya mauzo, uanachama, au huduma, kwa kujumuisha ofa za bidhaa za mhusika mwingine na huduma. Hatuwajibikii bidhaa na huduma zinazotolewa na wahusika wa tatu kama hao.

Huduma Zisizo na Kikomo zinaweza kukosa kupatikana kwa watumiaji wote. Tutafafanua ni huduma gani zinazopatikana kwako wakati unapojisajili kwa huduma. Ikiwa unaghairi usajili wako kwenye Huduma Zisizo na Kikomo, au ikiwa usajili wako kwenye Huduma Zisizo na Kikomo unachachawizwa (kwa mfano, ikiwa unabadilisha maelezo yako ya malipo), unaweza kushindwa kujisajili tena kwenye Huduma Zisizo na Kikomo. Fahamu kwamba Huduma Zisizo na Kikomo zinaweza kukatizwa mbeleni, ambapo katika hiyo hali hutaweza kulipishwa kwa Huduma.

Majaribio

Mara kwa mara, sisi au wengine kwa niaba yetu wanaweza kutoa majaribio ya Usajili wa Kulipiwa kwa kipindi maalum bila kulipia au kwa kiwango kilichopunguzwa ("Jaribio"). Kwa kutumia Huduma ya Spotify kupitia Jaribio, unakubali Masharti ya Ofa ya Matangazo ya Spotify Premium.

Programu za Mhusika Mwingine, Vifaa na Programu Huria

Huduma ya Spotify inaweza kujumuishwa na, au vinginevyo inaweza kutumia programu, tovuti na huduma za mhusika mwingine ("Programu za Mhusika Mwingine") na kompyuta za binafsi, vifaa vya mkononi, tableti, vifaa vya kuvaa, spika za mhusika mwingine na vifaa vingine ("Vifaa"). Matumizi yako ya Programu na Vifaa hivyo vya Mhusika Mwingine yanaweza kutii masharti, sheria na sera za ziada ulizopewa na mhusika mwingine husika. Spotify haihakikishi kuwa Programu na Vifaa vya Mhusika Mwingine vitaoana na Huduma ya Spotify.

Vikomo na Maboresho kwa Huduma

Tunatumia utunzaji na ujuzi wa busara kuhakikisha kuwa Huduma ya Spotify inaendelea na kukupa hali ya utumiaji wa sauti iliyoboreshwa. Hata hivyo, ofa zetu za huduma na upatikanaji wazo vinaweza kubadilika mara kwa mara na kutii sheria husika, bila kuwajibika kwako; kwa mfano:

 • Huduma ya Spotify inaweza kukumbana na uchachawizaji wa muda mfupi kutokana na matatizo ya ufundi, matengenezo au kujaribu, au masasisho, ikiwemo yale yanayohitajika ili kuakisi mabadiliko katika sheria husika na matakwa ya udhibiti.
 • Tunalenga kuzinduka na kuboresha Huduma zetu mara kwa mara na tunaweza kubadilisha, kuahirisha, au kusimamisha (kabisa au kwa muda mfupi) kutoa Huduma ya Spotify yote au kidogo (ikiwemo utendaji, vipengele, mipango ya usajili na ofa fulani za matangazo).
 • Spotify haina wajibu wa kutoa maudhui yoyote mahususi kupitia Huduma ya Spotify na Spotify au wamiliki wake husika wanaweza kuondoa nyimbo, video, podikasti fulani na Maudhui mengine bila ilani.

Ikiwa una ada za kulipa kabla moja kwa moja kwa Spotify kwa Usajili wa Kulipiwa ambao Spotify inasimamisha kabla ya mwisho wa Kipindi chako cha Kulipa Awali (kama sharti hilo lilivyofafanuliwa katika sehemu ya Malipo na kughairi hapa chini), Spotify itakurejeshea ada ulizolipa kabla kwa Kipindi cha Usajili wa Kulipiwa wa sasa baada ya usimamishaji kama huo. Maelezo ya akaunti na bili yako lazima yasasishwe ili tukurejeshee malipo.

Spotify haina dhima kwako, wala jukumu lolote la kukurejeshea pesa, kuhusiana na kutokuwepo au kasoro za intaneti au huduma nyingine zinazosababishwa na hatua za mamlaka ya serikali, wahusika au matukio mengine ambayo ni zaidi ya uwezo wetu.

3. Matumizi Yako ya Huduma ya Spotify

Kufungua akaunti ya Spotify

Huenda ukahitajika kufungua akaunti ya Spotify ili utumie Huduma ya Spotify yote au kidogo. Jina la mtumiaji na nenosiri lako ni ya matumizi yako ya binafsi pekee na yanapaswa kuwekwa kwa siri. Unaelewa kuwa unawajibika kwa matumizi yote (kwa kujumuisha matumizi yoyote yasiyoruhusiwa) ya jina lako la mtumiaji na nenosiri. Ifahamishe timu ya Huduma kwa Wateja mara moja ikiwa jina la mtumiaji au nenosiri limepotea au kuibwa, au ikiwa unaamini kuna ufikiaji usioidhinishwa wa akaunti yako.

Spotify inaweza kudai tena, au kuhitaji ubadilishe jina lako la mtumiaji kwa sababu yoyote.

Haki zako za kutumia Huduma ya Spotify

Ufikiaji wa Huduma za Spotify

Kulingana na uzingatiaji wako wa Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti mengine yoyote husika), tunakupa ruhusa isiyo ya kikomo, isiyo ya kipekee na isiyobatilika ili utumie kwa njia ya binafsi na isiyo ya biashara Huduma ya Spotify na Maudhui (kwa pamoja, "Ufikiaji"). Ufikiaji huu utasalia kutumika isipokuwa na hadi ukatizwe na wewe au Spotify. Unakubali kuwa hutasambaza tena wala kuhamisha Huduma ya Spotify wala Maudhui.

Programu za Spotify na Maudhui yamepewa leseni, hayauzwi wala kuhamishwa kwako na Spotify na wataoji wake wa leseni wanadumisha umiliki nakala zote za programu za Spotify na Maudhui hata baada ya usakinishaji kwenye Vifaa vyako.

Hakimiliki za Spotify

Huduma ya Spotify na Maudhui ni mali ya Spotify au watoaji leseni wa Spotify. Alama za biashara za Spotify, alama za huduma, majina ya biashara, logo, majina ya vikoa na vipengele vingine vyovyote vya chapa ya Spotify ("Vipengee vya Chapa ya Spotify") ni mali ya Spotify au watoaji wake wa leseni. Masharti haya hayakupi haki zozote za kutumia Vipengele vya Chapa ya Spotify iwe kwa utumiaji wa kibiashara au usio wa kibiashara.

Unakubali kufuata Miongozo ya Mtumiaji wa Spotifyna kutotumia Huduma ya Spotify, Maudhui, au sehemu yoyote kwa njia yoyote isiyokubaliwa moja kwa moja na Masharti haya.

Malipo na kughairi

Bili

Unaweza kununua Usajili wa Kulipiwa moja kwa moja kutoka Spotify au kulipia mhusika mwingine kwa:

 • kulipa ada ya usajili mapema kila mwezi au vipindi vingine vya kujirudia ulivyofahamishwa kabla ya ununuzi wako; au
 • malipo ya mapema yanayokupa ufikiaji wa Huduma ya Spotify kwa kipindi mahususi ("Kipindi cha Kulipia Kabla").

Viwango vya kodi vinakokotelwa kulingana na maelezo unayotoa na kiwango kinachotumika wakati wa ada yako ya kila mwezi.

Ukinunua ufikiaji wa Usajili wa Kulipiwa kupitia mhusika mwingine, sheria na masharti tofauti na mhusika huyo mwingine yanaweza kutumika kwenye matumizi yako ya Huduma ya Spotify mbali na Masharti haya. Ukinunua Usajili wa Kulipiwa kwa kutumia msimbo, kadi ya zawadi, ofa ya kulipia kabla, au ofa inayotolewa au kuuzwa na au kwa niaba ya Spotify kwa ajili ya ufikiaji wa Usajili wa Kulipiwa ("Misimbo"), unakubali Masharti ya Kadi ya Spotify.

Mabadiliko ya bei na kodi

Spotify inaweza kubadilisha bei ya Usajili wa Kulipiwa mara kwa mara, kwa kujumuisha ada za usajili wa kurudiarudia, Kipindi cha Malipo ya Kabla (kwa vipindi ambavyo havijalipiwa), au Misimbo (iliyofafanuliwa hapo juu), na tutakufahamisha mapema kuhusu mabadiliko yoyote ya bei. Mabadiliko ya bei yataanza kufanya kazi mwanzoni mwa kipindi cha usajili unaofuata tarehe ya mabadiliko ya bei. Kwa kuzingatia sheria husika, kwa kuendelea kutumia Huduma ya Spotify baada ya mabadiliko ya bei kuanza kutumika, utakuwa umeikubali bei mpya. Ikiwa hukubali mabadiliko ya bei, unaweza kukataa mabadiliko kwa kuondoa usajili wako kwenye Usajili wa Kulipiwa kabla ya kuanza kutumika kwa mabadiliko ya bei.

Viwango vya kodi vinalingana na viwango vinavyotumika wakati wa ada yako ya kila mwezi. Viwango hivi vinaweza kubadilika baada ya muda kulingana na matakwa ya kodi ya ndani ya nchi, jimbo, himaya au hata jiji lako. Badiliko lolote la kiwango cha Kodi litatumika kiotomatiki kulingana na maelezo ya akaunti unayotoa

Kujisajili Upya na Kughairi

Bila kujumuisha Usajili wa Kulipiwa kwa Kipindi cha Kulipia Kabla, malipo yako kwenye Spotify au mhusika mwingine ambapo ulinunua Usajili wa Kulipiwa yatafanya usajili upya mwishoni mwa kipindi cha usajili husika, isipokuwa ughairi Usajili wako wa Kulipia kabla ya mwisho wa kipindi cha usajili wa sasa. Wasiliana na timu yetu ya Usaidizi kwa Wateja hapa kwa maagizo kuhusu jinsi ya kughairi. Kughairiwa kutaanza kufanya kazi siku moja baada ya siku ya mwisho ya kipindi cha usajili wa sasa, na utarudishwa nyuma kwenye toleo la bila malipo la Huduma ya Spotify. Hatutoi marejesho ya fedha wala mikopo kwa vipindi vyovyote vya usajili mdogo, isipokuwa kama ilivyoelezwa katika Masharti haya.

Ikiwa umenunua Usajili wa Kulipiwa kwa kutumia Msimbo, usajili wako utakatizwa mara moja mwishoni mwa kipindi kilichotajwa kwenye Msimbo, au wakati kuna salio lisilotosha kulipia Huduma ya Spotify.

Haki ya kujiondoa

Ukijisajili kwa Jaribio, unakubali kwamba haki ya kujiondoa kwa Usajili wa Kulipiwa ambao unapata Jaribio itakwisha siku kumi na nne (14) baada ya kuanza Jaribio. Usipoghairi Usajili wa Kulipiwa kabla ya Jaribio kuisha, unapoteza haki yako ya kujiondoa na unaidhinisha Spotify kukulipisha moja kwa moja bei mliyokubaliana kila mwezi hadi utakapoghairi Usajili wa Kulipiwa. Kwa matoleo chini ya siku kumi na nne (14), unatuidhinisha kwa njia ya maandishi kukupa huduma ya kulipia mara tu baada ya mwisho wa Jaribio lako na kwamba kutoka wakati huo unapoteza haki yako ya kujiondoa.

Ukinunua Usajili wa Kulipiwa bila Jaribio, unakubali kuwa una siku kumi na nne (14) baada ya ununuzi wako kujiondoa kwa sababu yoyote na lazima utulipe kwa huduma ulizopewa hadi wakati unatuambia kwamba umebadilisha nia yako. . Unatukubalia kwa njia ya maandishi kukupa huduma mara tu baada ya ununuzi wako, kuwa unapoteza haki yako ya kujiondoa na unaidhinisha Spotify kukutoza kiotomatiki kila mwezi hadi ughairi.

Miongozo ya Mtumiaji

Tumeunda miongozo ya kutumia Huduma ya Spotify, kuhakikisha kuwa Huduma ya Spotify inaendelea kufurahiwa na kila mtu ("Miongozo ya Mtumiaji ya Spotify"). Kwa kutumia Huduma ya Spotify, lazima uzingatie Miongozo ya Mtumiaji ya Spotify na pia sheria na kanuni zote husika na uheshimu hakibinifu, faragha na haki nyingine za wahusika wengine.

Akaunti za Chapa

Ukifungua akaunti ya Spotify kwa niaba ya kampuni, shirika, taasisi, au chapa ("Chapa," na akaunti kama hiyo "Akaunti ya Biashara"), maneno "wewe" na "yako," kama yanavyotumika katika Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti mengine ya Spotify yaliyojumuishwa na rejeo lililo humu), yanahusu wewe na Chapa.

Ukifungua Akaunti ya Biashara, unawakilisha na unathibitisha kuwa umeidhinishwa kutoa ruhusa na leseni zote zinazotolewa katika Masharti (ikiwemo sheria na masharti mengine husika ya Spotify) na kuibana Chapa kwenye Masharti haya.

Chapa inaweza kufuata watumiaji na kuunda na kushiriki orodha za muziki, mradi Chapa haichukui hatua yoyote ambayo inamaanisha kuidhinisha au uhusiano wa kibiashara kati ya Chapa na mtumiaji anayefuatwa, msanii, mtunzi wa nyimbo, au mtu mwingine yeyote, isipokuwa kama Chapa kipekee imepata haki za kuashiria uthibitisho kama huo. Kwa kuongezea, Chapa lazima ziwe wazi kwa watumiaji wetu juu ya kufichua uungwaji mkono wowote au maanani yaliyotolewa kwa wasanii, watunzi wa nyimbo, watumiaji, au mtu mwingine yeyote na lazima izingatie sheria, masharti na kanuni zote zinazotumika wakati wa kushiriki shughuli zilizotajwa hapo juu.

Hamisha udhibiti na vikwazo

Bidhaa za Spotify zinaweza kuwa chini ya sheria na masharti ya Marekani ya udhibiti wa uhamishaji au sheria kama hizo zinazotumika katika mamlaka nyingine, kwa kujumuisha Masharti ya Usimamizi wa Uhamishaji ("EAR") yanayodumishwa na Marekani. Idara ya Biashara, biashara na vikwazo vya kiuchumi vinavyodumishwa na Ofisi ya Idara ya Hazina ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ("OFAC"), na Kanuni za Usafiri wa Kimataifa ("ITAR") zinazodumishwa na Idara ya Jimbo. Unathibitisha kuwa wewe (1) hauko katika nchi yoyote ambayo Marekani imezuia bidhaa au imetumia vikwazo vyovyote vya kiuchumi; na (2) sio mtu aliyekataliwa kama ilivyoainishwa katika sheria yoyote inayotumika ya kuuza nje au kuuza nje tena au kanuni au sheria zinazofanana zinazotumika katika mamlaka mengine au vinginevyo zilizoorodheshwa kwenye orodha yoyote ya ya serikali ya Marekani au watu waliowekewa vikwazo.

Unakubali kuzingatia sheria na kanuni zote husika za udhibiti wa uhamishaji na uhamishaji tena, ikiwemo bila kikomo kwenye vikwazo vya EAR na biashara na uchumi vinavyodumishwa na OFAC. Hasa, unakubali kwamba – hutatumia, kuuza, kuhamisha, kuuza nje, kuuza nje tena, kuhamisha, kugeuza, au vinginevyo kutupa bidhaa yoyote, programu, au teknolojia (pamoja na bidhaa zinazotokana na au kulingana na teknolojia hiyo) iliyopokelewa kutoka Spotify chini ya Masharti hata hadi eneo, taasisi au mtu au kwa matumizi yoyote yaliyokatazwa na EAR, vikwazo vya biashara na uchumi vinavyodumishwa na OFAC, au sheria au kanuni zozote zinazofaa za Marekani au mamlaka nyingine yoyote bila kupata idhini yoyote ya mapema inayohitajika kutoka kwenye mamlaka yanayofaa ya serikali kama inavyotakiwa na sheria na kanuni hizo.

4. Maudhui na Hakibunifu

Maudhui ya mtumiaji

Maudhui unayochapisha kwenye huduma

Watumiaji wa Spotify wanaweza kuchapisha, kupakia, au vinginevyo kuchangia maudhui kwenye Huduma ya Spotify ("Maudhui ya Mtumiaji"). Ili kuwa na uhakika, "Maudhui ya Mtumiaji" ni pamoja na maelezo, nyenzo na maudhui mengine yanayoongezwa, kuundwa, kupakiwa, kuwasilishwa, kusambazwa, au kuchapishwa kwenye Huduma ya Spotify (ikiwemo kwenye Jamii ya Usaidizi ya Spotify) na watumiaji.

Unawajibikia binafsi Maudhui yote ya Mtumiaji unayochapisha.

Unaahidi kwamba, kulingana na Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayochapisha kwenye Spotify, (1) unamiliki au una haki ya kuchapisha Maudhui hayo ya Mtumiaji; (2) Maudhui hayo ya Mtumiaji, au matumizi yake na Spotify kulingana na leseni iliyotolewa hapa chini, hayakiuki: (i) Masharti haya, sheria husika, au hakibunifu au haki nyingine za mhusika mwingine; au (ii) Maudhui hayo ya Mtumiaji hayadokezi ushirika wowote na au uidhinishaji wako au Maudhui yako ya Mtumiaji na Spotify au msanii, chapa, lebo yoyote au mtu au taasisi nyingine bila idhini ya maandishi ya mapema kutoka Spotify au mtu au taasisi hiyo.

Kwa kuchapisha na kushiriki Maudhui ya Mtumiaji au maelezo mengine kwenye Huduma ya Spotify, tafadhali fahamu kwamba maudhui na maelezo mengine yatafikiwa hadharani na yanaweza kutumiwa na kushirikiwa tena na wengine kwenye Huduma ya Spotify na kwenye wavuti wote, kwa hivyo tahadhari unapochapisha au kushiriki kwenye Huduma ya Spotify na uzingatie mipangilio ya akaunti yako. Spotify haiwajibikii kile ambacho wewe au wengine wanachapisha au wanashiriki kwenye Huduma ya Spotify.

Kufuatilia maudhui ya mtumiaji

Spotify inaweza, lakini haina jukumu la, kufuatilia au kupitia Maudhui ya Mtumiaji. Spotify ina haki ya kuondoa au kulemaza ufikiaji wa Maudhui yoyote ya Mtumiaji kwa sababu yoyote au bila sababu. Spotify inaweza kuchukuwa hatua bila notisi ya kabla kwako.

Leseni unazotupa

Maudhui ya Mtumiaji

Unahifadhi umiliki wa Maudhui yako ya Mtumiaji unapoyachapisha kwenye Huduma. Hata hivyo, ili tufanye Maudhui yako ya Mtumiaji yapatikane kwenye Huduma ya Spotify, tunahitaji leseni yenye kikomo kutoka kwako kwa ajili ya Maudhui hayo ya Mtumiaji. Kwa hivyo, unaipa Spotify leseni isiyo ya kipekee, ya kuhamisha, ya kugawa, isiyo ya mrabaha, iliyolipiwa kikamilifu, isiyobatilika ya duniani kote ili kuzalisha tena, kufanya kupatikana, kutekeleza na kuonyesha, kutafsiri, kurekebisha, kuunda kazi za mwigo, kusambaza na vinginevyo kutumia Maudhui yoyote ya Mtumiaji kupitia chombo chochote, yawe pekee au pamoja na Maudhui au nyenzo nyingine, kwa namna na kwa njia, mbinu au teknolojia yoyote, iwe inajulikana sasa au iundwe baadaye, kuhusiana na Huduma ya Spotify. Mahali inatumika na kwa kiwango cha sheria inayotumika, pia unakubali kuondoa na kutotekeleza "haki zozote za maadili" au haki kama hizo, kama vile haki yako ya kutambuliwa kama mwandishi wa Maudhui yoyote ya Mtumiaji, kwa kujumuish Maoni, na haki yako ya kukataa kutumiwa kwa Maufhui ya Mtumiaji kama hayo bila heshima.

Maoni

Ukitoa hoja, mapendekezo, au maoni mengine kuhusiana na matumizi yako ya Huduma ya Spotify au Maudhui yoyote ("Maoni"), Maoni hayo si ya siri na yanaweza kutumiwa na Spotify bila kikwazo na bila malipo kwako. Maoni yanazingatiwa kuwa aina ya Maudhui ya Mtumiaji chini ya Masharti haya.

Kifaa Chako.

Pia unatupa haki ya (1) kuruhusu Huduma ya Spotify kutumia kichakataji, kipimo data na maunzi ya programu kwenye Kifaa chako ili kuwezesha shughuli ya Huduma ya Spotify, (2) kukupa matangazo na maelezo mengine na kuruhusu wabia wetu wa biashara kufanya vivyo hivyo, inavyoruhusiwa kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Spotify.

Hali ya utumiaji wa maudhui

Katika sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify, Maudhui unayofikia, kwa kujumuisha uchaguzi na uwekaji wake, yanaweza kuathiriwa na uzingatiaji wa kibiashara, kwa kujumuisha makubaliano ya Spotify na wahusika wengine.

Maudhui mengine yaliyoruhusiwa na, kutolewa kwa, kuundwa na au vinginevyo kuwezeshwa kupatikana na Spotify (k.v. matangazo ya sauti) yanaweza kujumuisha matangazo na Spotify haiwajibikii matangazo yoyote kama hayo.

Madai ya ukiukaji

Spotify inaheshimu haki za wamiliki wa hakibunifu. Ikiwa unaamini kuwa Maudhui yoyote yanakiuka hakimiliki zako, tafadhali tazama Sera ya Hakimiliki ya Spotify.

5. Usaidizi, Maelezo, Maswali na Malalamishi ya Mteja

Jumuia ya Usaidizi wa Spotify

Jumuia ya Usaidizi wa Spotify ni mahali pa majadiliano na kubadilishana taarifa, vidokezo, na vifaa vingine vinavyohusiana na Huduma ya Spotify. Kwa kutumia Jumuia ya Usaidizi ya Spotify unakubali Masharti ya Jumuia.

Usaidizi, Maelezo, Maswali na Malalamishi ya Mteja

Kwa usaidizi wa wateja walio na maswali yanayohusiana na akaunti na malipo ("Maswali ya Usaidizi kwa Wateja"), tafadhali tumia rasilimali za Usaidizi kwa Wateja zilizoorodheshwa kwenye sehemu ya Kutuhusu ya tovuti yetu.

Ikiwa una swali lolote kuhusu Huduma ya Spotify au Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada ya Spotify yaliyojumuishwa humu), tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja wa Spotify kwa kutembelea sehemu ya Kutuhusu ya tovuti yetu.

Ikiwa unakaa katika Umoja wa Ulaya, unaweza pia kuwasilisha malalamiko kwenye jukwaa mkondoni kwa suluhisho mbadala la mzozo (jukwaa la ODR). Unaweza kupata jukwaa la ODR kupitia kiungo kifuatacho: https://ec.europa.eu/consumers/odr.

6. Matatizo na Migogoro

Kusimamisha na Kukomesha Huduma za Spotify

Masharti haya yataendelea kutumika kwako hadi itakapokomeshwa na wewe au Spotify. Spotify inaweza kukomesha Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada yaliyojumuishwa humu) au kusimamisha ufikiaji wako wa Huduma ya Spotify wakati wowote ikiwa tunaamini kwamba umekiuka Masharti haya, tukiacha kutoa Huduma ya Spotify au kipengee chochote cha nyenzo kwenye notisi inayofaa kwako, au tunapoamini ni muhimu kutii sheria husika. Ikiwa wewe au Spotify itakomesha Masharti haya, au ikiwa Spotify inasimamisha ufikiaji wako wa Huduma ya Spotify, unakubali kuwa Spotify haitakuwa na dhima wala wajibu kwako kulingana na sheria husika na (isipokuwa kama ilivyobainishwa katika Masharti haya) Spotify haitarejesha pesa zozote ambazo tayari umelipa. Unaweza kukomesha Masharti haya wakati wowote, ambapo huwezi kuendelea kufikia wala kutumia Huduma ya Spotify. Ili kujifunza jinsi ya kukomesha akaunti yako ya Spotify, tafadhali tumia rasilimali za Usaidizi kwa Wateja kwenye ukurasa wetu wa Kutuhusu.

Sehemu za 4 (Maudhui na Hakibunifu), 3 (Matumizi Yako ya Huduma ya Spotify), 2 (Huduma ya Spotify Tunayotoa), 6 (Matatizo na Migogoro), 7 (Kuhusu Masharti haya) humu, na pia sehemu nyingine zozote za Masharti haya ambazo lazima ziendelee kutumika hata baada ya ukomeshaji wa Masharti haya kwa njia ya wazi au hali yake ya asilia, hayatakomeshwa.

Makanusho ya hakikisho

Spotify itatoa Huduma ya Spotify kwa kutumia utunzaji na ujuzi unaofaa na kwa mujibu wa maelezo yoyote ya Huduma ya Spotify yanayotolewa na Spotify, hata hivyo, kulingana na hiyo, Huduma ya Spotify inatolewa na "kama ilivyo" na "inavyopatikana," bila mahakikisho ya aina yoyote, yawe ya bayana, yanayodokezwa, au ya sheria. Vilevile, Spotify na wamiliki wote wa maudhui wanakanusha mahakikisho yoyote ya bayana, ya kudokezwa na ya sheria kuhusu maudhui, ikiwemo mahakikisho ya ubora wa kuridhisha, uwezo wa kufanya biashara, ufaafu kwa madhumuni fulani, au kutokiuka. Si Spotify wala mmiliki yeyote wa maudhui anatoa udhamini kwamba huduma ya Spotify haina programu hasidi au vifaa vingine hatari. Kwa kuongezea, Spotify haifanyi uwakilishi wala haitoi udhamini, kuthibitisha, kuhakikisha, au kuwajibikia programu zozote za mhusika wa tatu (au maudhui yaliyomo), maudhui ya mtumiaji, vifaa au bidhaa nyingine yoyote au huduma inayotangazwa, inayouzwa au kutolewa na mhusika wa tatu kwenye au kupitia huduma ya Spotify au tovuti yoyote iliyotolewa kiungo, au iliyoonyeshwa kwenye bango lolote au utangazaji mwingine na Spotify haiwajibiki kwa biashara yoyote kati yako na watoaji wa huduma za mhusika wa tatu inayoendelea. Hakuna ushauri wala taarifa iwe ya maneno au kwa uandishi inayopatikana na wewe kutoka kwa Spotify itaunda udhmini wowote kwa niaba ya Spotify. Wakati unatumia huduma ya Spotify, unaweza kupata ufikiaji kwa vipengee vya kuchuja maudhui, lakini matumizi ya vipengee hivi bado yanaweza kusababisha maudhui ya kina kutolewa kwako na usitegemee vipengee kama hivyo kujuja maudhui yote ya kina. Sehemu hii inatumika kwa kiwango kikubwa zaidi kinachoruhusiwa na sheria inayotumika.

Baadhi ya mamlaka hayaruhusu uondoaji wa mahakikisho au vikomo vinavyodokezwa kwenye haki za sheria husika za mtumiaji, hivyo uondoaji na vikomo katika sehemu hii huenda visitumike kwako na hakuna kitakachoathiri haki zako za kisheria.

Kikomo cha Dhima na Wakati wa Kuwasilisha Dai

Kulingana na sheria husika, unakubali kuwa suluhisho lako la pekee kwa matatizo au kutoridhishwa na Huduma ya Spotify ni kusakinusha programu yoyote ya Spotify na kuacha kutumia Huduma ya Spotify. Wewe unakubali kuwa Spotify haina wajibu au uwajibikaji unaotokana na au kuhusiana na programu za mhusika wa tatu au maudhui hayo yaliyopatikana kupitia au kwa kuungana na Huduma ya Spotify, na wakati uhusiano wako na programu kama hizo za mhusika wa tatu unaweza kuongozwa na makubaliano tofauti na hao wahusika wa tatu, utatuzi wako wa pekee na binafsi, kuhusiana na Spotify, kwa matatizo yoyote au kutoridhika na programu za mhusika wa tatu, au maudhui yaliyomo, ni kusakinua na/au kuacha kutumia programu kama hizo za mhusika wa tatu.

Hakuna wakati ambapo Spotify, maafisa, wadau, waajiriwa, mawakala, wakurugenzi, mashirika tanzu, warithi, wahawilishaji, wagawaji, au watoa leseni wake watawajibikia (1) uharibifu wowote usio wa moja kwa moja, maalum, unaoambatana, wa adhabu, funzo au unaoandamana; (2) hasara yoyote ya matumizi, data, biashara au faida (iwe moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja), katika kesi zote zinazotokana na matumizi ya au kutoweza kutumia Huduma ya Spotify, vifaa, programu za wahusika wengine, au maudhui ya programu ya mhusika mwingine; au (3) dhima ya jumla ya madai yote yanayohusiana na Huduma ya Spotify, programu za mhusika mwingine au maudhui ya programu ya mhusika mwingine zaidi ya (a) pesa ulizolipa Spotify wakati wa miezi kumi na miwili kabla ya dai la kwanza; au (b) $30.00. Dhima yoyote tuliyo nayo kwa hasara uliyopata ni ya hasara tu ambazo ziliweza kutabirika.

Kwa uthibitishaji, masharti haya hayazuii dhima ya Spotify kwa ajili ya udanganyifu, uwasilishaji mbaya wa udanganyifu, kifo au jeraha la binafsi kwa kiwango ambacho sheria husika itazuia kikomo kama hicho na kwa dhima nyingine yoyote ambayo, kwa sheria husika, huenda isiwe na kikomo wala kuondolewa.

**Isipokuwa pale ambapo vikwazo hivyo vinapigwa marufuku chini ya sheria husika, dai lolote linalotokana na masharti haya lazima lianzishwe (kwa kuwasilisha dai la rufaa au kuwasilisha hatua ya binafsi chini ya makubaliano ya rufaa yaliyo hapa chini) ndani ya mwaka mmoja (1) baada ya tarehe ambayo mtu anayeweka madai kwanza afahamu au kwa kweli inapaswa kufahamu juu ya kitendo hicho, upungufu, au kasoro inayosababisha madai; na hakutakuwa na haki kwa suluhisho lolote la madai yoyote ambayo hayadaiwi katika kipindi hicho cha wakati. **

Haki za Mhusika Mwingine

Unatambua na unakubali kuwa wamiliki wa Maudhui na wasambazaji fulani (kama vile watoaji wa duka la programu) ndio wanaokusudiwa kufaidika na Masharti haya na wana haki ya kutekeleza Masharti haya moja kwa moja dhidi yako. Kando na jinsi ilivyoainishwa katika sehemu hii, Masharti haya hayajakusudiwa kutoa haki kwa mtu yeyote isipokuwa wewe na Spotify, na kwa vyovyote vile Masharti haya huunda haki za mnufaika wa mhusika wa tatu.

Ikiwa umepakua programu yetu yoyote ya kifaa cha mkononi (kila moja, "App") kutoka Apple Inc. ("App") App Store au ikiwa unatumia Programu kwenye kifaa cha iOS, unakubali kuwa umesoma, umeelewa, na unakubali ilani ifuatayo kuhusu Apple. Masharti haya ni kati yako na Spotify pekee, sio na Apple, na Apple haiwajibiki kwa Huduma ya Spotify na maudhui yaliyomo. Apple haina wajibu wowote wa kutoa huduma zozote za matengenezo na msaada kuhusiana na Huduma ya Spotify. Katika tukio la kushindwa kokote kwa Huduma ya Spotify kutii udhamini unaotumika, unaweza kuarifu Apple na Apple itarejesha bei inayotumika ya ununuzi wa Programu kwako; na, kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria inayotumika, Apple haina jukumu jingine la dhamana kuhusiana na Huduma ya Spotify. Apple haina jukumu la kushughulikia madai yoyote yako au ya mhusika yeyote wa tatu kuhusiana na Huduma ya Spotify au milki yako au utumiaji wa Huduma ya Spotify, pamoja na: (1) madai ya wajibu kwa bidhaa; (2) madai yoyote kwamba Huduma ya Spotify inashindwa kufuata matakwa yoyote ya kisheria au ya udhibiti; (3) madai yanayotokana na ulinzi wa watumiaji au sheria kama hiyo na; (4) madai kuhusiana na ukiukaji wa hakibunifu. Apple haiwajibiki kwa uchunguzi, utetezi, uamuzi, na kutolewa kwa madai ya mhusika yeyote wa tatu kwamba Huduma ya Spotify au milki yako na utumiaji wa Programu zinakiuka haki za hakimiliki ya mhusika huyo wa tatu. Unakubali kufuata masharti yoyote yanayotumika ya mhusika wa tatu, unapotumia Huduma ya Spotify. Apple, na kampuni tanzu za Apple, ni walengwa wa tatu wa kufaidika kwa Masharti haya, na kwa kukubali kwako Masharti haya, Apple itakuwa na haki (na itachukuliwa kuwa imekubali haki) kutekeleza Masharti haya dhidi yako kama mnufaika wa mhusika wa tatu wa Masharti haya.

Kuondolea lawama

Unakubali kuiondolea lawama Spotify dhidi ya hasara zozote za kutabirika za moja kwa moja, uharibifu na gharama (pamoja na ada na gharama za wakili) ambazo Spotify imepata au imepitia zinazotokana na au zinazohusiana na: (1) ukiukaji wako wa Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada ya Spotify yaliyojumuishwa humu); (2) Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayochapisha au kuchangia vinginevyo; (3) shughuli yoyote unayoshiriki au kupitia Huduma ya Spotify; na (4) ukiukaji wako wa sheria yoyote au haki za mhusika wa tatu.

Sheria Inayotawala, Rufaa ya Lazima na Eneo

6.1 Sheria Inayotawala / Mamlaka

Isipokuwa vinginevyo inavyotakiwa na sheria za lazima katika nchi ya makazi, Makubaliano (na mizozo yoyote/madai yoyote yasiyokuwa ya kandarasi yanayotokana au yanayohusiana nayo) yanatii sheria za serikali au nchi zilizoorodheshwa hapa chini, bila kuzingatia uchaguzi au migongano ya kanuni za sheria.

Vilevile, wewe na Spotify mnakubali mamlaka ya mahakama yaliyoorodheshwa hapa chini kusuluhisha mgogoro, dai au mabishano yoyote yanayotokea kuhusiana na Makubaliano (na migogoro/madai yoyote yasiyo ya mkataba yanayotokana na au kuhusiana nayo), isipokuwa pale ambapo chini ya sheria za lazima husika, unaweza kuchagua kuwasilisha kesi za kisheria katika nchi yako, au tunahitajika kuwasilisha kesi za kisheria katika nchi yako

Nchi au eneo Uchaguzi wa Sheria Mamlaka
Nchi na maeneo mengine yote ambayo Spotify inapatikana.
Uswidi
Kipekee; Mahakama za Uswidi
Bulgaria, Saiprasi, Estonia, Ufaransa, Hong Kong, Lativia, Lithuania, Luxemburg, Malta, Monaco, Norway, Ufilipino, Ureno, Slovakia, Uhispania, Uturuki
Sheria za Uswidi
Zisizo za Kipekee; Mahakama za Uswidi
Brazil
Sheria za Brazil
Kipekee; Mahakama za Jimbo na Shirikisho la São Paulo, Jimbo la São Paulo, Brazili
Kanada
Haitumiki kwa wakazi wa Quebec: Sheria za Mkoa wa OntarioResidents of Quebec: Sheria za Mkoa wa Quebec, Kanada
Haitumiki kwa wakazi wa Quebec: Kipekee isipokuwa kwa madhumuni ya kutekeleza hukumu; Mahakama za Ontario, CanadaResidents of Quebec: Mahakama za Quebec, Kanada
Argentina, Bolivia, Chile, Kolombia, Kosta Rika, Jamhuri ya Dominika, Ekwado, El Salvador, Guatemala, Honduras, Nikaragua, Panama, Paraguay, Peru, Uruguay
Jimbo la California, Marekani
Kipekee; Mahakama za Jimbo na Shirikisho za Kaunti ya San Francisco, CA au New York, NY
Uingereza
Sheria za Uingereza na Wales
Maalum

6.2 ONDOLEO LA KESI YA KUNDI

MAHALI INAPORUHUSIWA CHINI YA SHERIA INAYOTUMIKA, WEWE NA SPOTIFY MNAKUBALI KUWA KILA MTU ANAWEZA KULETA MADAI DHIDI YA MWINGINE PEKEE KWA UWEZO WAKO AU BINAFSI NA WALA SI KAMA MJUMBE WA WAFANYAKAZI AU WA DARASA KATIKA DARASA LOLOTE LINALOKISIWA AU SHUGHULI YA UWAKILISHI. Isipokuwa wewe na Spotify mnakubaliana, hakuna msuluhishi au jaji anayeweza kujumuisha zaidi ya madai ya mtu mmoja au vinginevyo kusimamia aina yoyote ya mwakilishi au masikizo ya darasa.

6.3 USULUHISHI

Ikiwa uko katika, unaishi katika, una ofisi katika, au unafanya biashara katika mamlaka ambayo Sehemu hii ya 6.3. inatekezeka, vifungu vifuatavyo vya usuluhishi wa lazima vinatumika kwako:

6.3.1 Utatuzi na usuluhishi wa migogoro

Wewe na Spotify mnakubali kuwa mzozo wowote, dai, au ubishani kati yako na Spotify unaotokana na au unaohusiana kwa njia yoyote na Makubaliano haya au kwa uhusiano wako na Spotify kama mtumiaji wa Huduma (iwe ni kwa kandarasi, mateso, sheria, ulaghai, uwakilishi mbaya, au nadharia nyingine yoyote ya kisheria, na ikiwa madai yanatokea wakati wa au baada ya kukatiza Makubaliano) utaamuliwa na usuluhishi wa lazima wa mtu binafsi. Usuluhishi sio rasmi kuliko kesi mahakamani. HAKUNA HAKIMU AU MWAMUZI KATIKA USULUHISHI, NA UPITIAJI WA MAHAKAMA WA TUZO YA USULUHISHI NI MDOGO. Kunaweza kuwa na ugunduzi mdogo zaidi kuliko kortini. Msuluhishi lazima afuate makubaliano haya na anaweza kutoa uharibifu sawa na unafuu kama mahakama (pamoja na ada ya wakili), isipokuwa kwamba msuluhishi hawezi kutoa unafuu wa tamko au amri ya kumnufaisha mtu yeyote isipokuwa wahusika kwenye usuluhishi. Kifungu hiki cha usuluhishi hakitakomeshwa kwa ukatizaji wa Makubaliano.

6.3.2 Mambo ya kipekee

Bila kujali kifungu cha 6.3.1 hapo juu, wewe na Spotify wote mnakubali kwamba hakuna kitu hapa kitachotupiliwa mbali, kuzuia, au vinginevyo kupunguza mipaka ya haki zetu, wakati wowote, ili (1) kuleta hatua ya mtu binafsi katika korti ndogo ya madai, ( 2) kufuata hatua za utekelezaji kupitia wakala wa shirikisho, serikali, au wakala husika wa ndani ambapo vitendo kama hivyo vinapatikana, (3) kutafuta afueni ya kisheria katika korti ya sheria, au (4) kufungua kesi katika korti ya sheria kushughulikia madai ya ukiukaji wa mali miliki.

6.3.3 Kanuni za usuluhishi

Wewe au sisi tunaweza kuanzisha kesi za usuluhishi. Usuluhishi wowote kati yako na Spotify hatimaye utasuluhishwa chini ya Kanuni za Usuluhishi za Jumba la Biashara la Kimataifa ("ICC") zinazofanya kazi wakati huo ("Sheria za ICC") na msuluhishi mmoja au zaidi walioteuliwa kwa mujibu wa Kanuni za ICC, kama ilivyobadilishwa na Makubaliano haya, na utasimamiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya ICC.

Usuluhishi wowote utafanywa kwa lugha ya Kiingereza na isipokuwa vinginevyo ikitakiwa na sheria ya lazima ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya au mamlaka nyingine yoyote, sheria ya kutumika katika usuluhishi wowote itakuwa sheria ya [jimbo husika au nchi iliyoelezwa katika kifungu cha 6.1], bila kuzingatia uchaguzi au migogoro ya kanuni za sheria.

6.3.4 Wakati wa kufungua kesi

Usuluhishi wowote lazima uanzishwe kwa kuweka mahitaji ya usuluhishi ndani ya MWAKA MMOJA (1) baada ya tarehe ambayo mtu anayeweka madai kwanza afahamu au kwa kweli inapaswa kufahamu juu ya kitendo hicho, upungufu, au kasoro inayosababisha madai; na hakutakuwa na haki kwa suluhisho lolote la madai yoyote ambayo hayadaiwi katika kipindi hicho cha wakati. Ikiwa sheria inayotumika inakataza kipindi cha mwaka mmoja kwa kuthibitisha madai, madai yoyote yanapaswa kuthibitishwa ndani ya muda mfupi zaidi unaoruhusiwa na sheria inayotumika.

6.3.5 Ilani; Mchakato

Mtu ambaye anakusudia kutafuta usuluhishi lazima kwanza atume ilani ya maandishi ya mzozo kwa mwingine, kwa barua iliyothibitishwa au Federal Express (sahihi inahitajika), au ikiwa hakuna anwani ya mahali kwenye faili, kwa barua ya kielektroniki ("Ilani"). Anwani ya Spotify ya Ilani ni: [Spotify, Attn: General Counsel, 4 World Trade Center, 150 Greenwich Street, 62nd Floor, New York, New York 10007, USA]. Ilani lazima (1) ieleze asili na msingi wa madai au mzozo; na (2) kuweka wazi unafuu maalum unaotafutwa ("Mahitaji"). Tunakubali kutumia juhudi nzuri za imani kutatua madai hayo moja kwa moja, lakini ikiwa hatufikii makubaliano ya kufanya hivyo ndani ya siku 30 baada ya Ilani kupokelewa, wewe au Spotify mnaweza kuanzisha hatua za usuluhishi. Wakati wa usuluhishi, kiasi cha ofa yoyote ya maamuzi iliyotolewa na wewe au Spotify haitafunuliwa kwa msuluhishi mpaka baada ya msuluhishi kutoa uamuzi wa mwisho na tuzo, ikiwa ipo. Endapo mzozo wetu hatimaye unasuluhishwa kwa njia ya usuluhishi kwa kukupendelea, Spotify itakulipa (1) kiwango kilichotolewa na msuluhishi, ikiwa kipo, (2) kiasi cha mwisho cha malipo kilichoandikwa kilichotolewa na Spotify katika kusuluhisha mzozo kabla ya tuzo ya msuluhishi; au (3) $ 1,000.00, yoyote iliyo kubwa. Hati na maelezo yote yaliyofichuliwa wakati wa rufaa yatawekwa kwa siri na mpokeaji na hayatatumiwa na mpokeaji kwa madhumuni yoyote ambayo si kwa madhumuni ya rufaa wala utekelezaji wa uamuzi na hukumu ya mpatanishi na hayatafichuliwa isipokuwa kwa imani kwa watu walio na hitaji la kujua kwa madhumuni hayo au inavyohitajika na sheria husika. Isipokuwa kama inavyohitajika ili kutekeleza uamuzi na hukumu ya mpatanishi, hakuna kati yako na Spotify atakayetoa tangazo la umma au maoni ya umma au kuanzisha tangazo lolote kuhusu rufaa, ikiwemo lakini si tu, ukweli kwamba wahusika wana mgogoro, uwepo wa rufaa, au uamuzi au hukumu yoyote ya mpatanishi.

6.3.6 Marekebisho

Ikitokea kwamba Spotify inafanya mabadiliko yoyote ya usoni kwa kifungu hiki cha usuluhishi (isipokuwa mabadiliko ya anwani ya Spotify kwa ajili ya Ilani), unaweza kukataa mabadiliko yoyote kama hayo kwa kututumia ilani iliyoandikwa ndani ya siku 30 za mabadiliko kwa anwani ya Spotify ya Ilani, ambayo katika hali hiyo akaunti yako na Spotify itakatizwa mara moja na kifungu hiki cha usuluhishi, jinsi kinavyotumika mapema kabla ya marekebisho unayoyakataa, kitaendelea kutumika.

6.3.7 Utekelezaji

Ikiwa ondoleo la kesi ya kundi katika Sehemu ya 6.2 linapatikana kutoweza kutekelezeka katika usuluhishi au ikiwa sehemu yoyote ya Sehemu hii ya 6.3 itapatikana kuwa batili au haiwezi kutekelezeka, basi ukamilifu wa Sehemu hii ya 6.3 itakuwa batili na, kwa hali kama hiyo, watu wanakubaliana kuwa mamlaka ya kipekee na ukumbi ulioelezewa katika Sehemu ya 6.1 itasimamia hatua yoyote inayotokana na au inayohusiana na Makubaliano na hutazuiwa kuwasilisha kesi wakati wowote.

7. Kuhusu Masharti haya

Chini ya sheria husika, huenda ukawa na haki fulani ambazo haziwezi kuzuiwa na mkataba. Masharti haya hayanuii kwa njia yoyote kuzuia haki hizo.

Mabadiliko

Tunaweza kufanya mabadiliko kwenye Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada ya Spotify yaliyojumuishwa na rejeo lililo humu) mara kwa mara kwa kukuarifu kuhusu mabadiliko hayo kwa njia yoyote inayofaa (kabla hayajaanza kutumika), ikiwemo kwa kuchapisha Makubaliano yaliyorekebishwa kuhusu Huduma ya Spotify husika (mradi tu, kwa mabadiliko ya nyenzo, tutajitahidi kuongeza ilani hiyo kwa barua pepe, ujumbe wa ibukizi ya huduma ya ndani, au njia nyinginezo). Mabadiliko yoyote kama hayo hayatatumika kwa mgogoro wowote kati yako na sisi unaotokea kabla ya tarehe ambayo tulichapisha Masharti yalirekebishwa, au sheria na masharti mengine ya Spotify, yanayojumuisha mabadiliko hayo, au vinginevyo kukuarifu kuhusu mabadiliko hayo. Matumizi yako ya Huduma ya Spotify baada ya mabadiliko yoyote kwenye Masharti haya yatahusu ukubalifu wako wa mabadiliko hayo. Ikiwa usingependa kuendelea kutumia Huduma ya Spotify chini ya Masharti yaliyosasishwa, unaweza kukomesha akaunti yako kwa kuwasiliana nasi. Tarehe ya kuanza kutumika iliyowekwa juu ya hati hii inaonyesha wakati Masharti haya yalipobadilishwa mara ya mwisho.

Makubaliano Yote

Kando na jinsi ilivyoelezwa katika sehemu hii au kama ilivyokubaliwa wazi kwa maandishi kati yako na Spotify, Masharti haya yanajumuisha sheria na masharti yote yaliyokubaliwa kati yako na Spotify na yanashinda makubaliano yoyote ya hapo awali kuhusiana na mada ya Masharti haya, yawe yameandikwa au kwa mdomo. Kama ilivyobainika hapo juu, sheria na masharti mengine yanayotawala matumizi ya Huduma ya Spotify yanajumuishwa humu kwa rejeo, ikiwemo sheria na masharti yafuatayo: Masharti ya Ofa ya Matangazo ya Spotify Premium;Masharti ya Kadi ya Spotify; Miongozo ya Mtumiaji ya Spotify; Sera ya Hakimiliki ya Spotify; na Masharti ya Jumuia ya Usaidizi wa Spotify.

Kifungu cha Sheria Kinachotumika na Ondoleo

Isipokuwa kama vinginevyo ilivyotajwa katika Masharti haya, endapo kifungu chochote cha Masharti haya kitasemekana si halali au kisichoweza kutekelezwa kwa sababu yoyote au kwa kiwango chochote, vifungu vinavyosalia vya Masharti haya havitaathiriwa na utumiaji wa kifungu hicho utatekelezwa kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria.

Ukosefu wowote wa Spotify au mnufaika yeyote wa mhusika wa tatu wa kutekeleza Masharti haya au kifungu chochote hautaondoa haki ya Spotify au ya mnufaika wa mhusika wa tatu kufanya hivyo.

Kazi

Spotify inaweza kugawa Masharti haya yote au sehemu na inaweza kugawa au kuteua sehemu fulani au nzima ya haki au makujumu yake chini ya Masharti haya. Huenda usitoe Masharti haya, yote au sehemu, au kuhamisha au kutoa leseni ndogo haki zako chini ya Masharti haya, kwa mhusika yeyote wa tatu.