Unaweza kupakua nyimbo 30 kwenye kifaa kimoja cha mkononi, kisha ucheze orodha ya Nyimbo Ulizopakua bila WiFi au huduma isipokuwepo.
Usipoongeza salio la Mini kabla muda wa kutumia mpango wako haujaisha, utabadilishiwa utumie mpango wetu usiolipishwa. Utaendelea kutumia maktaba na orodha zako za kucheza, lakini nyimbo zako ulizopakua zitaondolewa. Ukirudi kutumia Mini baada ya kutumia mpango wetu usiolipishwa, unaweza kupakua tena orodha ya kucheza uliyokuwa nayo ya Nyimbo Ulizopakua.
Ukishapakua nyimbo 30, utahitaji kuondoa baadhi iwapo ungependa kupakua zaidi. Ikiwa unataka zaidi ya nyimbo 30, jaribu moja ya mipango yetu mingine ya Premium ili upate nyimbo 10,000 kwenye kila kifaa, kwenye hadi vifaa 5 kwa kila akaunti.
Hapana, unaruhusiwa kuwa na nyimbo 30 pekee ulizopakua kwenye kifaa chako wakati wowote. Ikiwa ungependa kupakua nyimbo zaidi, angalia Premium ya Binafsi, inayokuruhusu kupakua nyimbo 10,000 kwenye kila kifaa, kwenye hadi vifaa 5 kwa kila akaunti.
Kwa chaguomsingi, kutiririsha kwa saa moja hutumia takriban MB 10 za data. Kupakua wimbo mmoja wa dakika 3 kutatumia takriban MB 0.5 za nafasi kwenye kifaa chako. Ili uokoe data, tiririsha kupitia WiFi, na hakikisha kuwa mipangilio yako ya kutiririsha imewekwa kuwa: Chini kwa ajili ya kutiririsha, Kawaida kwa ajili ya kupakua.
Unaweza kuongeza Premium zaidi kwenye akaunti yako wakati wowote. Ikiwa bado unatumia Premium wakati unaongeza salio, basi siku mpya zitaanza kuhesabiwa siku zako zilizopo zitakapoisha. Unaweza kuongeza salio la akaunti yako kwa hadi miezi 3 ya Premium ukinunua Mini.
Kumbuka kuwa wakati wowote unaorudisha mpango wetu usiolipishwa, nyimbo ulizopakua zitaondolewa na utahitaji kuzipakua upya utakaporudi kutumia Premium.
Unaweza kufikia akaunti yako ya Spotify kwenye vifaa vingi, lakini Mini hufanya kazi kwenye simu ya mkononi au tablet ndogo pekee (chini ya inchi 7). Bado utaweza kutumia bila malipo kwenye kifaa kingine chochote kisicho cha mkononi wakati unatumia kifurushi kinachotumika cha Premium Mini.