Sera ya Hakimiliki ya Spotify

Mara ya mwisho kusasishwa: 23/02/2021

Hujambo, na asante kwa kutembelea ukurasa wa sera ya hatimiliki ya Spotify. Spotify inaheshimu haki za hakibunifu na huwatarajia watumiaji wake kufanya vivyo hivyo. Ikiwa wewe ni mmiliki wa hatimiliki, au wakala, na unaamini kwamba nyenzo yoyote iliyochapishwa inayopatikana moja kwa moja kwenye Huduma ya Spotify inakiuka kazi yako iliyochapishwa, tafadhali tufahamishe.

Tafadhali tumia fomu hii ya wavuti kuwasilisha notisi ya ukiukwaji wa hakimiliki unaokisiwa. Kwa njia nyingine notisi ya ukiukwaji wa hatimiliki unaokisiwa inaweza kutumwa kwa wakala wa hatimiliki wa Spotify kwenye anwani ifuatayo:

Spotify USA Inc.

Kwa: Idara ya Sheria Legal, Wakala wa Hatimiliki

4 World Trade Center, 150 Greenwich Street, 62nd Floor, New York, NY 10007

infringement-claim@spotify.com

Notisi ya ukiukwaji wa uanokisiwa wa hatimiliki lazima itumwe kwa wakala wa hatimiliki wa Spotify jinsi ilivyoorodheshwa hapo juu. Tafadhali jumuisha maelezo mengi iwezekanavyo ili kutuwezesha kutambua ukweli au hali, kwa kujumuisha, mahali inapowezekana:

  1. Sahihi halisi au ya kielektroniki ya mmiliki (mtu aliyeidhinishwa kufanya kazi kwa niaba ya mmiliki) wa hatimiliki ambaye anakisiwa kukiukwa;
  2. Utambuzi maalum wa kila kazi iliyochapishwa inayodaiwa kukiukwa;
  3. Maelezo ya mahali ambapo nyenzo inayoaminika kukiuka inapatikana kwenye Huduma ya Spotify au Tovuti za Spotify (tafadhali toa maelezo mengi iwezekanavyo na utoe URL ili kutusaidia kuipata nyenzo unayoiripoti);
  4. Taarifa za mawasiliano za mtu anayelalamika, kama vile jina kamili, anwani, namba ya simu, na baruapepe;
  5. Tamko kwamba mhusika anayelalamika ana imani nzuri kwamba utumiaji wa kazi kwa namna ambavyo imelalamikiwa hauruhusiwi na mmiliki wa hatimiliki, wakala wake, au sheria; na
  6. Tamko kwamba taarifa zilizo kwenye nitisi ni sahihi, na kwamba mhusika anayelalamika ni mmiliki wa haki ambayo inakisiwa kukiukwa, au wakala wa mmiliki.

Pia tunafaa kukufahamisha kwamba Spotify ina sera ya kukatiza katika hali zifaazo akaunti za wasajiliwa ambao wamekiuka kwa kurudiarudia.

Hakimiliki © 2012 Spotify AB. Haki zote zimehifadhiwa.

Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501