Sheria na Masharti ya Spotify® Premium for Family

TAFADHALI SOMA MASHARTI HAYA KWA MAKINI NA KIKAMILIFU.** YANA HALI MUHIMU NA VIKWAZO KUHUSU UPATIKANAJI WA USAJILI WA SPOTIFY PREMIUM FAMILY.**

2021-02-23

1. Utangulizi

Usajili wa Spotify Premium Family ("Usajili wa Premium Family") hutolewa na Spotify, kulingana na sheria na masharti haya ("Sheria na Masharti ya Premium Family"), na kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya Spotify, ambayo yamejumuishwa hapa kwa marejeleo. Masharti yaliyo kwenye herufi kubwa yanayotumika lakini hayajafafanuliwa hapa yatatumika vivyo hivyo kwenye Sheria na Masharti ya Spotify.

Usajili wa Premium Family humpa mmiliki wa akaunti ya msingi na hadi wanafamilia watano (5) ufikiaji kwa akaunti tanzu kwa huduma ya Spotify Premium Family, kuanzia wakati unapoamilisha akaunti kuu kwa kuwasilisha maelezo yako ya malipo na kulipa bei iliyotangazwa. Kwa kuwasilisha maelezo yako ya malipo, wewe (i) unakubali kwetu kutumia maelezo yako ya malipo kulingana na Sera ya Faragha, na (ii) kutambua na kukubali Sheria na Masharti haya ya Premium Family.

Kama sehemu ya huduma ya Spotify Premium Family, Spotify inaweza kutoa Spotify Kids App. Kwa kufungua akaunti ndogo za Spotify Kids, unathibitisha kuwa wewe ndiye mlezi halali wa mtoto yeyote anayetumia akaunti hiyo. Tafadhali soma Sera ya Faragha ya Spotify Kids, ambayo inatumika kwa matumizi yoyote ya Spotify Kids. Spotify Kids inatolewa pekee kama sehemu ya Usajili wa Premium Family.

2. Ustahiki na Uthibitishaji

  1. Ili kustahiki kwenye Usajili wa Premium Family, mmiliki wa akaunti ya msingi na wamiliki wa akaunti tanzu lazima wawe wanafamilia wanaoishi kwenye anwani moja.
  2. Baada ya kuamilisha akaunti tanzu ya Premium Family (bila kujumuisha akaunti y(z)a Spotify Kids), utaulizwa uthibitishe anwani yako ya nyumbani.
  3. Tunaweza kukuuliza mara kwa mara kuthibitisha anwani ya nyumbani kwako ili kuthibitisha kwamba bado unafikia kriteria ya ustahiki.

Tunatumia kitafutaji cha anwani cha Google Maps kukusaidia kupata na kuweka anwani yako. Anwani unayoingiza baada ya kuamilisha au uthibitishaji upya itawiana na Masharti ya Ziada Ramani za Google na Sera ya Faragha ya Google.

Spotify ina haki ya kukatiza au kusimamisha ufikiaji wa huduma ya Spotify Premium Family na akaunti y(z)a Spotify Premium Family mara moja na wakati wowote ikiwa unashindwa kutimiza vigezo vya ustahiki na kama ilivyoainishwa katika Sheria na Masharti ya Utumiaji wa Spotify.

3. Kughairi

Unaweza kughairi Usajili wa Premium Family wakati wowote kwa kuingia kwenye akaunti yako ya Spotify na kufuata vidokezo kwenye ukurasa wa Akaunti, au kwa kubofya hapa na kufuata maagizo. Ikiwa mmiliki wa akaunti ya msingi ataghairi Usajili wa Premium Family au vinginevyo akaunti imekatizwa, Akaunti za Msingi na tanzu za Premium zitashushwa moja kwa moja kwa Huduma ya Bure ya Spotify na akaunti yoyote ya(zozote za) Spotify Kids (z)itafutwa.

4. Upatikanaji wa Usajili wa Premium Family

Spotify ina haki ya kukatiza, kurekebisha au kusitisha Usajili wa Premium Family kikamilifu au kwa sehemu wakati wowote na kwa sababu yoyote. Baada ya wakati kama huo, Spotify haitakuwa na jukumu la kudumisha au kuruhusu usajili wowote zaidi kwa Usajili wa Premium Family.

5. Vikwazo Vingine

  1. Kadi za zawadi za Spotify na kadi za kulipia mbeleni haziwezi kutumiwa kama njia halali ya malipo ya Usajili wa Premium Family.
  2. Hakuna mapunguzo mengine yanayoweza kutumika.
  3. Hakuna urejeshaji wa pesa au ulipaji wa usajili nusu wa usajili wa kila mwezi.
  4. Spotify itajulisha mabadiliko yoyote ya bei kwako, na unaweza kukubali au kukataa mabadiliko ya bei kama hayo, kulingana na Sheria na Masharti ya Utumiaji wa Spotify.
  5. Fahamu; Ikiwa wewe ni mmiliki wa akaunti ya Premium, kwa kujiunga na mpango wa Usajili wa Premium Family unatambua na unakubali kuwa hakuna marejesho ya pesa yanayopatikana kwa kubadilisha kutoka kwa mpango wako wa sasa wa Premium kabla ya kipindi chako cha usajili kilicholipiwa kumalizika. Baada ya kujiunga, utabadilisha mara moja kwenda Usajili wa Premium Family, na ufikiaji wako kwa huduma ya Spotify Premium utabaki bila kukatizwa, lakini muda wowote ambao haujatumiwa wa Premium ambao umeulipia tayari, pamoja na siku zozote zilizosalia za Majaribio ya bure, chini ya mpango wako wa sasa wa Premium zitapotezwa.

Kampuni ya kandarasi:

Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501