Nenda kwenye maudhui
Spotify
  • Premium
  • Usaidizi
  • Pakua
  • Jisajili
  • Ingia katika akaunti
  • Sheria
  • Vigezo na Masharti ya Kutumia
  • Sera ya Hakimiliki
  • Sera ya Faragha

Sheria na Masharti ya Spotify

Kufanya kazi kuanzia 23/02/2021

1 Utangulizi

2 Mabadiliko kwenye Makubaliano

3 Kufurahia Spotify

4 Malipo, kughairi, na kutuliza

5 Kutumia huduma zetu

6 Programu na Vifaa vya Mhusika wa Tatu

7 Maudhui Yanayoundwa na Mtumiaji

8 Haki unazotupa

9 Miongozo ya mtumiaji

10 Ukiukaji na kuripoti Maudhui ya Mtumiaji

11 Vikomo na maboresho kwa huduma

12 Akaunti za Chapa

13 Jumuia ya Usaidizi wa Spotify

14 Usaidizi kwa Wateja

15 Udhibiti wa uhamishaji

16 Masharti na ukomeshaji

17 Kanusho la hakikisho

18 Ukomo

19 Haki za mhusika wa tatu

20 makubaliano yote

21 Kutenganishwa, ondoleo na ufasiri

22 Kazi

23 Kuondolea lawama

24 Chaguo la sheria, usuluhishaji wa lazima, na mahali

25 Wasiliana nasi

Hujambo, na karibu kwenye Sheria na Masharti ya Utumiaji wa Spotify ("Masharti"). Masharti unayoyaona hapa chini ni muhimu kwa sababu:

  • Yanaorodhesha haki zako za kisheria kwenye Spotify
  • Yanafafanua haki unazotupa wakati unapotumia Spotify
  • Yanaelezea sheria ambazo kila mmoja anahitaji kufuata wakati anapotumia Spotify
  • Yana msamaha wa hatua na makubaliano kuhusu jinsi ya kusuluhisha migogoro yoyote inayoweza kutokea kwa usuluhishaji

Tafadhali soma Masharti haya, Sera ya Faragha na masharti mengine yoyote yanayorejelewa katika waraka huu kwa makini. Tunatarajia umeketi vizuri na unasikiliza muziki mzuri.

Hapa tunaanza...

1 Utangulizi

Asante kwa kuchagua Spotify ("Spotify," "sisi," "sisi," "yetu"). Spotify inatoa huduma zilizobinafsishwa na vipengee vya kijamii na kuingiliana kwa muziki mzuri na maudhui mengine pamoja na bidha nyingine na huduma ambazo zinaweza kuundwa kila mara. Kwa kujisajili au vinginevyo kutumia yoyote kati ya huduma za Spotify, kwa kujumuisha vipengee vyote vinavyohusika na utendaji kazi, tovuti na violesura vya mtumiaji, pamoja na maudhui yote na programu zinazohusiana na huduma zetu (kijumla,"Huduma ya Spotify" au "Huduma"), au kufikia muziki wowote, video au maudhui yoyote au nyenzo inayopatikana kupitia Huduma ("Maudhui") unaingia katika kandarasi ya makubaliano na kampuni ya Spotify iliyoonyeshwa kwenye Sehemu ya 25 (Wasiliana nasi).

Makubaliano yako nasi yanajumuisha Masharti haya na masharti mengine yoyote ya ziada unayokubaliana, jinsi ilivyojadiliwa katika sehemu ya Makubaliano Yote, iliyo hapa chini, kando na masharti ya mhusika wa tatu (kwa pamoja, "Makubaliano"). Makubaliano yanajumuisha masharti yanayohusiana na mabadiliko ya mbeleni kwene Makubaliano, vidhibiti vya uhamishaji, kufanya upya kiotomatiki, ukomo wa dhima, faragha, ondeleo la hatuana usuluhishaji wa migogoro kwa kuzungumza badala ya mahakama. Ikiwa ungependa kupitia kwenye masharti ya Makubaliano, toleo la makubaliano linalotumika kwa sasa linaweza kupatikana kwenye tovuti ya Spotify. Unakubali kwamba umesoma na kuelewa Makubaliano, unakubali Makubaliano haya, na unakubali kuyatii. Ikiwa hukubaliani na (au huwezi kutii) Makubaliano, basi hutaweza kuitumia Huduma ya Spotify wala kufikia Maudhui yoyote.

Ili kuitumia Huduma ya Spotify Service na kufikia Maudhui yoyote, unahitaji (1) kutimiza mahitaji ya umri kwenye chati iliyo hapa chini, (2) uwe na uwezo wa kuingia kwenye kandarasi ya makubaliano nasi na kutozuiliwa kufanya hivyo chini ya sheria zinazotumika, na (3) kuishi katika nchi ambayo Huduma inapatikana. Pia unaahidi kuwa taarifa yoyote ya usajili unayowasilisha kwenye Spotify ni ya kweli, sahihi na kamilifu na unakubali kuidumisha hivyo nyakati zote. Ikiwa wewe ni mkazi wa mojawapo ya nchi zifuatazo, rejelea kwenye chati hii kwa vikwazo maalum vya umri katika nchi yako:

Ikiwa nchi yako imealamishwa kwa alama ya nyota (*) kwenye chati iliyo hapa chini, na unahitaji idhini ya mzazi au mlezi, mzazi au mlezi wako ataingia kwenye makubaliano kwa niaba yako.

Nchi au eneo Matakwa ya umri
Nchi na maeneo mengine yote ambayo Spotify inapatikana Lazima uwe na miaka 18 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Aljeria Lazima uwe na miaka 19 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Brazil, Burundi, Curaçao, Kroashia, Ujerumani, Liberia, Togo Lazima uwe na miaka 18 au zaidi, au uwe na miaka 16 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Albania, Armenia, Belarus, Bulgaria*, Kolombia*, Chile, Hungary, Kazakhstan, Kosovo, Moldova, Masedonia Kaskazini, Peru, Romania, Shirikisho la Urusi, Ukraine Lazima uwe na miaka 18 au zaidi, au uwe na miaka 14 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Eswatini, Montenegro, Serbia Lazima uwe na miaka 18 au zaidi, au uwe na miaka 15 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Kanada Lazima uwe na miaka 13 au zaidi ili utumie Huduma za Bila Malipo. Kwa Usajili wa Kulipia, lazima uwe na umri unaokubalika kisheria katika mkoa au himaya ya makazi yako, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Kupro*, Italia, Lithuania, Uholanzi Ili kutumia Huduma za Bila Malipo, lazima uwe na miaka 16 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi. Ili kujisajili kwa Usajili wa Kulipia, lazima uwe na miaka 18 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Cameroon, Misri, Guinea, Indonesia, Niger, Samoa, Suriname Lazima uwe na miaka 21 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Japani, Taiwani, Uthai Lazima uwe na miaka 20 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Jamhuri ya Korea Lazima uwe na miaka 19 au zaidi, au uwe na miaka 14 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Slovakia* Lazima uwe na miaka 16 au zaidi, au uwe na miaka 13 au zaidi na uwe na idhini ya mzazi au mlezi.
Tunisia Lazima uwe na miaka 18 au zaidi.

2 Mabadiliko kwenye Makubaliano

Mara mojamoja tunaweza kufanya mabadiliko kwenye Makubaliano kwa sababu halali, kama vile kuboresha vipengee vilivyopo au kuongeza kazi au vipengee mpya kwa Huduma, kutekeleza maendeleo ya sayansi na teknolojia, na mabadiliko mazuri ya kimitambo kwa Huduma, kuhakikisha uendeshaji au usalama wa Huduma, na kwa sababu za kisheria au za kudhibiti. Wakati tukifanya mabadiliko muhimu kwenye Makubaliano, tutakupa notisi ifaavyo chini ya hali, k.v., kwa kuonyesha notisi inayojulikana au kutafuta makubaliano yako ndani ya Huduma au kwa kukutumia baruapepe. Katika hali nyingine, tutakufahamisha mapema, na kuendelea kwako kutumia Huduma baada ya mabadiliko kutaonyesha ukubalifu wako kwa mabadiliko. Tafadhali hakikisha unasoma notisi kama hiyo kwa makini. Ikiwa hutaki kuendelea kutumia Huduma chini ya toleo jipya la Makubaliano, unaweza kukatiza akaunti yako kwa wasiliana nasi. Ikiwa ulipata Usajili wa Majaribio au wa Kulipiwa kupitia kwa mhusika wa tatu, ni lazima ughairi Usajili wa Kulipiwa Unaotumika kupitia mhusika wa tatu kama huyo.

3 Kufurahia Spotify

Hizi hapa baadhi ya taarifa kuhusu namna zote ambazo unaweza kufurahia Spotify.

3.1 Machaguo ya Huduma

Unaweza kupata maelezo ya machaguo ya Huduma yetu kwenye tovuti yetu na tutaeleza ni machaguo yapi ya Huduma yanapatikana kwako wakati unapofungua akaunti ya Spotify. Machaguo fulani yanatolewa kwako bila malipo. Huduma ya Spotify isiyohitaji malipo kwa sasa inajulikana kama "Huduma Bila Malipo." Machaguo mengine yanahitaji malipo kabla ya kuweza kuyafikia ("Usajili wa Kulipiwa"). Pia tunaweza kutoa mipango maalum ya mauzo, uanachama, au huduma, kwa kujumuisha ofa za bidhaa za mhusika wa tatu na huduma kwa kushirikiana na au kupitia Huduma ya Spotify. Hatuwajibikii bidhaa na huduma zinazotolewa na wahusika wa tatu kama hao. Tuna haki ya kuboresha, kukatiza au vinginevyo kurekebisha mipango ya usajili tunaoutoa na ofa za mauzo wkati wowote kwa kuwiana na Masharti haya.

Huduma Zisizo na Kikomo zinaweza kukosa kupatikana kwa watumiaji wote. Tutafafanua ni huduma gani zinazopatikana kwako wakati unapojisajili kwa huduma. Ikiwa unaghairi usajili wako kwenye Huduma Zisizo na Kikomo, au ikiwa usajili wako kwenye Huduma Zisizo na Kikomo unachachawizwa (kwa mfano, ikiwa unabadilisha maelezo yako ya malipo), unaweza kushindwa kujisajili tena kwenye Huduma Zisizo na Kikomo. Fahamu kwamba Huduma Zisizo na Kikomo zinaweza kukatizwa mbeleni, ambapo katika hiyo hali hutaweza kulipishwa kwa Huduma.

Ikiwa umenunua au kupokea msimbo, kadi ya zawadi, ofa ya kulipia mbeleni au ofa nyingine zinazotolewa au kuuzwa na au kwa niaba ya Spotify kwa ufikiaji kwenye Usajili wa Kulipiwa ("Msimbo"), sheria na masharti tofauti yaliyowasilishwa kwako pamoja na Msimbo pia yanawza kutumika kwa ufikiaji wako kwa Huduma na unakubali kuwiana na sheria na masharti kama hayo. Pia unaweza kununua ufikiaji kwenye Usajili wa Kulipiwa kupitia mhusika wa tatu. Katika hali kama hizo, sheria na masharti tofauti ya mhusika wa tatu kama huyo kwa kuongezea kwenye Makubaliano yanaweza kutumika kwenye ufikiaji wako kwa Huduma.

3.2 Majaribio

Mara kwa mara, sisi au wengine kwa niaba yetu wanaweza kutoa majaribio ya Usajili wa Kulipiwa kwa kipindi maalum bila kulipia au kwa kiwango kilichopunguzwa ("Jaribio"). Spotify inaweza kuamua ustahiki wako kwa Jaribio, na kuondoa au kuboresha Jaribio wakati wowote bila notisi ya kabla na bila wajibu, kwa kiwango kinachoruhusiwa kwa sheria inayotumika.

Kwa Majaribio mengine, tutakuhitaji kutoa maelezo yako ya malipo ili kuanza Jaribio. Kwa kutoa maelezo kama hayo unakubali kwamba tunaweza kuanza kukulipisha moja kwa moja kwa Usajili wa Kulipiwa siku ya kwanza inayofuata mwisho wa Jaribio kwa msingi wa kurudirudia kila mwezi au kipindi kingine ambacho tutaweka wazi kwako mbeleni. IIKIWA HUTAKI KULIPISHWA, NI LAZIMA UGHAIRI USAJILI WA KULIPIWA KABLA YA MWISHO WA JARIBIO KWA KUBOFY HAPA IKIWA ULIJISAJILI KWA JARIBIO KUPITIA SPOTIFY, AU IKIWA ULIPATA JARIBIO LAKO KUPITIA MHUSIKA WA TATU, NI LAZIMA UGHAIRI USAJILI WA KULIPIWA UNAOTUMIKA KUPITIA MHUSIKA WA TATU.

4 Malipo, kughairi, na kutuliza

4.1 Bili

Unaweza kununua Usajili wa Kulipiwa noja kwa moja kutoka Spotify au kupitia mhusika wa tatu kwa (1) kulipia ada ya usajili mbeleni kwa msingi wa kila mwezi au kwa kipindi kingine cha kurudiarudia kilichowekwa wazi kwako kabla ya ununuzi wako; au (2) malipo ya kabla yanayokupa ufikiaji kwa Huduma ya Spotify kwa kipindi cha muda maalum ("Kipindi cha Malipo ya Mapema").

Spotify inaweza kubadilisha bei ya Usajili wa Kulipiwa, kwa kujumuisha ada ya usajili wa kurudiarudia, Kipindi cha Malipo ya Kabla (kwa vipindi ambavyo havijalipiwa), au Misimbo, mara kwa mara na tutawasiliana kuhusu mabadiliko yoyote ya bei kwako mbeleni na, ikiwa inatumika, jinsi ya kukubali mabadiliko hayo. Mabadiliko ya bei yataanza kufanya kazi mwanzoni mwa kipindi cha usajili unaofuata tarehe ya mabadiliko ya bei. Kulingana na sheria inayotumika, unakubali bei mpya kwa kuendelea kutumia Huduma ya Spotify baada ya kuanza kutumika kwa mabadiliko ya bei. Ikiwa hukubaliani na mabadiliko ya bei, una haki ya kukataa mabadiliko kwa kuondoa usajili wako kwenye Usajili wa Kulipiwa kabla ya kuanza kutumika kwa mabadiliko ya bei.

Ukijisajili kwa Usajili wa Kulipiwa, unaweza kubadilisha mawazo yako kwa sababu yoyote au bila sababu na kupata kurudishiwa pesa kikamilifu zilizolipwa ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia siku ya kujisajili kwa huduma ifaayo ("Kipindi cha Kutuliza") kwa uwiano na yafuatayo:

  • Ukijisajili kwa Jaribio, unakubali kwamba Kipindi cha Kutuliza kwa Usajili wa Kulipiwa ambacho unapata Jaribio kitakwisha siku kumi na nne (14) baada ya kuanza Jaribio. Usipoghairi Usajili wa Kulipiwa kabla ya Jaribio kuisha, unapoteza haki yako ya kujiondoa na unaidhinisha Spotify kukulipisha moja kwa moja bei mliyokubaliana kila mwezi hadi utakapoghairi Usajili wa Kulipiwa.
  • Ukinunua Usajili wa Kulipiwa bila Jaribio, unaidhinisha Spotify kukulipisha moja kwa moja kila mwezi hadi utakapoghairi. Unakubali kwamba Kipindi cha Kutuliza kinapatikana siku kumi na nne (14) baada ya ununuzi wako lakini kinapotea mara unapotumia Huduma ya Spotify katika wakati huo.

4.2 Kufanya upya; Kughairi

Isipokuwa Usajili wako wa Kulipiwa umenunuliwa kwa Kipindi cha Kulipiwa Kabla, malipo yako kwa Spotify au mhusika wa tatu ambaye kupitia kwake ulinunua Usajili wa Kulipiwa utafanywa upya moja kwa moja mwishoni mwa kipindi cha usajili, isipokuwa unaghairi Usajili wako wa Kulipiwa kabla ya mwisho wa kipindi cha usajili wa sasa kw kubofya hapa ikiwa ulinunua Usajili wa Kulipiwa kupitia Spotify, au ikiwa ulinunua Usajili wa Kulipiwa kupitia mhusika wa tatu, kwa kughairi usajili wa Kulipiwa kupiti kwa mhusika wa tatu kama huyo. Kughairiwa kutaanza kufanya kazi siku moja baada ya siku ya mwisho ya kipindi ch usajili wa sasa, na utarudishwa nyuma kwa Huduma Bila Malipo. Ikiwa ulinunua Usajili wako wa Kulipiwa kupitia Spotify and na ukaghairi malipo au Usajili wa Kulipiwa na/au kukatiza Makubaliano yoyote (1) baada ya Kipindi cha Kutuliza kimeisha (mahali kinatumika), au (2) kabla ya mwisho wa kipindi cha usajili wa sasa, hatutarudisha pesa za usajili zilizokuwa zimelipwa tayari kwetu. Ikiwa ungependa kurejeshewa kikamilifu pesa zote zilizolipwa kwa Spotify kabla ya muda wa Kutuliza kuisha, ni lazima uwasiliane na Usaidizi kwa Wateja. Wakati tukichakata urejeshaji wowote, tutarejesha viwango kwa kutumia njia uliyoitumia wakati wa malipo.

Ikiwa umenunua Usajili wa Kulipiwa kwa kutumia Msimbo, usajili wako utakatizwa mara moja mwishoni mwa kipindi kilichotajwa kwenye Msimbo, au wakati kuna salio lisilotosha kulipia Huduma. Ikiwa umenunua Usajili wako wa Kulipiwa kupitia kwa mhusika wa tatu, ni lazima ughairi moja kwa moja kwa huyo mhusika wa tatu.

5 Kutumia huduma zetu

Huduma ya Spotify na Maudhui ni mali ya Spotify au watoaji leseni wa Spotify. Tunakupa idhini inayodhibitiwa, isiyo ya kipekee, na ya kurejeshwa ili kutumia Huduma ya Spotify, na idhini ya kudhibitiwa, isiyo ya kipekee, na ya kurejeshwa ili kutumia Maudhui ya binafsi yasiyo ya kibiashara (kwa pamoja, "Ufikiaji"). Ufikiaji huu utasalia kutumika hadi na isipokuwa kukatizwa nawe au Spotify. Unaahidi na kukubali kwamba unatumia Huduma ya Spotify na Maudhui kwa utumiaji wa binafsi, usio wa biashara na kwamba hutasambaza tena au kuhamisha Huduma ya Spotify au Maudhui.

Programu za Spotify na Maudhui haziuzwi au kuhamishwa kwako, na Spotify na wataoji wake wa leseni wanadumisha umiliki nakala zote za programu za Spotify na Maudhui hata baada ya usakinishaji kwenye tarakilishi yako, simu,tabuletu, vifaa vya kuvalia, spika, na/au vifaa vingine ("Vifaa").

Alama za biashara za Spotify, alama za huduma, majina ya biashara, logo, majina ya vikoa na vipengele vingine vyovyote vya chapa ya Spotify ("Vipengee vya Chapa ya Spotify") ni mali ya Spotify au watoaji wake wa leseni. Makubaliano hayakupi haki zozote za kutumia Vipengee vya Chapa ya Spotify iwe kwa utumiaji wa kibiashara au usio wa kibiashara.

Unakubali kufuata miongozo yetu ya Mtumiaji na kutotumia Huduma ya Spotify, Maudhui, au sehemu yoyote kwa njia yoyote isiyokubaliwa moja kwa moja na Makubaliano. Isipokuwa kwa haki zilizotolewa moja kwa moja kwako katika Makubaliano, Spotify haitoi haki zozote, mada, au mapendeleo kwako kwa Huduma ya Spotify au Maudhui.

Programu ya Mhusika wa Tatu (kwa mfano, maktaba za programu wazi) zilizojumuisha katika Huduma ya Spotify zinafanywa kupatikana kwako chini ya masharti ya leseni ya maktaba za programu jinsi ilivyochapishwa kwenye sehemu za msaada au mipangilio wa tarakilishi na mteja na/au tovuti yetu.

6 Programu na Vifaa vya Mhusika wa Tatu

Huduma ya Spotify ni ya kuingiliana au vinginevyo inaweza kuingiliana na programu za mhusika wa tatu, tovuti, na huduma ("Programu za Mhusika wa Tatu") na vifaa vya mhusika wa tatu ili kuwezesha Huduma ya Spotify kupatikana kwako. Programu hizi za Mhusika wa Tatu na Vifaa vinaweza kuwa na sheria na masharti ya utumiaji na sera za usiri na utumiaji wako wa programu hizi za Mhusika wa Tatu na Vifaa vitaongozwa kwa kuwiana na sheria na masharti kama hizo na sera za usiri. Unaelewa na kukubali kwamba Spotify haiungi mkono wala hawajibikii au kuwa na wajibu kwa tabia, vipengee, au maudhui ya Programu au Vifaa vya Mhusika yeyote wa Tatu au kwa biashara unayoweza kufanya na mtoaji wa Programu au Vifaa vya Mhusika wa Tatu yeyote, wala Spotify kuhakikisha kuingiliana kwa Programu na Vifaa vya Mhusika wa Tatu na Huduma.

7 Maudhui Yanayoundwa na Mtumiaji

Watumiaji wa Spotify wanaweza kuchapisha, kupakia, au vinginevyo kuchangia kwa Huduma (ambapo kunajumuisha, kwa mfano, picha, matini, ujumbe, taarifa, mada za muziki, maelezo, na mikusanyiko, na/au maudhui ya aina nyingine) ("Maudhui ya Mtumiaji"). Kwa kuondoa shaka, "Maudhui ya Mtumiaji" yanajumuisha maudhui yoyote kama hayo yaliyochapishwa katika Jumuia ya Msaada wa Spotify pamoja na sehemu nyingine yoyote ya Huduma ya Spotify.

Unaahidi kwamba, kuhusiana na Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayochapisha kwenye Spotify, (1) unamiliki au una haki ya kuchapisha Maudhui ya Mtumiaji kama hayo, na (2) Maudhui ya Mtumiaji kama hayo, au utumiaji wake katika Spotify jinsi ilivyojadiliwa katika Makubaliano, haukiuki Makubaliano au haki nyingine zozote zilizotajua katika miongozo ya Mtumiaji, sheria inayotumika, au mali ya kiakili, uwekaji wazi, utu, au haki nyingine za wengine au kuonyesha muunganisho wowote na au kuungwa mkono na wewe au Maudhui yako ya Mtumiaji na Spotify au msanii yeyote, bendi, lebo, kampuni au mtu binafsi bila idhini iliyoandikwa ya moja kwa moja kutoka Spotify au mtu binafsi kama huyo au kampuni.

Spotify inaweza, lakini haina jukumu la, kufuatilia, kupitia, au kuhakiki Maudhui ya Mtumiaji. Katika matukio yote, Spotify ina haki ya kuondoa au kulemaza ufikiaji kwa Maudhui yoyote ya Mtumiaji kwa sababu yoyote au bila sababu, kwa kujumuisha Maudhui ya Mtumiaji kwamba, kwa ubusara wa Spotify, yanakiuka Makubaliano. Spotify inaweza kuchukuwa hatua bila notisi ya kabla kwako au mhusika yeyote wa tatu. Uondoaji au kulemaza ufikiaji kwa Maudhui ya Mtumiaji itakuwa kwa ubusra wetu, na hatuahidi kuondoa wala kulemaza ufikiaji kwa Maudhui ya Mtumiaji maalum.

Unawajibikia binafsi Maudhui yote ya Mtumiaji unayochapisha. Spotify haiwajibikii Maudhui ya Mtumiaji wala haiungi mkono maoni yoyote yaliyo katika Maudhui yoyote ya Mtumiaji. UNAKUBALI KWAMBA IKIWA MTU YEYOTE ANAIBUA DAI DHIDI YA SPOTIFY KUHUSIANA NA MAUDHUI YA MTUMIAJI UNAYOCHAPISHA, BASI, KWA KIWANGO KINACHORUHUSIWA CHINI YA SHERIA YA NDANI, UTAIONDOLEA LAWAMA SPOTIFY NA KWAMBA HAINA UBAYA WOWOTE KUTOKA KWA NA DHIDI YA UHARIBIFU WOTE, HASARA, NA MATUMIZI YA AINA YOYOTE (KWA KUJUMUISHA ADA NA GHARAMA ZA MWANASHERIA) YANAYOIBUKA KUTOKANA NA DAI KAMA HILO.

8 Haki unazotupa

Kwa kuzingatia haki ulizopewa chini ya Makubaliano, unatupa haki ya (1) kuiruhusu Huduma ya Spotify kutumia kichakataji, mawimbi kasi, na maunzi ya uhifadhi kwenye Kifaa chako ili kuwezesha uendeshaji wa Huduma, (2) kutoa matangazo na taarifa nyingine kwako, na (3) kuwaruhusu wabia wetu wa kibiashara kufanya hivyo. Katika sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify, Maudhui unayofikia, kwa kujumuisha uchaguzi na uwekaji wake, yanaweza kuathiriwa na uzingatiaji wa kibiashara, kwa kujumuisha makubaliano ya Spotify na wahusika wa tatu. Maudhui mengine yaliyoruhusiwa na, kutolewa kwa, kuundwa na au vinginevyo kuwezeshwa kupatikana na Spotify (k.v. matangazo ya sauti) yanaweza kuwa na matangazo kama sehemu ya Maudhui. Huduma ya Spotify hufanya Maudhui kama hayo kupatikana kwako bila kuboreshwa.

Ikiwa unatoa maoni, mawazo, au mapendekezo kwa Spotify kuhusiana na Huduma ya Spotify au Maudhui ("Maoni"), unakubali kwamba Maoni si ya siri na unaiidhinisha Spotify kutumia Maoni hayo bila vikwazo na bila malipo kwako. Maoni yanazingatiwa kuwa aina ya Maudhui ya Mtumiaji.

Unaipa Spotify leseni isiyo ya wazi, ya kuhamishika, ya kutolewa leseni ndogo, bila malipo, ya kila mara (au, katika mamlaka ambayo hili haliruhusiwi, kwa muda sawa na wa kipindi cha Makubaliano ukiongeza miaka ishirini (20)), isiyopinduliwa, ya iliyolipiwa kikamilifu, na ya kilimwengu kutumia, kuchapisha upya, kuweka wazi kwa umma (k.v. kutekeleza au kuonyesha), kuchapisha, kutafsiri, kuboresha, kuunda kazi, na kusambaza Maudhui yako yoyote ya Mtumiaji kuhusiana na Huduma kupitia njia yoyote, iwe peke yako au kwa pamoja na Maudhui au nyenzo, kwa namna yoyote na kwa njia yoyote, namna au teknolojia, iwe inajulikana sasa au baada ya kuundwa. Kando na haki zilizotolewa hasa hapa, unasalia na umiliki wa haki zote, kwa kujumuisha haki za mali ya kiakili, katika Maudhui ya Mtumiaji. Mahali inatumika na chini ya sheria inayotumika, pia unakubali kuondoa na kutotekeleza "haki zozote za maadili" au haki kama hizo, kama vile haki yako ya kutambuliwa kama mwandishi wa Maudhui yoyote ya Mtumiaji, kwa kujumuish Maoni, na haki yako ya kukataa kutumiwa kwa Maufhui ya Mtumiaji kama hayo bila heshima.

9 Miongozo ya mtumiaji

Spotify inaheshimu haki za mali ya kiakili na inakutarajia kufanya vivyo hivyo. Tumeweka sheria chache za kudumu za kufuata wakati unapotumia Huduma, ili kuhakikisha Spotify inadumu kuwa ya kufurahisha kwa kila mtu. Ni lazima ufuate sheria hizi na kuwahimiza watumiaji wengine kufanya vivyo hivyo. Yafuatayo hayaruhusiwi kwa sababu yoyote ile:

  1. kunakili, kusambaza tena, kuchapisha tena, "kurarua," kurekodi, kuhamisha, kuwasilisha au kuonyesha umma, kutangaza, au kuweka wazi kwa umma sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify au Maudhui ambayo hayaruhusiwi moja kwa moja chini ya Makubaliano au sheria inayotumika au ambayo vinginevyo yanakiuka haki za mali ya kiakili (kama vile hatimiliki) katika Huduma ya Spotify au Maudhui au sehemu yoyote yake;
  2. kutumia Huduma ya Spotify kuhamisha au kunakili faili zozote za ndani ambazo huna haki ya kisheria ya kuhamisha au kunakili kwa njia hii;
  3. kuhamisha nakala za Maudhui yaliyohifadhiwa kutoka kwenye Kifaa ambacho hakijaidhinishwa kwa Kifaa kingine chochote kupitia njia yoyote;
  4. utenguaji wa maunzi, kutoa kwenye mkusanyiko, kutawanya, kuboresha au kuunda kazi inayotokana ya Huduma ya Spotify, Maudhui au sehemu nyingine yoyote isipokuwa kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria inayotumika. [Ikiwa sheria inayotumika inakuruhusu kutoa kwenye mkusanyiko sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify au Maudhui mahali inapohitajika ili kupata taarifa zinazofaa kuunda programu ya kujitegemea inayoweza kuendeshwa na Huduma ya Spotify au na programu nyingine, taarifa unazopata kutoka kwenye shughuli kama hizo (a) zinaweza kutumika pekee kuahirisha lengo, (b) zinaweza kutofunuliwa au kuwasilishwa bila idhini ya maandishi ya mbeleni ya Spotify kwa mhusika yeyote wa tatu ambaye si lazima afunue au kuwasilisha ili kuafikia lengo, na (c) haziwezi kutumika kuunda programu yoyote au huduma ambayo inafanaa sana katika utendaji wake na sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify au Maudhui];
  5. kukwepa teknolojia yoyote inayitumiwa na Spotify, watoaji wake wa leseni, au mhusika yeyote wa tatu ili kulinda Maudhui au Huduma;
  6. kuuza, kukodi, kutoa leseni ndogo, au kukodisha sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify au Maudhui;
  7. kukwepa vikwazo vya himaya yoyote vilivyowekwa na Spotify au watoaji wake wa leseni;
  8. kuongeza kikawaida idadi ya michezo, idadi ya ufuatiliaji, au vinginevyo kutumia vibaya Huduma kwa (i) kutumia bot yoyote, maandishi, au mchakato wowote wa kiotomatiki; (ii) kutoa au kukubali aina yoyote ya fidia (kifedha au vinginevyo), au (iii) namna nyingine yoyote;
  9. kuondoa au kubadilisha hatimiliki yoyote, alama ya biashara, au notisi nyingine za mali ya kiakili zilizo katika Maudhui au Huduma au zinazotolewa kupitia Huduma (kwa kujumuisha kwa madhumuni ya kujifanya au kubadilisha ishara zozote za umiliki au chanzo cha Maudhui yoyote);
  10. kukwepa au kuzuia matangazo kwenye Huduma ya Spotify, au kuunda au kusambaza vifaa vilivyoundwa kuzuia matangazo katika Huduma ya Spotify
  11. kutoa nywila zako kwa mtu mwingine yeyote au kutumia jina la mtumiaji la mtu mwingine na nywila;
  12. kulemaza Huduma ya Spotify au vinginevyo kutumia njia yoyote ya kiotomatiki (kwa kujumuisha roboti, chakavu, na buibui) ili kuona, kufikia, au kukusanya taarifa kutoka Spotify au Huduma ya Spotify;
  13. kuuza akaunti ya mtumiaji au orodha ya muziki, au vinginevyo kukubali au kujitolea kupokea fidia yoyote, ya kifedha au vinginevyo, ili kuathiri jina la akaunti au orodha ya muziki au maudhui yaliyojumuishwa kwenye akaunti au orodha ya muziki; au
  14. kuuza kibandia Maudhui kwa njia ya kiotomatiki au vinginevyo.

Tafadhali iheshimu Spotify, wamiliki wa Maudhui, na watumiaji wengine wa Huduma ya Spotify. Usishiriki kwenye shughuli yoyote, kuchapisha Maudhui yoyote ya Mtumiaji, au kujisajili na/au kutumia jina la mtumiaji, ambalo ni au linajumuisha nyenzo ambayo:

  1. ni ya kukera, ya matusi, kukosesha heshima, kiponografia, ya kutisha, au mbaya;

  2. si halali, au inanuia kuendeleza au kutekeleza kitendo haramu cha aina yoyote, kwa kujumuisha ukiukwaji wa haki za mali ya kiakili, haki za usiri, au haki za umiliki wa Spotify au mhusika wa tatu;

  3. inajumuisha nywila zako au kimakusudi inajumuisha nywila za mtumiaji mwingine au data ya binafsi ya wahusika wa tatu au kulenga kutafuta data ya binafsi kama hiyo;

  4. inajumuisha maudhui hasidi kama programu hasidi, Trojan horses, au virusi, au vinginevyo huhitilafiana na ufikiaji wa mtumiaji yeyote kwa Huduma;

  5. inalenga au inanyanyasa au kudhulumu watumiaji wengine;

  6. huiga au huwakilisha vibaya muungano wako na mtumiaji mwingine, mtu, au kampuni, au vinginevyo ya ulaghai, uwongo, udanganyifu, au upotoshaji;

  7. inajumuisha upitishaji wa barua ambazo hazijaombwa au aina nyingine za barua taka ("barua taka"), barua mbaya, barua za kufuatana, au kama hizo;

  8. inajumuisha shughuli za kibiashara au mauzo, kama vile matangazo, mashindano, bahati nasibu, au miradi ya piramidi, ambazo hazijaidhinishwa wazi na Spotify;

  9. viungo kwa, marejeleo, au vinginevyo kukuza bidhaa za biashara au huduma, isipokuwa kama ilivyoidhinishwa wazi na Spotify;

  10. huhitilafiana na au kwa njia yoyote huharibu Huduma ya Spotify, huharibu, hukiuka, au kujaribu kuchunguza, kutambaza, au kufanya jaribio kwa madhaifu ya katika Huduma au kwa mifumo ya tarakilishia ya Spotify, mtandao, sheria za matumizi, au sehemu yoyote ya usalama ya Spotify, hatua za uthibitishaji au hatua nyingine zozote za ulinzi zinazotumika kwa Huduma, Maudhui au sehemu yoyote yake; au

  11. migogoro na Makubaliano, kama ilivyoamuliwa na Spotify.

Unatambua na unakubali kuwa kuchapisha Maudhui ya Mtumiaji ambayo yanakiuka miongozo hii ya Mtumiaji (au kwamba Spotify inaamini kabisa kwamba inakiuka miongozo hii ya Mtumiaji) kunaweza kusababisha kukomeshwa mara moja au kusimamishwa kwa akaunti yako ya Spotify. Unakubali pia kwamba Spotify inaweza kurudisha jina lako la mtumiaji mahali ambapo ni busara kwetu kufanya hivyo, pamoja na ikiwa umekiuka Makubaliano.

Tafadhali fikiria jinsi unavyotumia Huduma ya Spotify na kile unachoshiriki. Huduma ya Spotify inajumuisha vipengee vya kiJumuia na maingiliano, kwa kujumuisha uwezo wa kuchapisha Maudhui ya Mtumiaji, kushiriki maudhui, na kufanya taarifa fulani kukuhusu hadharani. Kumbuka kuwa taarifa zinazoshirikiwa au zinazopatikana hadharani zinaweza kutumiwa na kushirikiwa tena na watumiaji wengine kwenye Spotify au kwenye wavuti, kwa hivyo tafadhali tumia Spotify kwa uangalifu na uzingatie mipangilio ya akaunti yako. Spotify haina jukumu la uchaguzi wako kuchapisha nyenzo kwenye Huduma.

Nywila zako zinalinda akaunti yako ya mtumiaji, na unawajibika peke yako kutunza siri na usalama wa nywila zako. Unaelewa kuwa unawajibika kwa matumizi yote (kwa kujumuisha matumizi yoyote yasiyoruhusiwa) ya jina lako la mtumiaji na nywila kwenye Huduma. Ikiwa jina lako la mtumiaji au nywila zako zimepotea au zimeibiwa, au ikiwa unaamini kumekuwa na ufikiaji bila ruhusa kwenye akaunti yako na mtu mwingine, lazima utuarifu mara moja na ubadilishe nywila zako haraka iwezekanavyo.

10 Ukiukaji na kuripoti Maudhui ya Mtumiaji

Spotify inaheshimu haki za wamiliki wa hakibunifu. Ikiwa unaamini kuwa Maudhui yoyote yanakiuka haki zako za hakimiliki au haki nyingine, angalia sera ya hakimiliki ya Spotify. Ikiwa Spotify imearifiwa na mmiliki wa hakimiliki, kwa kutumia fomu zilizotolewa na Spotify, kwamba Maudhui yoyote yanakiuka hakimiliki, Spotify inaweza kwa hiari yake kuondoa Maudhui kama hayo kutoka kwa Huduma, au kuchukua hatua nyingine ambazo Spotify inaona zinafaa, bila taarifa ya awali kwa mtumiaji au mtu mwingine ambaye alitoa au kuchapisha Maudhui. Ikiwa mtumiaji kama huyo au mtu mwingine anaamini kuwa Maudhui hayakiuki, anaweza katika hali fulani kuwasilisha arifa ya kukanusha kwa Spotify na ombi la kurudisha maudhui yaliyotolewa, ambayo Spotify inaweza kukubali au kutokubali, kwa hiari ya Spotify.

kiwa unaamini kuwa Maudhui yoyote hayatii miongozo ya Mtumiaji, tafadhali jaza yetu ya notisi.

11 Vikomo na maboresho kwa huduma

Spotify itafanya juhudi nzuri kuweka Huduma ya Spotify kufanya kazi. Hata hivyo, shida fulani za kiufundi, matengenezo au upimaji, au masasisho yanayohitajika kuonyesha mabadiliko katika sheria zifaazo na mahitaji ya kisheria, yanaweza, mara kwa mara, kusababisha usumbufu wa muda mfupi. Spotify ina haki, mara kwa mara na wakati wowote, kurekebisha au kukomesha, kwa muda mfupi au kwa kudumu, kazi na huduma za Huduma ya Spotify, kwa taarifa ya mapema inapowezekana, yote bila dhima kwako, isipokuwa pale inapokatazwa na sheria, kwa sababu halali kama vile kwa tukio la usumbufu wa kweli, urekebishaji, au kukomesha Huduma ya Spotify au kazi yoyote au huduma yake, au unahitaji kukarabati, kudumisha au kuboresha kazi zilizopo au huduma, au kuongeza kazi mpya au huduma kwenye Huduma, au kutekeleza maendeleo katika sayansi na teknolojia au kuhakikisha uendeshaji au usalama wa Huduma, sababu za kisheria na za udhibiti.

Pamoja na hayo yaliyotangulia, ikiwa una ada ya kulipia mapema kwa Spotify kwa Usajili wa Kulipiwa ambao Spotify hukatiza kabisa kabla ya kumalizika kwa Kipindi cha Kulipia Mapema (kilichoainishwa katika sehemu ya Malipo, kughairi, na sehemu ya kutuliza), Spotify itakurudishia ada ya malipo ya mapema ya Kipindi cha Kulipiwa kabla baada ya kukatizwa kama huko. Unaelewa, unakubaliana, na unakubali kwamba Spotify itafanya juhudi nzuri, ingawa haina jukumu la kudumisha, kusaidia, kuboresha, au kusasisha Huduma, au kutoa maudhui yote au maalum kupitia Huduma. Spotify na/au wamiliki wa Maudhui yoyote wanaweza, mara kwa mara, kuondoa Maudhui kama hayo bila taarifa. Sehemu hii itatekelezwa kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria inayotumika.

12 Akaunti za Chapa

Ikiwa utaanzisha akaunti ya Spotify kwa niaba ya kampuni, shirika, taasisi, au chapa ("Chapa", na akaunti kama hiyo "Akaunti ya Biashara"), maneno "wewe" na "yako," kama yanavyotumika katika Makubaliano yote, yanahusu wewe na Chapa. Ukifungua Akaunti ya Biashara, unawakilisha na unathibitisha kuwa umeidhinishwa kutoa ruhusa na leseni zote zinazotolewa katika Makubaliano na kuifunga Chapa hiyo kwenye Makubaliano.

Chapa inaweza kufuata watumiaji, kuunda, na kushiriki orodha za muziki, mradi Chapa haichukui hatua yoyote ambayo inamaanisha kuidhinisha au uhusiano wa kibiashara kati ya Chapa na mtumiaji anayefuatwa, msanii, mtunzi wa nyimbo, au mtu mwingine yeyote, isipokuwa kama Chapa kipekee imepata haki za kuashiria uthibitisho kama huo. Kwa kuongezea, Chapa lazima ziwe wazi kwa watumiaji wetu juu ya kufichua uungwaji mkono wowote au maanani yaliyotolewa kwa wasanii, watunzi wa nyimbo, watumiaji, au mtu mwingine yeyote na lazima izingatie sheria, masharti na kanuni zote zinazotumika wakati wa kushiriki shughuli zilizotajwa hapo juu.

13 Jumuia ya Usaidizi wa Spotify

Jumuia ya Usaidizi wa Spotify ni mahali pa majadiliano na kubadilishana taarifa, vidokezo, na vifaa vingine vinavyohusiana na Huduma ya Spotify. Kwa kutumia Jumuia ya Usaidizi ya Spotify unakubali Masharti ya Jumuia.

14 Usaidizi kwa Wateja

Kwa usaidizi wa wateja na maswali yanayohusiana na akaunti na malipo ("Maswali ya Usaidizi kwa Wateja"), tafadhali wasilisha tikiti kwa idara yetu ya Huduma ya Wateja ukitumia fomu ya mawasiliano Huduma ya Wateja kwenye sehemu ya Kutuhusu Sisi kwenye tovuti yetu. Tutatumia juhudi za kawaida kujibu Maswali yote ya Usaidizi kwa Wateja kwa wakati unaofaa lakini hatuahidi kwamba Maswali yoyote ya Msaada wa Wateja yatajibiwa kwa wakati wowote maalum na/au kwamba tutaweza kujibu maswali kama hayo.

Unaweza pia kuwasilisha malalamiko kwenye jukwaa mkondoni kwa suluhisho mbadala la mzozo (jukwaa la ODR). Unaweza kupata jukwaa la ODR kupitia kiungo kifuatacho: https://ec.europa.eu/consumers/odr.

15 Udhibiti wa uhamishaji

Bidhaa za Spotify zinaweza kuwa chini ya sheria na masharti ya Marekani. ya udhibiti wa uhamishaji au sheria kama hizo zinazotumika katika mamlaka nyingine, kwa kujumuisha Masharti ya Usimamizi wa Uhamishaji (Export Administration Regulations ("EAR")) yanayodumishwa na Marekani. Idara ya Biashara, biashara na vikwazo vya kiuchumi vinavyodumishwa na Ofisi ya Idara ya Hazina ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ("OFAC"), na Kanuni za Usafiri wa Kimataifa ("ITAR") zinazodumishwa na Idara ya Jimbo. Unathibitisha kuwa wewe (1) hauko katika nchi yoyote ambayo Marekani imezuia bidhaa au imetumia vikwazo vyovyote vya kiuchumi; na (2) sio mtu aliyekataliwa kama ilivyoainishwa katika sheria yoyote inayotumika ya kuuza nje au kuuza nje tena au kanuni au sheria zinazofanana zinazotumika katika mamlaka nyingine.

Unakubali kufuata sheria na kanuni zote zinazotumika za usafirishaji na usafirishaji tena wa bidhaa nje, pamoja na EAR, vikwazo vya kiuchumi vinavyosimamiwa na OFAC, na ITAR. Hasa, unakubali kwamba hautauza – moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja – kuuza nje, kusafirisha tena, kuhamisha, kugeuza, au vinginevyo kutupa bidhaa yoyote, programu, au teknolojia (pamoja na bidhaa zinazotokana na au kulingana na teknolojia hiyo) iliyopokelewa kutoka Spotify chini ya Makubaliano ya marudio yoyote, chombo, au mtu aliyekatazwa na sheria au kanuni zozote zinazofaa za Marekani au mamlaka nyingine yoyote bila kupata idhini ya mapema kutoka kwa mamlaka inayofaa ya serikali kama inavyotakiwa na sheria na kanuni hizo.

16 Masharti na ukomeshaji

Makubaliano hayo yataendelea kutumika kwako hadi itakapokomeshwa na wewe au Spotify. Hata hivyo, unatambua na unakubali kuwa leseni ya kudumu uliyotolewa na wewe kuhusiana na Maudhui ya Mtumiaji, kwa kujumuisha Maoni, haibadiliki na kwa hivyo itaendelea baada ya kumalizika au kukatizwa kwa Makubaliano yoyote kwa sababu yoyote. Spotify inaweza kukatiza Makubaliano au kusimamisha ufikiaji wako wa Huduma ya Spotify wakati wowote, pamoja na tukio la utumiaji usiohalalishwa wa ruhusa yako halisi au inayoshukiwa kwa Huduma ya Spotify na/au Maudhui, kutotii Makubaliano, au ikiwa tuaziondoa Huduma na/au Maudhui (katika hali hii tutakupa arifa inayofaa kabla ya kufanya hivyo). Ikiwa wewe au Spotify mnakatiza Makubaliano, au ikiwa Spotify itasitisha ufikiaji wako kwenye Huduma ya Spotify, unakubali kwamba Spotify haitakuwa na dhima au jukumu kwako, na Spotify haitarudisha pesa zozote ambazo umelipa tayari, kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa chini ya sheria inayotumika. Unaweza kukatiza Makubaliano wakati wowote. Ili kujifunza jinsi ya kukatiza akaunti yako ya Spotify, tafadhali wasiliana nasi kupitia fomu ya mawasiliano ya Huduma kwa Wateja ambayo inapatikana kwenye ukurasa wetu wa Kutuhusu Sisi. Sehemu hii itatekelezwa kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria inayotumika.

Sehemu 7, 8, 9, 11, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, na 24 hapa, pamoja na sehemu nyingine za Makubaliano ambayo, iwe wazi au kwa asili yao, lazima yabaki kutumika hata baada ya kukatiza Makubaliano, zitasalia bila kukomeshwa.

17 Kanusho la hakikisho

UNAELEWA NA KUKUBALI KWAMBA HUDUMA YA SPOTIFYA INATOLEWA "JINSI ILIVYO" NA "JINSI INAVYOPATIKANA," BILA UDHAMINI WA MOJA KWA MOJA AU UNAOKISIWA AU HALI YA AINA YOYOTE. SPOTIFY NA WAMILIKI WOTE WA MAUDHUI HAWANA UWAKILISHI NA WANAKATAA UDHAMINI WOWOTE AU HALI ZA UBORA UNAOTOSHELEZA, UUZAJI, UFAAFU KWA KUSUDI FULANI, AU KUTOKIUKA. SI SPOTIFY WALA MMILIKI YEYOTE WA MAUDHUI ANATOA UDHAMINI KWAMBA HUDUMA YA SPOTIFY HAINA PROGRAMU HASIDI AU VIFAA VINGINE HATARI. KWA KUONGEZEA, SPOTIFY HAIFANYI UWAKILISHI WALA HAITOI UDHAMINI, KUTHIBITISHA, KUHAKIKISHA, AU KUWAJIBIKIA PROGRAMU ZOZOTE ZA MHUSIKA WA TATU (AU MAUDHUI YALIYOMO), MAUDHUI YA MTUMIAJI, VIFAA AU BIDHAA NYINGINE YOYOTE AU HUDUMA INAYOTANGAZWA, INAYOUZWA AU KUTOLEWA NA MHUSIKA WA TATU KWENYE AU KUPITIA HUDUMA YA SPOTIFY AU TOVUTI YOYOTE ILIYOTOLEWA KIUNGO, AU ILIYOONYESHWA KWENYE BANGO LOLOTE AU UTANGAZAJI MWINGINE NA SPOTIFY HAIWAJIBIKI KWA BIASHARA YOYOTE KATI YAKO NA WATOAJI WA HUDUMA ZA MHUSIKA WA TATU INAYOENDELEA.

HAKUNA USHAURI WALA TAARIFA IWE YA MANENO AU KWA UANDISHI INAYOPATIKANA NA WEWE KUTOKA KWA SPOTIFY ITAUNDA UDHMINI WOWOTE KWA NIABA YA SPOTIFY. WAKATI UNATUMIA HUDUMA YA SPOTIFY, UNAWEZA KUPATA UFIKIAJI KWA VIPENGEE VYA KUJUJA MAUDHUI, LAKINI MATUMIZI YA VIPENGEE HIVI BADO YANAWEZA KUSABABISHA MAUDHUI YA KINA KUTOLEWA KWAKO NA USITEGEMEE VIPENGEE KAMA HIVYO KUJUJA MAUDHUI YOTE YA KINA.

BILA KUZUIA YANAYOENDELEA, HAKUNA CHOCHOTE KWENYE SEHEMU HII KITAKUWA NA ATHARI YA KUPUNGUZA UWAJIBIKAJI WA SPOTIFY KATIKA TUKIO LA KUTOTENDA KABISA AU KIDOGO AU UTENDAJI USIOTOSHA WA MAJUKUMU YAKE MUHIMU YA UTOAJI WA HUDUMA CHINI YA MAKUBALIANO. SEHEMU HII INATUMIKA KWA KIWANGO KIKUBWA ZAIDI KINACHORUHUSIWA NA SHERIA INAYOTUMIKA.

SEHEMU HII HAIATHIRI HAKI ZAKO ZA HALI KAMA MTUMIAJI.

18 Ukomo

UNAKUBALI KWAMBA UTATUZI WAKO WA PEKEE NA BINAFSI KWA MATATIZO YOYOTE AU KUTORIDHIKA NA HUDUMA YA SPOTIFY NI KUSAKINUA PROGRAMU YOYOTE YA SPOTIFY NA KUACHA KUTUMIA HUDUMA YA SPOTIFY. WEWE UNAKUBALI KUWA SPOTIFY HAINA WAJIBU AU UWAJIBIKAJI UNAOTOKANA NA AU KUHUSIANA NA PROGRAMU ZA MHUSIKA WA TATU AU MAUDHUI HAYO YALIYOPATIKANA KUPITIA AU KWA KUUNGANA NA HUDUMA YA SPOTIFY, NA WAKATI UHUSIANO WAKO NA PROGRAMU KAMA HIZO ZA MHUSIKA WA TATU UNAWEZA KUONGOZWA NA MAKUBALIANO TOFAUTI NA HAO WAHUSIKA WA TATU, UTATUZI WAKO WA PEKEE NA BINAFSI, KUHUSIANA NA SPOTIFY, KWA MATATIZO YOYOTE AU KUTORIDHIKA NA PROGRAMU ZA MHUSIKA WA TATU, AU MAUDHUI YALIYOMO, NI KUSAKINUA NA/AU KUACHA KUTUMIA PROGRAMU KAMA HIZO ZA MHUSIKA WA TATU.

HAKUNA TUKIO AMBALO SPOTIFY, MAAFISA WAKE, WENYE HISA, WAFANYAKAZI, MAWAKALA, WAKURUGENZI, KAMPUNI TANZU, MATAWI, WARITHI, WATENDAKAZI, WAGAVI, AU WATOAJI LESENI WATAWAJIBIKA KWA:

(1) HASARA YOYOTE AU UHARIBIFU (PAMOJA NA UHARIBIFU WOWOTE WA MOJA KWA MOJA, MAALUM, KWA AJILI YA TUKIO, KUADHIBU AU MFANO) AMBAO HAUWEZI KUTABIRIWA. HASARA AU UHARIBIFU UNAWEZA KUTABIRIWA IKIWA NI DHAHIRI KUWA UTATOKEA AU IKIWA, WAKATI AMBAO KANDARASI ILIFANYWA, WOTE SISI NA WEWE TULIJUA UNAWEZA KUTOKEA; (2) YOYOTE: (A) HASARA YA UTUMIAJI; (B) KUPOTEZA DATA; (C) HASARA YA BIASHARA; (D) KUPOTEZA FAIDA; AU

(E) UHARIBIFU KWA VIFAA, KWA KIWANGO AMBACHO UNGEWEZA KUEPUSHA UHARIBIFU KAMA HUO KWA KUFUATA USHAURI WETU WA KUTUMIA MASASISHO KWA HUDUMA AU MAUDHUI AU IKIWA UHARIBIFU KAMA HUO UNASABABISHWA NA WEWE KUSHINDWA KUFUATA MAAGIZO YA USAKINISHAJI AU KUWA NA MAHITAJI YA CHINI YA MFUMO YALIYOSHAURIWA NASI,

KATIKA VISA VYOTE VINAVYOJITOKEZA KUTOKANA NA MATUMIZI YA AU KUTOWEZA KUTUMIA HUDUMA YA SPOTIFY, VIFAA, PROGRAMU ZA MHUSIKA WA TATU, AU MAUDHUI YA PROGRAMU ZA MHUSIKA WA TATU, BILA KUJALI NADHARIA YA KISHERIA, BILA KUJALI IWAPO SPOTIFY ILIONYWA KUHUSU UWEZEKANO WA UHARIBIFU HUO, NA IKIWA SULUHU LINAKOSA KUFANYA KAZI YAKE MUHIMU;

(3) KUJUMUISHA UWAJIBIKAJI KWA MADAI YOTE YANAYOHUSIANA NA HUDUMA YA SPOTIFY, PROGRAMU ZA MHUSIKA WA TATU, AU MAUDHUI YA PROGRAMU ZA MHUSIKA WA TATU ZAIDI YA PESA ZILIZOLIPWA NA WEWE KWA SPOTIFY WAKATI WA MIEZI KUMI NA MBILI YA MBELE INAYOZUNGUMZIWA; AU

(4) KUTOTENDA KAZI AU UTENDAJI USIOTOSHELEZA AU KUCHELEWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YANAYOTOKANA NA MAKUBALIANO KULIKOSABABISHWA NA MAJEURE AU SABABU YOYOTE AMBAYO HAIWEZEKANI KUTABIRIWA AU KUZIDI UDHIBITI MZURI WA SPOTIFY.

Hakuna chochote katika Makubaliano hayo kinachoondoa au kuzuia wajibu wa Spotify kwa ulaghai, uwakilishi wa ulaghai, kifo, au jeraha la binafsi linalosababishwa na uzembe wake, na, ikiwa inahitajika kwa sheria inayotumika, uzembe mkubwa.

SEHEMU HII INATUMIKA KWA KIWANGO KIKUBWA ZAIDI KINACHORUHUSIWA NA SHERIA INAYOTUMIKA. HUENDA UKAWA NA HAKI CHINI YA SHERIA INAYOTUMIKA KATIKA MAMLAKA YAKO YA MAHAKAMA YANAYOTOA MASULUHISHO MBALI NA ZILE ZILIZOBAINISHWA HAPO JUU.

19 Haki za mhusika wa tatu

Unatambua na unakubali kuwa wamiliki wa Maudhui na wasambazaji fulani (kama vile watoaji wa duka la programu) ndio wanaokusudiwa kufaidika na Makubaliano na wana haki ya kutekeleza Makubaliano moja kwa moja dhidi yako. Kando na jinsi ilivyoainishwa katika sehemu hii, Makubaliano hayajakusudiwa kutoa haki kwa mtu yeyote isipokuwa wewe na Spotify, na kwa vyovyote vile Makubaliano huunda haki za mnufaika wa mhusika wa tatu. Kwa kuongezea, haki za kukomesha, kufuta, au kukubali mabadiliko yoyote, msamaha, au suluhu la Makubaliano haziko chini ya idhini ya mtu mwingine yeyote.

Ikiwa umepakua Programu kutoka kwa Duka la Proramu la Apple, Inc ("Apple") au ikiwa unatumia Programu kwenye kifaa cha iOS, unakubali kuwa umesoma, umeelewa, na unakubali ilani ifuatayo kuhusu Apple. Makubaliano haya ni kati yako na Spotify pekee, sio na Apple, na Apple haiwajibiki kwa Huduma na maudhui yaliyomo. Apple haina wajibu wowote wa kutoa huduma zozote za matengenezo na msaada kuhusiana na Huduma. Katika tukio la kushindwa kwokwote kwa Huduma kutii udhamini unaotumika, basi unaweza kuarifu Apple na Apple itarejesha bei yoyote inayotumika ya ununuzi wa Programu kwako; na, kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria inayotumika, Apple haina jukumu jingine la dhamana kuhusiana na Huduma. Apple haina jukumu la kushughulikia madai yoyote yako au ya mhusika yeyote wa tatu kuhusiana na Huduma au milki yako na/au utumiaji wa Huduma, pamoja na: (1) madai ya wajibu kwa bidhaa; (2) madai yoyote kwamba Huduma inashindwa kufuata matakwa yoyote ya kisheria au ya udhibiti; na (3) madai yanayotokana na ulinzi wa watumiaji au sheria kama hiyo. Apple haiwajibiki kwa uchunguzi, utetezi, uamuzi, na kutolewa kwa madai ya mhusika yeyote wa tatu kwamba Huduma na/au milki yako na utumiaji wa Programu zinakiuka haki za hakimiliki ya mhusika huyo wa tatu. Unakubali kufuata masharti yoyote yanayotumika ya mhusika wa tatu, unapotumia Huduma. Apple, na kampuni tanzu za Apple, ni walengwa wa tatu wa kufaidika kwa Makubaliano haya, na kwa kukubali kwako Makubaliano haya, Apple itakuwa na haki (na itachukuliwa kuwa imekubali haki) kutekeleza Makubaliano haya dhidi yako kama mnufaika wa mhusika wa tatu wa Makubaliano haya. Hivyo basi unawakilisha na unathibitisha kwamba (1) hauko katika nchi ambayo iko chini ya Marekani. Vizuizi vya serikali, au imeteuliwa na Marekani. Serikali kama nchi "inayounga mkono ugaidi"; na (2) hujaorodheshwa kwenye orodha. ya serikali ya Marekani au watu waliowekewa vikwazo.

20 Makubaliano Yote

Kando na jinsi ilivyoelezwa katika sehemu hii au kama ilivyokubaliwa wazi kwa maandishi kati yako na Spotify, Makubaliano hayo yanajumuisha sheria na masharti yote yaliyokubaliwa kati yako na Spotify na yanashinda makubaliano yoyote ya hapo awali kuhusiana na mada ya Makubaliano haya, iwe imeandikwa au kwa mdomo.

Tafadhali fahamu, hata hivyo, kwamba mambo kadhaa ya matumizi yako ya Huduma ya Spotify yanaweza kutawaliwa na makubaliano ya ziada. Hiyo inaweza kujumuisha, kwa mfano, ufikiaji wa Huduma ya Spotify kama matokeo ya kadi ya zawadi, Majaribio ya bure au yaliyopunguzwa, au pamoja na huduma nyingine. Unapopewa ofa ya mambo kama hayo ya matumizi yako, utapewa makubaliano yoyote ya ziada yanayohusiana, na unaweza kupata nafasi ya kukubali masharti ya ziada. Baadhi ya masharti hayo ya ziada yameorodheshwa kwenye tovuti ya Spotify. Kwa kiwango ambacho kuna mzozo wowote usioweza kurekebishwa kati ya masharti yoyote ya ziada na Masharti haya, masharti ya ziada yatashinda.

21 Kutenganishwa, ondoleo na ufasiri

Isipokuwa kama ilivyoelezewa katika Makubaliano, iwapo kifungu chochote cha Makubaliano kitachukuliwa kuwa batili au kisichoweza kutekelezeka kwa sababu yoyote au kwa kiwango chochote, ubatilifu kama huo au utekelezwaji hautaathiri kwa njia yoyote au kubatilisha vifungu vilivyobaki au visivyoweza kutekelezeka vya Makubaliano hayo, na matumizi ya kifungu hicho yatatekelezwa kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria.

Ukosefu wowote wa Spotify au mnufaika yeyote wa mhusika wa tatu wa kutekeleza Makubaliano au kifungu chochote hautaondoa haki ya Spotify au ya mnufaika wa mhusika wa tatu kufanya hivyo.

Kama inavyotumika katika Masharti haya, maneno "ni pamoja na" na "pamoja na," na tofauti zake, yatachukuliwa kufuatwa na maneno "bila kikomo."

22 Kazi

Spotify inaweza kupeana Makubaliano, na haki zake zozote chini ya Makubaliano, yote au sehemu, na Spotify inaweza kukabidhi majukumu yake yoyote chini ya Makubaliano. Huenda usitoe Makubaliano, yote au sehemu, au kuhamisha au kutoa leseni ndogo haki zako chini ya Makubaliano, kwa mhusika yeyote wa tatu.

23 Kuondolea lawama

Unakubali kuiondolea lawama na kuishikilia Spotify kutokuwa na madhara kutoka na dhidi ya uharibifu wote, hasara, na matumizi ya aina yoyote (pamoja na ada na gharama za wakili) zinazotokana na au zinazohusiana na: (1) ukiukaji wako wa Makubaliano au yoyote kati yao; (2) Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayochapisha au kuchangia vinginevyo; (3) shughuli yoyote unayoshiriki au kupitia Huduma ya Spotify; na (4) ukiukaji wako wa sheria yoyote au haki za mhusika wa tatu.

24 Uchaguzi wa sheria, usuluhishi wa lazima na mahali

24.1 Sheria Inayotawala / Mamlaka

Isipokuwa vinginevyo inavyotakiwa na sheria ya lazima ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya au mamlaka nyingine yoyote, Makubaliano (na mizozo yoyote / madai yoyote yasiyokuwa ya kandarasi yanayotokana au yanayohusiana nayo) yanatii sheria za serikali au nchi zilizoorodheshwa hapa chini, bila kuzingatia uchaguzi au migongano ya kanuni za sheria.

Zaidi ya hayo, wewe na Spotify mnakubali mamlaka ya korti zilizoorodheshwa hapa chini kusuluhisha mzozo wowote, madai, au ubishani unaotokea kuhusiana na Makubaliano (na mizozo / madai yoyote yasiyokuwa ya kandarasi yanayotokana na au kwa uhusiano wao). (Katika visa vingine, mamlaka hayo yatakuwa "ya kipekee", ikimaanisha kuwa hakuna korti za nchi nyingine zinazoweza kusimamia suala hilo; kuwa na mamlaka; katika kesi nyingine, mamlaka "sio ya kipekee", ikimaanisha kuwa mahakama za nchi nyingine zinaweza kuwa na mamlaka pia. Hii imeonyeshwa kwenye chati pia.)

Nchi au eneo Chaguo la Sheria Mamlaka ya Kisheria
Nchi na maeneo mengine yote ambayo Spotify inapatikana. Uswidi Maalum; Mahakama za Uswidi
Bulgaria, Kupro, Estonia, Ufaransa, Hong Kong, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Monako, Norwei, Ufilipino, Ureno, Slovakia, Hispania, Uturuki Sheria za Uswidi Si maalum; Mahakama za Uswidi
Brazil Sheria za Brazil Maalum; Mahakama za Jimbo na Serikali Kuu za São Paulo, Jimbo la São Paulo, Brazil
Kanada Haitumiki kwa wakazi wa Quebec: Sheria za Mkoa wa OntarioWakazi wa Quebec: Sheria za Mkoa wa Quebec, Kanada Hazitumiki kwa wakazi wa Quebec: Maalum mbali na kwa madhumuni ya kutekeleza hukumu; Mahakama za Ontario, KanadaWakazi wa Quebec: Mahakama za Quebec, Kanada
Ajentina, Bolivia, Chile, Kolombia, Kosta Rica, Jamhuri ya Dominika, Ekuador, El Salvador, Guatemala, Honduras, Nikaragua, Panama, Paraguay, Peru, Uruguay Jimbo la California, Marekani Maalum; Mahakama za Jimbo na Serikali Kuu za Kaunti ya San Francisco, CA au New York, NY
Uingereza Sheria za Uingereza na Wales Maalum

24.2 ONDOLEO LA KESI YA KUNDI

MAHALI INAPORUHUSIWA CHINI YA SHERIA INAYOTUMIKA, WEWE NA SPOTIFY MNAKUBALI KUWA KILA MTU ANAWEZA KULETA MADAI DHIDI YA MWINGINE PEKEE KWA UWEZO WAKO AU BINAFSI NA WALA SI KAMA MJUMBE WA WAFANYAKAZI AU WA DARASA KATIKA DARASA LOLOTE LINALOKISIWA AU SHUGHULI YA UWAKILISHI. Isipokuwa wewe na Spotify mnakubaliana, hakuna msuluhishi au jaji anayeweza kujumuisha zaidi ya madai ya mtu mmoja au vinginevyo kusimamia aina yoyote ya mwakilishi au masikizo ya darasa.

24.3 USULUHISHI

Ikiwa uko katika, unaishi katika, una ofisi katika, au unafanya biashara katika mamlaka ambayo Sehemu hii ya 24.3. inatekezeka, vifungu vifuatavyo vya usuluhishi wa lazima vinatumika kwako:

24.3.1 Utatuzi na usuluhishi wa migogoro

Wewe na Spotify mnakubali kuwa mzozo wowote, dai, au ubishani kati yako na Spotify unaotokana na au unaohusiana kwa njia yoyote na Makubaliano haya au kwa uhusiano wako na Spotify kama mtumiaji wa Huduma (iwe ni kwa kandarasi, mateso, sheria, ulaghai, uwakilishi mbaya, au nadharia nyingine yoyote ya kisheria, na ikiwa madai yanatokea wakati wa au baada ya kukatiza Makubaliano) utaamuliwa na usuluhishi wa lazima wa mtu binafsi. Usuluhishi sio rasmi kuliko kesi mahakamani. HAKUNA HAKIMU AU MWAMUZI KATIKA USULUHISHI, NA UPITIAJI WA MAHAKAMA WA TUZO YA USULUHISHI NI MDOGO. Kunaweza kuwa na ugunduzi mdogo zaidi kuliko kortini. Msuluhishi lazima afuate makubaliano haya na anaweza kutoa uharibifu sawa na unafuu kama mahakama (pamoja na ada ya wakili), isipokuwa kwamba msuluhishi hawezi kutoa unafuu wa tamko au amri ya kumnufaisha mtu yeyote isipokuwa wahusika kwenye usuluhishi. Kifungu hiki cha usuluhishi hakitakomeshwa kwa ukatizaji wa Makubaliano.

24.3.2 Mambo ya kipekee

Bila kujali kifungu cha 24.3.1 hapo juu, wewe na Spotify wote mnakubali kwamba hakuna kitu hapa kitachotupiliwa mbali, kuzuia, au vinginevyo kupunguza mipaka ya haki zetu, wakati wowote, ili (1) kuleta hatua ya mtu binafsi katika korti ndogo ya madai, ( 2) kufuata hatua za utekelezaji kupitia wakala wa shirikisho, serikali, au wakala husika wa ndani ambapo vitendo kama hivyo vinapatikana, (3) kutafuta afueni ya kisheria katika korti ya sheria, au (4) kufungua kesi katika korti ya sheria kushughulikia madai ya ukiukaji wa mali miliki.

24.3.3 Kanuni za usuluhishi

Wewe au sisi tunaweza kuanzisha kesi za usuluhishi. Usuluhishi wowote kati yako na Spotify hatimaye utasuluhishwa chini ya Kanuni za Usuluhishi za Jumba la Biashara la Kimataifa ("ICC") zinazofanya kazi wakati huo ("Sheria za ICC") na msuluhishi mmoja au zaidi walioteuliwa kwa mujibu wa Kanuni za ICC, kama ilivyobadilishwa na Makubaliano haya, na utasimamiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya ICC.

Usuluhishi wowote utafanywa kwa lugha ya Kiingereza na isipokuwa vinginevyo ikitakiwa na sheria ya lazima ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya au mamlaka nyingine yoyote, sheria ya kutumika katika usuluhishi wowote itakuwa sheria ya [jimbo husika au nchi iliyoorodheshwa katika kifungu cha 24.1], bila kuzingatia uchaguzi au migogoro ya kanuni za sheria.

24.3.4 Wakati wa kufungua kesi

Usuluhishi wowote lazima uanzishwe kwa kuweka mahitaji ya usuluhishi ndani ya MWAKA MMOJA (1) baada ya tarehe ambayo mtu anayeweka madai kwanza afahamu au kwa kweli inapaswa kufahamu juu ya kitendo hicho, upungufu, au kasoro inayosababisha madai; na hakutakuwa na haki kwa suluhisho lolote la madai yoyote ambayo hayadaiwi katika kipindi hicho cha wakati. Ikiwa sheria inayotumika inakataza kipindi cha mwaka mmoja kwa kuthibitisha madai, madai yoyote yanapaswa kuthibitishwa ndani ya muda mfupi zaidi unaoruhusiwa na sheria inayotumika.

24.3.5 Ilani; Mchakato

Mtu ambaye anakusudia kutafuta usuluhishi lazima kwanza atume ilani ya maandishi ya mzozo kwa mwingine, kwa barua iliyothibitishwa au Federal Express (sahihi inahitajika), au ikiwa hakuna anwani ya mahali kwenye faili, kwa barua ya kielektroniki ("Ilani"). Anwani ya Spotify ya Ilani ni: [Spotify, Attn: General Counsel, 4 World Trade Center, 150 Greenwich Street, 62nd Floor, New York, New York 10007, USA]. Ilani lazima (1) ieleze asili na msingi wa madai au mzozo; na (2) kuweka wazi unafuu maalum unaotafutwa ("Mahitaji"). Tunakubali kutumia juhudi nzuri za imani kutatua madai hayo moja kwa moja, lakini ikiwa hatufikii makubaliano ya kufanya hivyo ndani ya siku 30 baada ya Ilani kupokelewa, wewe au Spotify mnaweza kuanzisha hatua za usuluhishi. Wakati wa usuluhishi, kiasi cha ofa yoyote ya maamuzi iliyotolewa na wewe au Spotify haitafunuliwa kwa msuluhishi mpaka baada ya msuluhishi kutoa uamuzi wa mwisho na tuzo, ikiwa ipo. Endapo mzozo wetu hatimaye unasuluhishwa kwa njia ya usuluhishi kwa kukupendelea, Spotify itakulipa (1) kiwango kilichotolewa na msuluhishi, ikiwa kipo, (2) kiasi cha mwisho cha malipo kilichoandikwa kilichotolewa na Spotify katika kusuluhisha mzozo kabla ya tuzo ya msuluhishi; au (3) $ 1,000.00, yoyote iliyo kubwa. Nyaraka zote na taarifa zilizofunuliwa wakati wa usuluhishi zitahifadhiwa kwa siri na mpokeaji na hazitatumiwa na mpokeaji kwa madhumuni yoyote isipokuwa kwa madhumuni ya usuluhishi au utekelezaji wa uamuzi na tuzo ya msuluhishi na hazitafunuliwa isipokuwa kwa siri kwa watu ambao wana hitaji la kujua kwa madhumuni kama hayo au jinsi inavyotakiwa na sheria inayotumika. Isipokuwa inavyotakiwa kutekeleza uamuzi na tuzo ya msuluhishi, si wewe wala Spotify mtatoa tangazo la umma au maoni ya umma au kuanzisha utangazaji wowote kuhusu usuluhishi, pamoja na, lakini sio tu, ukweli kwamba watu wana mgogoro, uwepo wa usuluhishi, au uamuzi wowote au tuzo ya msuluhishi.

24.3.6 Marekebisho

Ikitokea kwamba Spotify inafanya mabadiliko yoyote ya usoni kwa kifungu hiki cha usuluhishi (isipokuwa mabadiliko ya anwani ya Spotify kwa ajili ya Ilani), unaweza kukataa mabadiliko yoyote kama hayo kwa kututumia ilani iliyoandikwa ndani ya siku 30 za mabadiliko kwa anwani ya Spotify ya Ilani, ambayo katika hali hiyo akaunti yako na Spotify itakatizwa mara moja na kifungu hiki cha usuluhishi, jinsi kinavyotumika mapema kabla ya marekebisho unayoyakataa, kitaendelea kutumika.

24.3.7 Utekelezaji

Ikiwa ondoleo la kesi ya kundi katika Sehemu ya 24.2 linapatikana kutoweza kutekelezeka katika usuluhishi au ikiwa sehemu yoyote ya Sehemu hii ya 24.3 itapatikana kuwa batili au haiwezi kutekelezeka, basi ukamilifu wa Sehemu hii ya 24.3 itakuwa batili na, kwa hali kama hiyo, watu wanakubaliana kuwa mamlaka ya kipekee na ukumbi ulioelezewa katika Sehemu ya 24.1 itasimamia hatua yoyote inayotokana na au inayohusiana na Makubaliano.

25 Wasiliana nasi

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Huduma ya Spotify au Makubaliano, tafadhali wasiliana na Huduma kwa Wateja ya Spotify kwa kutembelea sehemu ya Kutuhusu Sisi kwenye tovuti yetu.

Asante kwa kusoma Masharti yetu. Tunatumai utafurahia Spotify!

Shirika linalotoa kandarasi: Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501

© Spotify AB.

Spotify
Kampuni
Kuhusu
Kazi
For the Record
Jumuiya
Kwa Wasanii
Watengenezaji
Matangazo
Wawekezaji
Wauzaji
Viungo muhimu
Usaidizi
Kichezaji cha Wavuti
Programu ya Bure ya Vifaa vya Mkononi
Kenya (Swahili)
  • Sheria
  • Kituo cha Faragha
  • Sera ya Faragha
  • Cookies
  • Kuhusu Matangazo
© 2021 Spotify AB