Sheria na Masharti ya Spotify® Premium Duo

TAFADHALI SOMA MASHARTI HAYA KWA MAKINI NA KIKAMILIFU.** YANAJUMUISHA MASHARTI NA VIKWAZO MUHIMU KUHUSU UPATIKANAJI WA USAJILI WA SPOTIFY PREMIUM DUO.**

Kufanya kazi kuanzia 02/23/2021

1. Utangulizi

Usajili wa Spotify Premium Duo ("Usajili wa Premium Duo") unafanywa kupatikana na Spotify, kulingana na sheria na masharti ("Masharti ya Usajili wa Premium Duo"), na Kwa Mujibu wa Sheria na Masharti ya Spotify, ambayo yamejumuishwa kwa marejeo. Masharti yaliyo kwenye herufi kubwa yanayotumika lakini hayajafafanuliwa hapa yatatumika vivyo hivyo kwenye Sheria na Masharti ya Spotify.

Usajili wa Premium Duo unampa mmiliki mkuu wa akaunti na mmiliki mmoja (1) wa akaunti tanzu katika familia ili kufikia huduma ya Spotify Premium Duo, namna ya Usajili Unaolipiwa, kuanzia wakati unapoamilisha akaunti kuu kwa kuwasilisha maelezo yako ya malipo na kulipia bei iliyotangazwa. Kwa kuwasilisha maelezo yako ya malipo, wewe (i) unatukubalia sisi kutumia maelezo yako ya malipo kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha, na (ii) unatambua na kukubali Masharti ya Usajili wa Premium Duo.

2. Ustahiki na Uthibitishaji

  1. Ili kustahiki kwa Usajili wa Premium Duo, mmiliki wa akaunti kuu na mmiliki wa akaunti tanzu wa familia lazima waishi katika eneo la anwani moja.
  2. Baada ya kuamilisha yoyote kati ya akaunti za Usajili wa Premium Duo, utaulizwa kuthibitisha anwani yako ya nyumbani.
  3. Tunaweza kukuuliza mara kwa mara kuthibitisha anwani ya nyumbani kwako ili kuthibitisha kwamba bado unafikia kriteria ya ustahiki.

Tunatumia kitafutaji cha anwani cha Google Maps kukusaidia kupata na kuweka anwani yako. Anwani unayoingiza baada ya kuamilisha au uthibitishaji upya itawiana na Masharti ya Ziada Ramani za Google na Sera ya Faragha ya Google.

Spotify inahifadhi haki ya kukatiza au kusimamisha ufikiaji kwa huduma ya Spotify Premium Duo mara moja na kwa wakati wowote ikiwa unakosa kufikia kriteria ya ustahiki na vinginevyo ilivyopangwa katika Sheria na Masharti ya Utumiaji wa Spotify.

3. Kughairi

Unaweza kughairi Usajili wa Premium Duo wakati wowote kwa kunigia katika akaunti yako ya Spotify na kufuata maagizo kwenye ukurasa wa Akaunti, au kwa kubofya hapa na kufuata maagizo. Ikiwa mmiliki mkuu wa akaunti anaghairi Usajili wa Premium Duo, akaunti ya mtumiaji mkuu na mtumiaji tanzu zitarudishwa chini mara moja kwa kiwango cha Huduma ya Spotify Bila Malipo.

4. Upatikanaji wa Usajili wa Premium Duo

Spotify inahifadhi haki ya kukatiza, kuboresha au kusimamisha Usajili wa Premium Duo kijumla au kisehemu wakati wowote na kwa sababu yoyote. Baada ya muda kama huo, Spotify haitawajibikia kudumisha au kuruhusu usajili mwingine wowote kwenye Usajili wa Premium Duo.

5. Vikwazo Vingine

  1. Kadi za zawadi za Spotify na kadi za kulipia mapema haziwezi kutumika kama njia halali ya malipo kwa Usajili wa Premium Duo.
  2. Hakuna mapunguzo mengine yanayoweza kutumika.
  3. Hakuna urejeshaji wa pesa au ulipaji wa usajili nusu wa usajili wa kila mwezi.
  4. Spotify itajulisha mabadiliko yoyote ya bei kwako, na unaweza kukubali au kukataa mabadiliko ya bei kama hayo, kulingana na Sheria na Masharti ya Utumiaji wa Spotify.
  5. Fahamu; Ikiwa wewe ni mmiliki wa akaunti ya Premium, kwa kujiunga na mpango wa Usajili wa Premium Duo unatambua na kukubali kwamba hakuna urejeshwaji wa pesa unaopatikana kwa kubadilisha kutoka kwa mpango wa sasa wa Premium kabla ya mwisho wa kipindi chako cha usajili uliolipiwa. Baada ya kujiunga, utabadilisha mara moja hadu kwenye Usajili wa Premium Duo, na ufikiaji wako kwenye huduma ya Spotify Premium utasalia kutochachawizwa, lakini muda wowote wa Premium usiotumika ambao umeshalipia, kwa kujumuisha siku zozote zinazosalia za Majaribio ya bila malipo, chini ya mpango wako wa sasa wa Premium utapotezwa.

Kampuni ya kandarasi:

Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501