Sheria na Masharti ya Spotify

Ilisasishwa Mwisho: Agosti 26, 2025

1. Utangulizi

2. Huduma ya Spotify Tunayotoa.

3. Matumizi Yako ya Huduma ya Spotify

4. Haki za Maudhui na Mali ya Uvumbuzi

5. Usaidizi, Maelezo, Maswali na Malalamishi ya Mteja

6. Matatizo na Migogoro

7. Kuhusu Sheria Hizi

1. Utangulizi

Tafadhali soma Masharti haya ya Matumizi ("Masharti" haya) kwa makini kwa kuwa yanaongoza matumizi yako ya (ambayo yanajumuisha ufikiaji wa) huduma za Spotify zilizoboreshwa kwa ajili ya kutiririsha muziki na maudhui mengine, ikiwemo tovuti zetu zote na programu zinazojumuisha au zinazounganisha Masharti haya (kwa pamoja, "Huduma ya Spotify") na muziki, video, podikasti zozote, au nyenzo nyingine ambazo zinapatikana kupitia Huduma ya Spotify ("Maudhui").

Matumizi ya Huduma ya Spotify yanazingatia sheria na masharti yanayowasilishwa na Spotify, ambayo yamejumuishwa na rejeo hili ndani ya masharti haya (kwa pamoja "Makubaliano"). Tafadhali rejelea Sehemu ya 7 hapa chini kwa maelzo kuhusu masharti hayoo ya ziada na jinsi tunaweza kubadilisha Masharti haya au mashatri ya ziada yaliyojumuishwa kwa njia ya marejeleo. Ili kujifunza mengi zaidi kuhusu jinsi Spotify hukusanya, kutumia, kushiriki na kulinda maelezo yako ya kibinafsi, tafadhali tazama Spotify Privacy Policy.

Kwa kujisajili kwa, au vinginevyo kutumia Huduma ya Spotify, unakubali Masharti haya. Usipokubali Masharti haya, basi hupaswi kutumia Huduma ya Spotify wala kufikia Maudhui yoyote.

Mtoa Huduma

Masharti haya ni kati yako na Spotify AB, Regeringsgatan 19, 111 53, Stockholm, Sweden.

Masharti ya umri na ustahiki

Ili uweze kutumia Huduma ya Spotify na kufikia Maudhui yoyote, unahitaji (1) kuwa na umri wa miaka 13 (au umri wa chini zaidi unaokubalika katika nchi unakoishi) au zaidi, (2) kuwa na idhini ya mzazi au mlezi ikiwa wewe ni mtoto mdogo katika nchi unakoishi; (3) kuwa na uwezo wa kuingia katika mkataba wa kisheria nasi na huzuiwi kufanya hivyo chini ya sheria zozote zinazotumika, na (4) unaishi katika nchi ambako Huduma hii inapatikana. Pia unaahidi kuwa maelezo yoyote ya usajili unayowasilisha kwa Spotify ni ya kweli, sahihi, na kamili, na unakubali kuyahifadhi hivyo nyakati zote. Ikiwa wewe ni mtoto katika nchi yako, mzazi au mlezi wako atahitaji kuingia kwenye Masharti haya kwa niaba yako. Usipokidhi mahitaji ya umri ili kutumia Huduma ya Spotify na kufikia Maudhui basi lazima ujisajili kama mtumiaji. Katika soko zingine, Spotify inaweza kuwapa wamiliki wa akaunti wa msingi fursa ya kuruhusu ufikiaji kwa uzoefu wa watoto kama sehemu ya usajili wa familia. Kwa kuruhusu ufikiaji kama huu, mmiliki wa msingi wa akaunti anadhibitisha yeye ni mlezi wa kisheria kwa mtumiaji yeyote anayefikia uzoefu huo na kwamba anatoa idhini kwa mtumiaji mchanga kutumia Spotify.

2. Huduma ya Spotify Tunayotoa.

Machaguo ya Huduma ya Spotify

Tunatoa machaguo mbalimbali ya Huduma ya Spotify. Machaguo fulani ya Huduma ya Spotify yanatolewa bila malipo, huku mengine yakihitaji malipo kabla hayajafikiwa ("Usajili wa Kulipiwa"). Pia tunaweza kutoa mipango maalum ya mauzo, uanachama, au huduma, kwa kujumuisha ofa za bidhaa za mhusika mwingine na huduma. Hatuwajibikii bidhaa na huduma zinazotolewa na wahusika wa tatu kama hao.

Majaribio

Mara kwa mara, sisi au wengine kwa niaba yetu wanaweza kutoa majaribio ya Usajili wa Kulipiwa kwa kipindi maalum bila kulipia au kwa kiwango kilichopunguzwa ("Jaribio"). Kwa kutumia Huduma ya Spotify kupitia Jaribio, ni lazima ukubali Masharti ya Ofa ya Uendelezaji ya Spotify Premium.

Programu za Mhusika Mwingine, Vifaa na Programu Huria

Huduma ya Spotify inaweza kujumuishwa na, au vinginevyo inaweza kutumia programu, tovuti na huduma za mhusika mwingine ("Programu za Mhusika Mwingine") na kompyuta za binafsi, vifaa vya mkononi, tableti, vifaa vya kuvaa, spika za mhusika mwingine na vifaa vingine ("Vifaa"). Matumizi yako ya Programu na Vifaa hivyo vya Mhusika Mwingine yanaweza kutii masharti, sheria na sera za ziada ulizopewa na mhusika mwingine husika. Spotify haihakikishi kuwa Programu na Vifaa vya Mhusika Mwingine vitaoana na Huduma ya Spotify.

Vizuizi na Marekebisho ya Huduma

Tunatumia utunzaji na ujuzi wa busara kuhakikisha kuwa Huduma ya Spotify inaendelea na kukupa hali ya utumiaji wa sauti iliyoboreshwa. Hata hivyo, huduma zetu tunazotoa na upatikanaji wake unaweza kubadilika mara kwa mara kwa kutegemea sheria zinazotumika, bila kuwajibika kwako; kwa mfano:

  • Huduma ya Spotify inaweza kukumbana na uchachawizaji wa muda mfupi kutokana na matatizo ya ufundi, matengenezo au kujaribu, au masasisho, ikiwemo yale yanayohitajika ili kuakisi mabadiliko katika sheria husika na matakwa ya udhibiti.
  • Tunalenga kuzinduka na kuboresha Huduma zetu mara kwa mara na tunaweza kubadilisha, kuahirisha, au kusimamisha (kabisa au kwa muda mfupi) kutoa Huduma ya Spotify yote au kidogo (ikiwemo utendaji, vipengele, mipango ya usajili na ofa fulani za uendelezaji).
  • Toleo letu la maudhui linalobadilika mara kwa mara linabadilika na kubadilika na mahitaji ya jumuiya ya Spotify. Spotify haina wajibu wa kutoa maudhui yoyote mahususi kupitia Huduma ya Spotify, na Spotify au wamiliki wake husika wanaweza kuondoa nyimbo, video, podikasti, vitabu fulani vya suati na Maudhui mengine bila ilani.

Haki yako ya kukomesha Sheria hizi ikiwa hutaki tena kutumia Huduma ya Spotify imeelezwa katika Sehemu ya 6 hapa chini.

Ikiwa una ada za kulipa kabla moja kwa moja kwa Spotify kwa Usajili wa Kulipiwa ambao Spotify inasimamisha kabla ya mwisho wa Kipindi chako cha Kulipa Awali (kama sharti hilo lilivyofafanuliwa katika sehemu ya Malipo na kughairi hapa chini), Spotify itakurejeshea ada ulizolipa kabla kwa Kipindi cha Usajili wa Kulipiwa wa sasa baada ya usimamishaji kama huo. Maelezo ya akaunti na bili yako lazima yasasishwe ili tukurejeshee malipo.

Spotify haina wajibu wowote kwako, wala jukumu lolote la kukurejeshea pesa, kuhusiana na kukatika kwa muunganisho wa intaneti au huduma nyingine au hitilafu zinazosababishwa na hatua za mamlaka ya serikali, watu wengine au matukio ambayo hatuwezi kuyadhibiti.

3. Matumizi Yako ya Huduma ya Spotify

Kufungua akaunti ya Spotify

Unawea kuhitaji kufungua akaunti ya Spotify ili kutumia yote au sehemu ya Huduma ya Spotify, na akaunti hii lazima iwe katika nchi unayoishi. Ni wewe pekee unayepaswa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri lako na unapaswa kuweka maelezo haya kwa usiri. Unaelewa kuwa unawajibika kwa matumizi yote (ikijumuisha matumizi yoyote ambayo hayajaidhinishwa) ya jina la mtumiaji na nenosiri lako. Ifahamishe timu ya Huduma kwa Wateja mara moja ikiwa jina la mtumiaji au nenosiri limepotea au kuibwa, au ikiwa unaamini kuna ufikiaji usioidhinishwa wa akaunti yako.

Spotify inaweza kuondoa, au kuhitaji ubadilishe jina lako la mtumiaji kwa sababu yoyote.

Haki zako za kutumia Huduma ya Spotify

Ufikiaji wa Huduma ya Spotify

Kulingana na uzingatiaji wako wa Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti mengine yoyote husika), tunakupa ruhusa isiyo ya kikomo, isiyo ya kipekee na inayoweza kubatilika ili utumie kwa njia ya binafsi na isiyo ya biashara Huduma ya Spotify na Maudhui (kwa pamoja, "Ufikiaji"). Ni lazima Ufikie tu aina ya Huduma ya Spotify inayotolewa katika nchi unayoishi. Uwezo huu wa Kufikia huduma utaendelea kutumika isipokuwa na hadi wewe au Spotify itakapoukomesha. Unakubali kuwa hutasambaza tena, kuuza wala kuhamisha Huduma ya Spotify wala Maudhui.

Programu za Spotify na Maudhui yake yana leseni, hayauzwi wala kuhamishwa kwako na Spotify, na watoaji leseni wake ni wa miliki wa nakala zote za programu za Spotify na Maudhui yake hata baada ya kuzisakinisha kwenye Vifaa vyako.

Haki za Umiliki za Spotify

Huduma ya Spotify na Maudhui ni mali ya Spotify au watoaji leseni wa Spotify. Alama za biashara za Spotify, alama za huduma, majina ya biashara, logo, majina ya vikoa na vipengele vingine vyovyote vya chapa ya Spotify ("Vipengee vya Chapa ya Spotify") ni mali ya Spotify au watoaji wake wa leseni. Sheria na Masharti haya hayakupi haki zozote za kutumia Vipengele vya Chapa ya Spotify iwe kwa matumizi ya kibiashara au yasiyo ya kibiashara.

Unakubali kufuata miongozo yetu ya Mtumiajina Sheria za Mfumo na kutotumia Huduma ya Spotify, Maudhui, au sehemu yoyote kwa njia yoyote isiyokubaliwa moja kwa moja na Makubaliano.

Malipo na kughairi

Usajili wa Kulipiwa

Unaweza kununua Usajili wa Kulipiwa moja kwa moja kutoka Spotify au kulipia mhusika mwingine kwa:

  • kulipa ada ya usajili mapema kila mwezi au vipindi vingine vya kujirudia ulivyofahamishwa kabla ya ununuzi wako; au
  • malipo ya mapema yanayokupa ufikiaji wa Huduma ya Spotify kwa kipindi mahususi ("Kipindi cha Kulipia Kabla").

Viwango vya kodi vinakokotelwa kulingana na maelezo unayotoa na kiwango kinachotumika wakati wa ada yako ya kila mwezi.

Ukinunua ufikiaji wa Usajili wa Kulipiwa kupitia mhusika mwingine, sheria na masharti tofauti na mhusika huyo mwingine yanaweza kutumika kwenye matumizi yako ya Huduma ya Spotify mbali na Masharti haya. Ukinunua Usajili wa Kulipiwa kwa kutumia msimbo, kadi ya zawadi, ofa ya kulipia kabla, au ofa nyingine inayotolewa au kuuzwa na au kwa niaba ya Spotify kwa ajili ya ufikiaji wa Usajili wa Kulipiwa ("Misimbo"), ni lazima ukubali Masharti ya Kadi ya Spotify.

Mabadiliko ya bei na kodi

Spotify inaweza kubadilisha bei ya Usajili wa Kulipiwa mara kwa mara, kwa kujumuisha ada za usajili wa kurudiarudia, Kipindi cha Malipo ya Kabla (kwa vipindi ambavyo havijalipiwa), au Misimbo (iliyofafanuliwa hapo juu), na tutakufahamisha mapema kuhusu mabadiliko yoyote ya bei. Mabadiliko ya bei yataanza kufanya kazi mwanzoni mwa kipindi cha usajili unaofuata tarehe ya mabadiliko ya bei. Kwa kuzingatia sheria husika, kwa kuendelea kutumia Huduma ya Spotify baada ya mabadiliko ya bei kuanza kutumika, utakuwa umeikubali bei mpya. Ikiwa hukubali mabadiliko ya bei, unaweza kukataa mabadiliko kwa kuondoa usajili wako kwenye Usajili wa Kulipiwa kabla ya kuanza kutumika kwa mabadiliko ya bei.

Viwango vya kodi vinalingana na viwango vinavyotumika wakati wa ada yako ya kila mwezi. Viwango hivi vinaweza kubadilika baada ya muda kulingana na matakwa ya kodi ya ndani ya nchi, jimbo, himaya au hata jiji lako. Badiliko lolote la kiwango cha Kodi litatumika kiotomatiki kulingana na maelezo unayotoa ya akaunti.

Bei ya Usajili wa Kulipiwa au Jaribio ni mahususi kwa aina ya Huduma ya Spotify inayotolewa katika nchi unayoishi na unakubali kutohusika na njia zozote za Kufikia Usajili wa Kulipiwa au Jaribio bila kulipa bei inayohusika au kutatiza majaribio halali ya Spotify ya kukusanya malipo ya Ufikiaji kama huo.

Bili na Ughairi

Isipokuwa imeonyeshwa vinginevyo (kwa mfano, ikiwa umejisajili kwa Kipindi cha Kulipiwa Mapema), Usajili wa Kulipiwa utaendelea kwa muda usio na kipimo hadi kughairiwa. Utatozwa bili mara kwa mara katika siku ya kwanza ya kila kipindi cha bili na utalipa na kutuidhinisha (au mhusika mwingine anayefaa, ikiwa utajisajili kupitia mhusika mwingine) ili kutoza njia yako ya malipo ya ada ya usajili wa wakati huo.

Unaweza kughairi Usajili wako wa Kulipiwa wakati wowote kwa kuingia kwenye akaunti yako ya Spotify na kufuata vidokezo kwenye ukurasa wa Akaunti, au kwa kubofya hapa na kufuata maagizo.
Isipokuwa imeonyeshwa viginevyo, ughairi utaanza kutumika kutoka mwisho mwa kipindi cha bili ambacho unaghairi na utashushwa hadi toleo lisilolipishwa la Huduma ya Spotify. Hatutoi marejesho ya fedha wala mikopo kwa vipindi vyovyote vya usajili mdogo, isipokuwa kama ilivyoelezwa katika Masharti haya.

Ikiwa umenunua Usajili wa Kulipiwa kwa kutumia Msimbo, usajili wako utakatizwa mara moja mwishoni mwa kipindi kilichotajwa kwenye Msimbo, au wakati kuna salio lisilotosha kulipia Huduma ya Spotify.

Pamoja na hayo, bila kujali, haki zingine zozote tunazoweza kuwa nazo chini ya Sheria hizi, tunahifadhi haki ya kusitisha Usajili wa Kulipiwa wakati wowote, kwa notisi isiyopungua siku 14 kwako. Isipokuwa tukujulishe vinginevyo, tutakuruhusu kudumisha ufikiaji wa Usajili wa Kulipiwa kwa muda uliobaki wa kipindi cha bili ya wakati huo, kisha tutashusha akaunti yako kwa toleo lisilolipishwa la Huduma ya Spotify.

Haki ya kujiondoa

Ukijisajili kwa Jaribio, unakubali kwamba haki ya kujiondoa kwa Usajili wa Kulipiwa ambao unapata Jaribio itakwisha siku kumi na nne (14) baada ya kuanza Jaribio. Usipoghairi Usajili wa Kulipiwa kabla ya Jaribio kuisha, unapoteza haki yako ya kujiondoa na unaidhinisha Spotify kukulipisha moja kwa moja bei mliyokubaliana kila mwezi hadi utakapoghairi Usajili wa Kulipiwa. Kwa matoleo chini ya siku kumi na nne (14), unatuidhinisha kwa njia ya maandishi kukupa huduma ya kulipia mara tu baada ya mwisho wa Jaribio lako na kwamba kutoka wakati huo unapoteza haki yako ya kujiondoa.

Ukinunua Usajili wa Kulipiwa bila Jaribio, unakubali kuwa una siku kumi na nne (14) baada ya ununuzi wako kujiondoa kwa sababu yoyote na lazima utulipe kwa huduma ulizopewa hadi wakati unatuambia kwamba umebadilisha nia yako. Unatukubalia kwa njia ya maandishi kukupa huduma mara tu baada ya ununuzi wako, kuwa unapoteza haki yako ya kujiondoa na unaidhinisha Spotify kukutoza kiotomatiki kila mwezi hadi ughairi.

Mwongozo wa Mtumiaji

Tumeunda miongozo ya kutumia Huduma ya Spotify, ili kuhakikisha kuwa Huduma ya Spotify inaendelea kufurahiwa na kila mtu ("Miongozo ya Mtumiaji ya Spotify"). Kwa kutumia Huduma ya Spotify, lazima uzingatie Miongozo ya Mtumiaji ya Spotify na Sheria za Mfumo, na pia sheria, masharti, na kanuni zote husika na uheshimu hakibunifu, faragha, na haki nyingine za wahusika wengine.

Akaunti za Chapa

Ikiwa utaanzisha akaunti ya Spotify kwa niaba ya kampuni, shirika, taasisi, au chapa ("Chapa", na akaunti kama hiyo "Akaunti ya Chapa"), maneno "wewe" na "yako," yanavyotumika kote katika Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti mengine ya Spotify yaliyojumuishwa kwa kurejelea hapa), yatatumika kwako wewe na Chapa.

Ukifungua Akaunti ya Biashara, unawakilisha na unathibitisha kuwa umeidhinishwa kutoa ruhusa na leseni zote zinazotolewa katika Masharti (ikiwemo sheria na masharti mengine husika ya Spotify) na kuibana Chapa kwenye Masharti haya.

Chapa inaweza kufuata watumiaji na kuunda na kushiriki orodha za muziki, mradi Chapa haichukui hatua yoyote ambayo inamaanisha kuidhinisha au uhusiano wa kibiashara kati ya Chapa na mtumiaji anayefuatwa, msanii, mtunzi wa nyimbo, au mtu mwingine yeyote, isipokuwa kama Chapa kipekee imepata haki za kuashiria uthibitisho kama huo. Kwa kuongezea, Chapa lazima ziwe wazi kwa watumiaji wetu juu ya kufichua uungwaji mkono wowote au maanani yaliyotolewa kwa wasanii, watunzi wa nyimbo, watumiaji, au mtu mwingine yeyote na lazima izingatie sheria, masharti na kanuni zote zinazotumika wakati wa kushiriki shughuli zilizotajwa hapo juu.

Udhibiti na vikwazo vya mauzo ya nje

Unawakilisha na kuhakikisha kuwa (1) huishi katika, hudhibitiwi chini ya sheria za, kwa kawaida unaishi katika nchi au eneo lolote lililowekewa vikwazo vya kieneo (kwa pamoja "Nchi Zilizowekewa Vikwazo"), wala humilikiwi au kutenda kwa niaba ya serikali iliyowekewa vikwazo vya uzuiaji wa mali au mtu au shirika lolote lililobuniwa, linalopatikana au kwa kawaida linahudumu katika Nchi Iliyowekewa Vikwazo; na (2) wewe si mtu aliyetajwa kwenye, au anayemilikiwa au kudhibitiwa kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 50, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na, au unatenda kwa niaba au kwa maelekezo ya shirika lililotajwa kwenye orodha ya Umoja wa Ulaya, Uingereza, Marekani, au orodha nyingine inayotumika ya serikali ya washirika wasioruhusiwa, Kama vile Orodha Iliyojumlishwa ya watu, makundi na mashirika yaliyowekewa vikwazo vya kifedha na Umoja wa Ulaya, au Orodha Iliyojumlishwa ya Uingereza au Orodha ya Wananchi Maaalum iliyobuniwa na serikali ya Marekani.

Bidhaa za Spotify zinaweza kuwa chini ya udhibiti wa sheria za udhibiti wa mauzo ya nje na vikwazo vya kiuchumi za Umoja wa Ulaya, Uingereza, Marekani, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu Kanuni ya 2021/821 kama ilivyorekebishwa (Kanuni ya Utumiaji Mara Mbili ya Umoja wa Ulaya), Sheria ya Udhibiti wa Mauzo ya Nje ya Uingereza ya 2002, Sheria ya Udhibiti wa Mauzo ya Nje ya Uingereza ya 2002 na Sheria ya Udhibiti wa Mauzo ya Nje ya Uingereza ya 2008, Kanuni za Usimamizi wa Mauzo ya Nje zinazodumishwa na Idara ya Biashara ya Marekani, vikwazo vya biashara na kiuchumi vinavyodumishwa na Ofisi ya Idara ya Hazina ya Udhibiti wa Mali za Kigeni na Kanuni za Kimataifa za Usafiri wa Silaha zinazodumishwa na Idara ya Nchi (kwa pamoja, "Sheria za Kudhibiti Biashara").

Unakubali kutii Sheria zote husika za Udhibiti wa Biashara katika matumizi yako ya bidhaa na huduma za Spotify. Hasa, unakubali kutotumia, kuuza, kuuza nje, kurudia kuuza nje, kuhamisha, kuelekeza kwingine, kuchapisha au kuuza bidhaa, programu au teknolojia yoyote moja kwa moja au kwa njia isiyo ya - moja kwa moja - (ikijumuisha bidhaa zinazotokana na au zilizobuniwa kutokana na teknolojia hiyo) ulizopokea kutoka Spotify chini ya Sheria na Masharti haya, mahali popote, kwa shirika lolote au mtu au mtumiaji yeyote aliyezuiwa na Sheria za Udhibiti wa Biashara. Spotify haitatakiwa kuchukua hatua kwa njia yoyote ambayo hairuhusiwi chini ya Sheria za Udhibiti wa Biashara zinazotumika, na itakuwa kwa hiari ya Spotify kujizuia kuhusika moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika utoaji wa bidhaa au huduma zinazoweza kuzuiwa chini ya Sheria za Udhibiti wa Biashara zinazotumika.

4. Haki za Maudhui na Mali ya Uvumbuzi

Maudhui ya mtumiaji

Maudhui unayoyachapisha kwenye huduma

Watumiaji wa Spotify wanaweza kuchapisha, kupakia, au vinginevyo kuchangia maudhui kwenye Huduma ya Spotify ("Maudhui ya Mtumiaji"). Ili kuweka wazi, "Maudhui ya Mtumiaji" yanajumuisha maelezo, nyenzo, jumbe zote au mawasiliano mengine, na maudhui mengine yanayoongezewa, kubuniwa, kupakiwa, kuwasilishwa, kusambazwa au kuchapishwa kwenye Huduma ya Spotify na watumiaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu Maudhui ya Mtumiaji au maudhui ya mtu mwingine na udhibiti wake, angalia Sheria za Mfumo, maelezo kuhusu Hatua za Maudhui, Kituo cha Usalama & Faragha na Sera ya Malibunifu.s

Unawajibikia kibinafsi kwa Maudhui yote ya Mtumiaji unayochapisha.

Unaapa ya kwamba, kwa heshima ya Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayochapisha kwenye Spotify, (1) unamiliki au una haki ya kuchapisha Maudhui kama hayo ya Mtumiaji; na (2) Maudhui kama hayo ya Mtumiaji, au matumizi yake na Spotify kwa mujibu wa leseni iliyotolewa hpa chini, haita: (i) Kiuka Masharti haya, sheria inayotumika, au sheria za uvumbuzi au sheria zingine za mhusika mwingine yeyote; au (ii) kuashiria uhusiano wowote na au uidhinishaji wako au Maudhui yako ya Mtumiaji na Spotify au msanii yeyote, bendi, lebo, au mtu mwingine au huluki bila idhini ya awali ya maandishi kutoka Spotify au mtu ama huluki kama hiyo.

Tunaweza kukupa uwezo wa kuchapisha au kushiriki Maudhui ya Mtumiaji kwa njia tofauti, ikiwemo kwa kutuma jumbe au mawasiliano kwa watumiaji wengine wa Spotify. Kwa kuchapisha na kushiriki Maudhui ya Mtumiaji au maelezo mengine kwenye Huduma ya Spotify, tafadhali fahamu kwamba,kulingana na njia ya kuchapisha au kushiriki, maudhui na maelezo mengine yanaweza kushirikiwa kisiri kwa mtumiaji mmoja au zaidi na kushirikiwa tena na wengine kwenye Huduma ya Spotify na kwenye wavuti wote, kwa hivyo tahadhari unapochapisha au kushiriki kwenye Huduma ya Spotify, na uzingatie mipangilio ya akaunti yako. Spotify haiwajibikii kile ambacho wewe au wengine wanachapisha au wanashiriki kwenye Huduma ya Spotify.

Kufuatilia maudhui ya mtumiaji

Spotify inaweza, lakini haina wajibu wa, kufuatilia au kukagua Maudhui ya Mtumiaji (yawe yamechapishwa hadharani ay kushikikiwa kisiri). Spotify ina haki ya kuondoa au kulemaza ufikiaji wa Maudhui yoyote ya Mtumiaji kwa sababu yoyote au bila sababu. Spotify inaweza kuchukuwa hatua bila notisi ya kabla kwako.

Leseni unazotupatia

Maudhui ya Mtumiaji

Unabaki kuwa mmiliki wa Maudhui yako ya Mtumiaji unapoyachapisha kwenye Huduma. Hata hivyo, ili tuweze kufanya Maudhui yako ya Mtumiaji yapatikane kwenye Huduma ya Spotify na kukupa vipengele na hali fulani za utumiaji, tunahitaji kutoka kwako leseni inayodhibitiwa ya Maudhui hayo ya Mtumiaji. Kwa hivyo, unaipa Spotify leseni isiyo ya kipekee, ya kuhamisha, ya kugawa, isiyo ya mrabaha, iliyolipiwa kikamilifu, isiyobatilika ya duniani kote ili kuzalisha tena, kufanya kupatikana, kutekeleza na kuonyesha, kutafsiri, kurekebisha, kuunda kazi za mwigo, kusambaza na vinginevyo kutumia Maudhui yoyote ya Mtumiaji kupitia chombo chochote, yawe pekee au pamoja na Maudhui au nyenzo nyingine, kwa namna na kwa njia, mbinu au teknolojia yoyote, iwe inajulikana sasa au iundwe baadaye, kuhusiana na Huduma ya Spotify. Mahali inatumika na kwa kiwango cha sheria inayotumika, pia unakubali kuondoa na kutotekeleza "haki zozote za maadili" au haki kama hizo, kama vile haki yako ya kutambuliwa kama mwandishi wa Maudhui yoyote ya Mtumiaji, kwa kujumuish Maoni, na haki yako ya kukataa kutumiwa kwa Maudhui ya Mtumiaji kama hayo bila heshima.

Maoni

Ukitoa hoja, mapendekezo, au maoni mengine kuhusiana na matumizi yako ya Huduma ya Spotify au Maudhui yoyote ("Maoni"), Maoni hayo si ya siri na yanaweza kutumiwa na Spotify bila kikwazo na bila malipo kwako. Maoni yanazingatiwa kuwa aina ya Maudhui ya Mtumiaji chini ya Masharti haya.

Kifaa Chako.

Pia unatupa haki ya (1) kuruhusu Huduma ya Spotify kutumia kichakataji, kipimo data, na maunzi ya kuhifadhai kwenye Kifaa chako ili kuwezesha shughuli ya Huduma ya Spotify, na (2) kukupa matangazo na maelezo mengine, na kuwaruhusu washirika wetu wa biashara kufanya vivyo hivyo, kama inavyoruhusiwa kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Spotify.

Hali ya utumiaji wa maudhui

Huku Spotify, tunalenga kuunda uzoefu mzuri na wa kipekee kwa kila mtumiaji. Katika Kuelewa mapendekezo kuhusu Spotify, unaweza kujifunza mengi zaidi kuhusu jinsi mifumo yetu ya mapendekezo hufanya kazi, ikiwemo jinsi na kwa nini maudhui fulani yataonyeshwa kwako. Katika sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify, Maudhui unayofikia, kwa kujumuisha uchaguzi na uwekaji wake, yanaweza kuathiriwa na uzingatiaji wa kibiashara, kwa kujumuisha makubaliano ya Spotify na wahusika wengine.

Maudhui mengine yaliyoruhusiwa na, kutolewa kwa, kuundwa na au vinginevyo kuwezeshwa kupatikana na Spotify (k.v. matangazo ya sauti) yanaweza kujumuisha matangazo na Spotify haiwajibikii matangazo yoyote kama hayo.

Madai ya ukiukaji

Spotify inaheshimu haki za wamiliki wa mali ya uvumbuzi. Ikiwa unaamini kuwa Maudhui yoyote yanakiuka haki zako za hakimiliki, chapa ya biashara au haki nyingine za mali ya uvumbuzi, tafadhalia angalia Sera ya Mali ya Uvumbuzi ya Spotify.

5. Usaidizi, Maelezo, Maswali na Malalamishi ya Mteja

Jumuia ya Usaidizi wa Spotify

Jumuiya ya Usaidizi ya Spotifyni mahali pa majadiliano na ubadilishanaji wa maelezo, vidokezo, na nyenzo zingine zinazohusiana na Huduma ya Spotify. Kwa kutumia Jumuia ya Usaidizi ya Spotify, unakubali Masharti ya Jumuia.

Usaidizi, Maelezo, Maswali, Malalamishi ya Mteja

Kwa usaidizi kwa wateja walio na maswali yanayohusiana na- akaunti na malipo- ("Maswali ya Usaidizi kwa Wateja"), tafadhali tumia rasilimali za Usaidizi kwa Wateja zilizoorodheshwa kwenye sehrmu ya Kutuhusu ya tovuti yetu.

Ikiwa una swali lolote kuhusu Huduma ya Spotify au Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada ya Spotify yaliyojumuishwa humu), tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja wa Spotify kwa kutembelea sehemu ya Kutuhusu ya tovuti yetu.

6. Matatizo na Migogoro

Kusimamisha na kukomesha Huduma ya Spotify

Sheria na Masharti haya yataendelea kutumika hadi utakapoyakomesha au yatakapokomeshwa na Spotify. Spotify inaweza kukomesha Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada yaliyojumuishwa humu) au kusimamisha ufikiaji wako wa Huduma ya Spotify wakati wowote ikiwa tunaamini kwamba umekiuka Masharti haya, tukiacha kutoa Huduma ya Spotify au kipengee chochote cha nyenzo kwenye notisi inayofaa kwako, au tunapoamini ni muhimu kutii sheria husika. Ikiwa wewe au Spotify itakomesha Masharti haya, au ikiwa Spotify inasimamisha ufikiaji wako wa Huduma ya Spotify, unakubali kuwa Spotify haitakuwa na dhima wala wajibu kwako kulingana na sheria husika na (isipokuwa kama ilivyobainishwa katika Masharti haya) Spotify haitarejesha pesa zozote ambazo tayari umelipa. Unaweza kukomesha Masharti haya wakati wowote, ambapo huwezi kuendelea kufikia wala kutumia Huduma ya Spotify. Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufunga akaunti yako ya Spotify, tafadhali tumia huduma za Usaidizi kwa Wateja zilizowekwa kwenye ukurasa wetu wa Kutuhusu.

Sehemu za 4 (Maudhui na Hakibunifu), 3 (Matumizi Yako ya Huduma ya Spotify), 2 (Huduma ya Spotify Tunayotoa), 6 (Matatizo na Migogoro), 7 (Kuhusu Masharti haya) humu, na pia sehemu nyingine zozote za Masharti haya ambazo lazima ziendelee kutumika hata baada ya ukomeshaji wa Masharti haya kwa njia ya wazi au hali yake ya asilia, hayatakomeshwa.

Makanusho ya hakikisho

Baadhi ya mamlaka hayaruhusu uondoaji wa mahakikisho au vikomo vinavyodokezwa kwenye haki za sheria husika za mtumiaji, hivyo uondoaji na vikomo katika sehemu hii huenda visitumike kwako na hakuna kitakachoathiri haki zako za kisheria.

Spotify itatoa Huduma ya Spotify kwa kutumia utunzaji na ujuzi unaofaa na kwa mujibu wa maelezo yoyote ya Huduma ya Spotify yanayotolewa na Spotify, hata hivyo, kulingana na hiyo, Huduma ya Spotify inatolewa na "kama ilivyo" na "kama inavyopatikana," bila mahakikisho ya aina yoyote, yawe ya bayana, yanayodokezwa, au ya kisheria. Vilevile, Spotify na wamiliki wote wa maudhui wanakanusha mahakikisho yoyote ya wazi, ya kudokezwa na ya kisheria kuhusu maudhui, ikiwemo mahakikisho ya ubora wa kuridhisha, uwezo kuuzika, ufaafu kwa madhumuni fulani, au kutokiuka. Si Spotify wala mmiliki yeyote wa maudhui anatoa udhamini kwamba huduma ya Spotify haina programu hasidi au vifaa vingine hatari. Kwa kuongezea, Spotify haifanyi uwakilishi wala haitoi udhamini, kuthibitisha, kuhakikisha, au kuwajibikia programu zozote za mhusika wa tatu (au maudhui yaliyomo), maudhui ya mtumiaji, vifaa au bidhaa nyingine yoyote au huduma inayotangazwa, inayouzwa au kutolewa na mhusika wa tatu kwenye au kupitia huduma ya Spotify au tovuti yoyote iliyotolewa kiungo, au iliyoonyeshwa kwenye bango lolote au utangazaji mwingine na Spotify haiwajibiki kwa biashara yoyote kati yako na watoaji wa huduma za mhusika wa tatu inayoendelea. Hakuna ushauri au maelezo iwe kwa matamshi au kwa maandishi unayopata kwenye Spotify yataunda hakikisho lolote kwa niaba ya Spotify. Wakati unatumia huduma ya Spotify, unaweza kupata ufikiaji kwa vipengee vya kuchuja maudhui, lakini matumizi ya vipengee hivi bado yanaweza kusababisha maudhui ya kina kutolewa kwako na usitegemee vipengee kama hivyo kujuja maudhui yote ya kina. Sehemu hii inatumika kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria inayotumika.

Kikomo cha Dhima na Wakati wa Kuwasilisha Dai

Kulingana na sheria husika, unakubali kuwa suluhisho lako la pekee kwa matatizo au kutoridhishwa na Huduma ya Spotify ni kusakinusha programu yoyote ya Spotify na kuacha kutumia Huduma ya Spotify. Wewe unakubali kuwa Spotify haina wajibu au uwajibikaji unaotokana na au kuhusiana na programu za mhusika wa tatu au maudhui hayo yaliyopatikana kupitia au kwa kuungana na Huduma ya Spotify, na wakati uhusiano wako na programu kama hizo za mhusika wa tatu unaweza kuongozwa na makubaliano tofauti na hao wahusika wa tatu, utatuzi wako wa pekee na binafsi, kuhusiana na Spotify, kwa matatizo yoyote au kutoridhika na programu za mhusika wa tatu, au maudhui yaliyomo, ni kusakinua na/au kuacha kutumia programu kama hizo za mhusika wa tatu.

Hakuna wakati ambapo Spotify, maafisa, wadau, waajiriwa, mawakala, wakurugenzi, mashirika tanzu, warithi, wahawilishaji, wagawaji, au watoa leseni wake watawajibikia (1) uharibifu wowote usio wa moja kwa moja, maalum, unaoambatana, wa adhabu, funzo au unaoandamana; (2) hasara yoyote ya matumizi, data, biashara au faida (iwe moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja), katika kesi zote zinazotokana na matumizi ya au kutoweza kutumia Huduma ya Spotify, vifaa, programu za wahusika wengine, au maudhui ya programu ya mhusika mwingine; au (3) dhima ya jumla ya madai yote yanayohusiana na Huduma ya Spotify, programu za mhusika mwingine au maudhui ya programu ya mhusika mwingine zaidi ya (a) pesa ulizolipa Spotify wakati wa miezi kumi na miwili kabla ya dai la kwanza; au (b) $30.00. Dhima yoyote tuliyo nayo kwa hasara uliyopata ni ya hasara tu ambazo ziliweza kutabirika.

Kwa uthibitishaji, masharti haya hayazuii dhima ya Spotify kwa ajili ya udanganyifu, uwasilishaji mbaya wa udanganyifu, kifo au jeraha la binafsi kwa kiwango ambacho sheria husika itazuia kikomo kama hicho na kwa dhima nyingine yoyote ambayo, kwa sheria husika, huenda isiwe na kikomo wala kuondolewa.

Isipokuwa pale ambapo vikwazo hivyo vinapigwa marufuku chini ya sheria husika, dai lolote linalotokana na masharti haya lazima lianzishwe (kwa kuwasilisha dai la rufaa au kuwasilisha hatua ya binafsi chini ya makubaliano ya rufaa yaliyo hapa chini) ndani ya mwaka mmoja (1) baada ya tarehe ambayo mtu anayeweka madai kwanza afahamu au kwa kweli inapaswa kufahamu juu ya kitendo hicho, upungufu, au kasoro inayosababisha madai; na hakutakuwa na haki kwa suluhisho lolote la madai yoyote ambayo hayadaiwi katika kipindi hicho cha wakati.

Haki za Watu Wengine

Unathibitisha na kukubali kuwa wamiliki wa Maudhui na wasambazaji fulani (kama vile watoa huduma ya duka la programu) ndio wanaokusudiwa kufaidika na Sheria na Masharti haya na wana haki ya kutekeleza Sheria na Masharti haya moja kwa moja dhidi yako. Kando na jinsi ilivyoainishwa katika sehemu hii, Masharti haya hayajakusudiwa kutoa haki kwa mtu yeyote isipokuwa wewe na Spotify, na kwa vyovyote vile Masharti haya huunda haki za mnufaika wa mhusika wa tatu.

Ikiwa umepakua programu yetu yoyote ya kifaa cha mkononi (kila moja, "Programu") kutoka Apple Inc. ("Apple") App Store au ikiwa unatumia Programu kwenye kifaa cha iOS, unathibitisha kuwa umesoma, umeelewa, na unakubali taarifa ifuatayo kuhusu Apple. Masharti haya ni kati yako na Spotify pekee, sio na Apple, na Apple haiwajibiki kwa Huduma ya Spotify na maudhui yaliyomo. Apple haina wajibu wowote wa kutoa huduma zozote za matengenezo na msaada kuhusiana na Huduma ya Spotify. Katika tukio la kushindwa kokote kwa Huduma ya Spotify kutii udhamini unaotumika, unaweza kuarifu Apple na Apple itarejesha bei inayotumika ya ununuzi wa Programu kwako; na, kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria inayotumika, Apple haina jukumu jingine la dhamana kuhusiana na Huduma ya Spotify. Apple haiwajibiki kushughulikia madai yoyote yako au mtu mwingine kuhusiana na Huduma ya Spotify au umiliki wako au matumizi ya Huduma ya Spotify, ikiwemo: (1) madai ya dhima ya bidhaa; (2) dai lolote kwamba Huduma ya Spotify inakosa kutii matakwa yoyote yanayotumika ya kisheria au udhibiti; (3) madai yanayotokana na ulinzi wa walaji au sheria sawa; na (4) madai yanayotokana na ukiukaji wa hakimiliki. Apple haiwajibiki kwa uchunguzi, utetezi, uamuzi, na kutolewa kwa madai ya mhusika yeyote mwingine kwamba Huduma ya Spotify au milki yako na utumiaji wa Programu zinakiuka haki za hakimiliki ya mhusika huyo mwingine. Unakubali kufuata masharti yoyote yanayotumika ya mhusika wa tatu, unapotumia Huduma ya Spotify. Apple, na kampuni tanzu za Apple, ni wanufaishwa wengine wa Sheria na Masharti haya, na unapokubali Sheria na Masharti haya, Apple itakuwa na haki (na itachukuliwa kuwa imekubali haki hiyo) ya kutekeleza Sheria na Masharti haya dhidi yako kama mnufaishwa mwingine wa Sheria na Masharti haya.

Kulipa fidia

Unakubali kufidia na kushikilia Spotify bila madhara kutoka na dhidi ya hasara zozote za moja kwa moja zinazoweza kutokea, uharibifu na gharama zinzaofaa (ikiwemo ada na gharama zinazofaa za wakili) zinazoathiriwa au kutozwa na Spotify kutokana na au kuhusiana na: (1) ukiukaji wako ya yoyote ya Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada ya Spotify yaliyojumuishwa hapa); (2) Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayochapisha au vinginevyo kuchangia; (3) shughuli yoyote unayoshiriki kwenye au kupitia Huduma ya Spotify; na (4) ukiujaji wako wa sheria yoyote ay haki za mhusika mwingine.

Sheria Simamizi, Upatanisho wa Lazima na Mahali

6.1 Sheria / Mamlakad ya Utawala

Isipokuwa vinginevyo inavyotakiwa na sheria za lazima katika nchi ya makazi, Makubaliano (na mizozo yoyote/madai yoyote yasiyokuwa ya kandarasi yanayotokana au yanayohusiana nayo) yanatii sheria za serikali au nchi zilizoorodheshwa hapa chini, bila kuzingatia uchaguzi au migongano ya kanuni za sheria.

Vilevile, wewe na Spotify mnakubali mamlaka ya mahakama yaliyoorodheshwa hapa chini kusuluhisha mgogoro, dai au mabishano yoyote yanayotokea kuhusiana na Makubaliano (na migogoro/madai yoyote yasiyo ya mkataba yanayotokana na au kuhusiana nayo), isipokuwa pale ambapo chini ya sheria za lazima husika, unaweza kuchagua kuwasilisha kesi za kisheria katika nchi yako, au tunahitajika kuwasilisha kesi za kisheria katika nchi yako

Nchi au eneo
Uchaguzi wa Sheria
Mamlaka
Nchi na maeneo mengine yote ambayo Spotify inapatikana.
Sheria za Uswidi
Kipekee; Mahakama za Uswidi
Bulgaria, Saiprasi, Estonia, Ufaransa, Hong Kong, Lativia, Lithuania, Luxemburg, Malta, Monaco, Norway, Ufilipino, Ureno, Slovakia, Uhispania, Uturuki
Sheria za Uswidi
Zisizo za Kipekee; Mahakama za Uswidi
Brazil
Sheria za Brazil
Kipekee; Mahakama za Jimbo na Shirikisho la São Paulo, Jimbo la São Paulo, Brazili
Kanada
Haitumiki kwa wakazi wa of Kwebeki: Sheria za Mkoa wa Ontario
Wakazi wa Kwebeki: Sheria za Mkoa wa Kwebeki, Kanada
Haitumiki kwa wakazi wa of Kwebeki: Isipokuwa kwa madhumuni ya kutekeleza hukumu; Mahakama za Ontario, Kanada
Wakazi wa Kwebeki: Mahakama za Kwebeki, Kanada
Bolivia, Chile, Kolombia, Kosta Rika, Jamhuri ya Dominika, Ekwado, El Salvador, Guatemala, Honduras, Nikaragua, Panama, Paraguay, Peru, Uruguay
Jimbo la New York, Marekani
Ya Kipekee; Mahakama za Jimbo na Shirikisho za New York, NY

6.2 ONDOLEO LA KESI LA KUNDI

PANAPORUHUSIWA CHINI YA SHERIA INAYOTUMIKA, WEWE NA SPOTIFY MNAKUBALI KUWA KILA MHUSIKA ANAWEZA KUWASILISHA MADAI DHIDI YA MWINGINE KATIKA HALI YA KIBINAFSI PEKEE NA WALA SI KAMA MLALAMIKAJI AU MSHIRIKA WA KIKUNDI KATIKA KIKUNDI CHAKO HUSIKA AU MWAKILISHI WA KIKUNDI. Isipokuwa wewe na Spotify mkubaliane, hakuna mpatanishi au hakimu anayeweza kujumuisha zaidi ya madai ya mtu mmoja au kusimamia aina yoyote ya kesi ya mwakilishi au kikundi.

6.3 UPATANISHO

Ikiwa unakaa, unaishi, una ofisi au unafanya biashara katika eneo ambako Sehemu hii ya 6.3 inaweza kutekelezwa, vifungu vifuatavyo vya upatanisho wa lazima vitatumika kwako.

6.3.1 Utatuzi na usuluhishi wa migogoro

Wewe na Spotify mnakubali kuwa mzozo wowote, dai, au ubishani kati yako na Spotify unaotokana na au unaohusiana kwa njia yoyote na Makubaliano haya au kwa uhusiano wako na Spotify kama mtumiaji wa Huduma (iwe ni kwa kandarasi, mateso, sheria, ulaghai, uwakilishi mbaya, au nadharia nyingine yoyote ya kisheria, na ikiwa madai yanatokea wakati wa au baada ya kukatiza Makubaliano) utaamuliwa na usuluhishi wa lazima wa mtu binafsi. Upatanisho si rasmi zaidi kuliko kesi ya mahakamani. HAKUNA HAKIMU AU MWAMUZI KATIKA UPATANISHO, NA KWAMBA UKAGUZI WA MAHAKAMA WA TUZO YA UPATANISHO UNA KIKOMO. Kunaweza kuwa na matokeo machache zaidi ya uchunguzi kuliko mahakamani. Msuluhishi lazima afuate makubaliano haya na anaweza kutoa uharibifu sawa na unafuu kama mahakama (pamoja na ada ya wakili), isipokuwa kwamba msuluhishi hawezi kutoa unafuu wa tamko au amri ya kumnufaisha mtu yeyote isipokuwa wahusika kwenye usuluhishi. Kifungu hiki cha usuluhishi hakitakomeshwa kwa ukatizaji wa Makubaliano.

6.3.2 Mambo ya kipekee

Bila kujali kifungu cha 6.3.1 hapo juu, wewe na Spotify wote mnakubali kwamba hakuna kitu hapa kitachotupiliwa mbali, kuzuia, au vinginevyo kupunguza mipaka ya haki zetu, wakati wowote, ili (1) kuleta hatua ya mtu binafsi katika mahakama ndogo ya madai, ( 2) kufuata hatua za utekelezaji kupitia wakala wa shirikisho, serikali, au wakala husika wa ndani ambapo vitendo kama hivyo vinapatikana, (3) kutafuta afueni ya kisheria katika mahakama ya sheria, au (4) kufungua kesi katika mahakama ya sheria ili kushughulikia madai ya ukiukaji wa mali miliki.

6.3.3 Kanuni za usuluhishi

Wewe au sisi tunaweza kuwasilisha kesi za upatanisho. Usuluhishi wowote kati yako na Spotify hatimaye utasuluhishwa chini ya Kanuni za Usuluhishi za Jumba la Biashara la Kimataifa ("ICC") zinazofanya kazi wakati huo ("Sheria za ICC") na msuluhishi mmoja au zaidi walioteuliwa kwa mujibu wa Kanuni za ICC, kama ilivyobadilishwa na Makubaliano haya, na utasimamiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya ICC.

Usuluhishi wowote utafanywa kwa lugha ya Kiingereza na isipokuwa vinginevyo ikitakiwa na sheria ya lazima ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya au mamlaka nyingine yoyote, sheria ya kutumika katika usuluhishi wowote itakuwa sheria ya [jimbo husika au nchi iliyoelezwa katika kifungu cha 6.1], bila kuzingatia uchaguzi au migogoro ya kanuni za sheria.

6.3.4 Wakati wa kufungua kesi

Upatanisho wowote lazima uanzishwe kwa kuwasilisha dai la upatanisho ndani ya kipindi cha MWAKA MMOJA (1) baada ya tarehe ambayo mhusika anayewasilisha dai anajua kwa mara ya kwanza au anapaswa kujua kitendo, kutotendeka, au kosa linalosababisha dai hilo; na hakutakuwa na haki ya kupata suluhu yoyote kwa dai lolote ambalo halikuwasilishwa katika kipindi hicho. Ikiwa sheria inayotumika hairuhusu kikomo cha kipindi cha mwaka mmoja kwa uwasilishaji wa madai, dai lolote lazima liwasilishwe ndani ya muda mfupi zaidi unaoruhusiwa na sheria inayotumika.

6.3.5 Ilani; Mchakato

Mtu ambaye anakusudia kutafuta usuluhishi lazima kwanza atume ilani ya maandishi ya mzozo kwa mwingine, kwa barua iliyothibitishwa au Federal Express (sahihi inahitajika), au ikiwa hakuna anwani ya mahali kwenye faili, kwa barua ya kielektroniki ("Ilani"). Anwani ya Spotify ya Notisi ni: [Spotify, Kwa: Genera Counsel, 4 World Trade Center, 150 Greenwich Street, Ghorofa ya 62, New York, NY 10007 Ilani lazima (1) ieleze asili na msingi wa madai au mzozo; na (2) kuweka wazi unafuu maalum unaotafutwa ("Mahitaji"). Tunakubali kujitahidi kwa nia njema kusuluhisha dai hilo moja kwa moja, lakini tusipofikia makubaliano ya kulisuluhisha ndani ya siku 30 baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa, wewe au Spotify inaweza kuwasilisha kesi ya upatanisho. Wakati wa upatanisho, kiasi cha malipo yoyote ambayo wewe au Spotify inatoa hakitafichuliwa kwa mpatanishi hadi mpatanishi atakapotoa uamuzi wa mwisho na tuzo, ikiwa ipo. Endapo mzozo wetu hatimaye unasuluhishwa kwa njia ya usuluhishi kwa kukupendelea, Spotify itakulipa (1) kiwango kilichotolewa na msuluhishi, ikiwa kipo, (2) kiasi cha mwisho cha malipo kilichoandikwa kilichotolewa na Spotify katika kusuluhisha mzozo kabla ya tuzo ya msuluhishi; au (3) $ 1,000.00, yoyote iliyo kubwa. Hati na maelezo yote yatakayofichuliwa katika utaratibu wa upatanisho yatahifadhiwa kwa usiri na mpokeaji na hayatatumiwa na mpokeaji kwa kusudi lolote isipokuwa kwa makusudi ya upatanisho au utekelezaji wa uamuzi na tuzo ya mpatanishi na hayatafichuliwa isipokuwa kwa usiri kwa watu ambao wanahitaji kuyajua kwa makusudi kama hayo au kama inavyotakiwa na sheria inayotumika. Isipokuwa kama inavyotakiwa ili kutekeleza uamuzi na tuzo ya mpatanishi, wewe au Spotify hampaswi kutoa tangazo lolote kwa umma au maoni ya umma au kusababisha ufichuzi wowote kuhusiana na upatanisho, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, ukweli kwamba kuna mgogoro kati ya wahusika, uwepo wa upatanisho, au uamuzi au tuzo yoyote ya mpatanishi.

6.3.6 Marekebisho

Iwapo Spotify itafanya mabadiliko yoyote ya baadaye kwa kifungu hiki cha upatanisho (isipokuwa kwa mabadiliko ya anwani ya Spotify ya kutuma Taarifa), unaweza kukataa badiliko lolote kama hilo kwa kututumia taarifa ya maandishi ndani ya siku 30 baada ya kufanywa kwa mabadiliko kwa anwani ya Spotify ya kutuma Taarifa, ambapo akaunti yako na Spotify itafungwa mara moja na kifungu hiki cha upatanisho, kama kinavyotumika mapema kabla ya marekebisho unayoyakataa, kitaendelea kutumika.

6.3.7 Utekelezaji

Ikiwa ondoleo la kesi ya kundi katika Sehemu ya 6.2 linapatikana kutoweza kutekelezeka katika usuluhishi au ikiwa sehemu yoyote ya Sehemu hii ya 6.3 itapatikana kuwa batili au haiwezi kutekelezeka, basi ukamilifu wa Sehemu hii ya 6.3 itakuwa batili na, kwa hali kama hiyo, wahusika wanakubaliana kuwa mamlaka ya kipekee na ukumbi ulioelezewa katika Sehemu ya 6.1 itasimamia hatua yoyote inayotokana na au inayohusiana na Makubaliano na hutazuiliwa kuwasilisha kesi wakati wowote.

7. Kuhusu Sheria Hizi

Chini ya sheria inayotumika, huenda ukawa na haki fulani ambazo haziwezi kuzuiwa na mkataba. Sheria na Masharti haya hayanuii kwa njia yoyote kuzuia haki hizo.

Mabadiliko

Tunaweza kufanya mabadiliko kwenye Masharti haya (ikiwemo sheria na masharti yoyote ya ziada ya Spotify yaliyojumuishwa na rejeo lililo humu) mara kwa mara kwa kukuarifu kuhusu mabadiliko hayo kwa njia yoyote inayofaa (kabla hayajaanza kutumika), ikiwemo kwa kuchapisha Makubaliano yaliyorekebishwa kuhusu Huduma ya Spotify husika (mradi tu, kwa mabadiliko ya nyenzo, tutajitahidi kuongeza ilani hiyo kwa barua pepe, ujumbe wa ibukizi ya huduma ya ndani, au njia nyinginezo). Mabadiliko yoyote kama hayo hayatatumika kwa mgogoro wowote kati yako na sisi unaotokea kabla ya tarehe ambayo tulichapisha Sheria na Masharti yaliyorekebishwa, au sheria na masharti mengine ya Spotify, yanayojumuisha mabadiliko hayo, au kukuarifu kuhusu mabadiliko hayo. Matumizi yako ya Huduma ya Spotify baada ya mabadiliko yoyote kwenye Masharti haya yatahusu ukubalifu wako wa mabadiliko hayo. Ikiwa usingependa kuendelea kutumia Huduma ya Spotify chini ya Masharti yaliyosasishwa, unaweza kukomesha akaunti yako kwa kuwasiliana nasi. Tarehe ya kuanza kutumika iliyowekwa juu ya hati hii inaonyesha wakati ambapo Sheria hizi zilipobadilishwa mara ya mwisho.

Makubaliano Yote

Kando na jinsi ilivyoelezwa katika sehemu hii au kama ilivyokubaliwa wazi kwa maandishi kati yako na Spotify, Sheria na Masharti haya yanaunda sheria na masharti yote yaliyokubaliwa kati yako na Spotify na yanachukua nafasi ya makubaliano yoyote ya awali kuhusiana na suala kuu la Sheria na Masharti haya, iwe kwa maandishi au kwa matamshi. Kama ilivyotajwa hapo juu, sheria na masharti mengine, miongozo na sera zinazosimamia matumizi ya Huduma ya Spotify zimejumuishwa hapa kwa njia ya marejeleo. Haya yanajumuisha yafuatayo: (a) sheria na masharti ya ziada yanayohusiana na huduma mahususi zinazotlewa kwenye Huduma ya Spotify: Masharti ya Ofa ya Uendelezaji ya Spotify Premium;Masharti ya Kadi ya Spotify na Masharti ya Jumuiya ya Usaidizi ya Spotify;na (b) miongozo na sera: Sera ya Faragha ya Spotify; Miongozo ya Mtumiaji ya Spotify; Sheria za Mfumo za Spotify na Sera ya Miliki ya Spotify.

Upekee na Ondoleo la Haki

Isipokuwa kama ilivyotajwa katika Sheria na Masharti haya, iwapo kifungu chochote cha Sheria na Masharti haya kitachukuliwa kuwa si halali au kisichoweza kutekelezwa kwa sababu yoyote au kwa kiwango chochote, vifungu vilivyosalia vya Sheria na Masharti haya havitaathiriwa na matumizi ya kifungu hicho yatatekelezwa kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria.

Hali yoyote ya Spotify au mnufaika mwingine ya kutoweza kutekeleza Sheria hizi au kifungu chochote haitaondoa haki ya Spotify au ya mnufaika mwingine kufanya hivyo.

Ukabidhi

Spotify inaweza kukabidhi Sheria na Masharti haya yoyote/yote, na inaweza kukabidhi au kupeana, haki au majukumu yake yote au sehemu yake chini ya Sheria na Masharti haya. Hupaswi kukabidhi Sheria na Masharti haya, yote au sehemu yake, au kuhamisha au kutoa leseni ndogo ya haki zako chini ya Sheria na Masharti haya, kwa mtu mwingine yeyote.