Kuelewa Faragha katika Spotify
Katika Spotify, tunataka kukupa hali bora kabisa ya utumiaji inayowezekana. Ili kufanya hivi tunatumia baadhi ya data ya binafsi kukuhusu ili kutoa huduma ya Spotify inayokufaa na kutengeneza mfumo bora kabisa wa sauti kwa ajili ya wasikilizaji na watayarishi wetu. Tumejitolea pia kulinda faragha na usalama wa data yako. Angalia nyenzo za faragha hapa chini na utazame video kwenye ukurasa huu ili upate maelezo zaidi.
- Kituo chetu cha Faragha ni kitovu kilicho rahisi kutumia kinachofafanua vipengele muhimu vya Sera yetu ya Faragha - data tunayokusanya, jinsi tunavyoitumia na kuilinda na haki na udhibiti ulionao kuhusu data hii.
- Sera yetu kamili ya Faragha ina maelezo yote muhimu.
- Kurasa zetu za Usaidizi wa Spotify wa Faragha na Usalama hutoa usaidizi wa ziada na majibu kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
- Ikiwa bado unahitaji usaidizi, unaweza kuwasiliana nasi.
Spotify hukusanya data ipi ya binafsi kunihusu?
Ni muhimu sana kwetu uelewe data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu, jinsi tunavyoikusanya na ni kwa nini tunahitaji kuikusanya.
Tunakusanya data yako ya binafsi kwa njia zifuatazo:
- Unapojisajili kwenye Huduma ya Spotify au unaposasisha akaunti yako - tunakusanya data fulani ya binafsi ili kufungua akaunti yako ya Spotify ili uweze kutumia Huduma ya Spotify. Hii ni pamoja na jina la wasifu na anwani yako ya barua pepe, kama ilivyofafanuliwa kwa maelezo zaidi katika sehemu ya 3 ya Sera yetu ya Faragha.
- Kupitia matumizi yako ya Huduma ya Spotify - unapotumia au kufikia huduma ya Spotify, tunakusanya na kuchakata data ya binafsi kuhusu vitendo vyako. Hii ni pamoja na nyimbo ulizocheza na orodha za kucheza ulizotengeneza. Hii ni aina ya Data ya Matumizi iliyo katika sehemu ya 3 ya Sera yetu ya Faragha.
- Data ya binafsi unayoamua kutupa - mara kwa mara, unaweza pia kutupa data ya ziada ya binafsi au kutupa ruhusa ya kukusanya data ya binafsi k.m. ili kukupa utendaji au vipengele zaidi. Hii inaweza kujumuisha aina za Data ya Sauti, Data ya Ununuzi na Malipo na Data ya Utafiti na Tafiti zilizo katika sehemu ya 3 ya Sera yetu ya Faragha.
- Data binafsi tunayopokea kutoka kwa vyanzo vya wahusika wengine - ukijisajili kwenye Spotify kwa kutumia huduma nyingine au uunganishe akaunti yako ya Spotify kwenye programu, huduma au kifaa cha wengine, tutapokea data yako kutoka kwa washirika hao wengine. Huenda tukapokea pia data yako kutoka kwa watoa huduma za kiufundi, washirika wa malipo na utangazaji na washirika wa utangazaji. Angalia sehemu ya 3 ya Sera ya Faragha kwa maelezo zaidi.
Ni kwa nini Spotify inakusanya na kutumia data hii ya binafsi?
Tunakusanya na kutumia data yako ya binafsi kwa sababu zifuatazo:
- ili kutoa Huduma ya Spotify
- ili kutoa vipengele fulani vya ziada vya Huduma ya Spotify visivyo vya lazima
- ili kuelewa, kuchunguza, kutatua na kurekebisha hitilafu katika Huduma ya Spotify
- ili kutathimini na kutengeneza vipengele vipya, teknolojia na maboresho katika Huduma ya Spotify
- kwa madhumuni ya utangazaji, ukuzaji na matangazo
- ili kutii wajibu wa kisheria na maombi ya vyombo vya usalama
- ili kutimiza wajibu wa kimkataba na wahusika wengine
- ili kuchukua hatua zinazofaa kuhusu ripoti za ukiukaji wa hakimiliki na maudhui yasiyofaa
- ili kuanzisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria
- ili kuweka mipango ya biashara, kuripoti na kutabiri
- ili kuchakata malipo yako
- ili kutambua na kuzuia ulaghai, ikiwa ni pamoja na matumizi ya ulaghai ya Huduma ya Spotify
- ili kufanya utafiti na tafiti
Kwa maelezo zaidi kuhusu ni kwa nini Spotify hutumia data yako ya binafsi, na misingi yetu ya kisheria ya kufanya hivyo, angalia sehemu ya 4 ya Sera yetu ya Faragha.
Spotify inalindaje data yangu ya binafsi?
Tumejitolea kulinda data ya binafsi ya watumiaji wetu. Tumeweka hatua zinazofaa za kiufundi na mipango ili kulinda usalama wa data yako ya binafsi. Hata hivyo, tafadhali fahamu kuwa hamna mfumo ambao ni salama kabisa daima.
Tumetekeleza mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuficha utambuzi wa data, usimbaji fiche, idhini ya ufikiaji na sera za uhifadhi ili kulinda dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa na uhifadhi usiohitajika wa data ya binafsi kwenye mifumo yetu.
Ili kulinda akaunti yako ya mtumiaji, tunakuhimiza:
- tumia nenosiri thabiti ambalo unatumia tu kwenye akaunti yako ya Spotify
- usiwahi kushiriki nenosiri lako na mtu yeyote
- dhibiti ufikiaji wa kompyuta na kivinjari chako
- ondoka katika akaunti mara tu unapomaliza kutumia Huduma ya Spotify kwenye kifaa kinachoshirikiwa
- soma maelezo zaidi kuhusu kulinda akaunti yako
Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya 8 ya Sera yetu ya Faragha.
Spotify inashirikije / inahamishaje data yangu ya binafsi?
Kwa sababu ya hali ya kimataifa ya biashara yetu, Spotify hushiriki data ya binafsi kimataifa na kampuni za Spotify, wakandarasi wadogo na washirika wakati tunatekeleza shughuli zilizofafanuliwa katika Sera yetu ya Faragha. Wanaweza kuchakata data yako katika nchi ambako sheria zake za ulinzi wa data hazichukuliwi kuwa ni thabiti kama zilivyo sheria za Umoja wa Ulaya au sheria zinazotumika unakoishi. Kwa mfano, huenda wasikupe haki sawa kuhusu data yako.
Kila tunapohamisha data ya binafsi kimataifa, tunatumia zana:
- kuhakikisha uhamishaji wa data unatii sheria inayotumika
- kusaidia kuipa data yako kiwango sawa cha ulinzi kama ilivyo katika Umoja wa Ulaya
Angalia sehemu ya 7 ya Sera yetu ya Faragha kwa maelezo zaidi kuhusu ulinzi tunaotumia tunapohamisha data yako ya binafsi kimataifa.
Haki Zako za Data ya Binafsi
Inawezekana unafahamu kuwa sheria za faragha, ikiwa ni pamoja na Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data "GDPR", zinatoa haki fulani kwa watu binafsi juu ya data yao ya binafsi. Haki hizi zinafafanuliwa hapa chini.
Kwa maelezo ya kina zaidi, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kutumia haki zako, angalia sehemu ya 2 ya Sera yetu ya Faragha.
Kufikia data yako ya binafsi
Ni haki yako kuomba idhini ya kufikia data ya binafsi tunayochakata kukuhusu.
Pata taarifa
Ni haki yako kupata taarifa kuhusu data ya binafsi tunayoichakata kukuhusu na jinsi tunavyoichakata.
Sasisha data yako ya binafsi
Ni haki yako kuomba turekebishe au tusasishe data yako ya binafsi pale ambapo si sahihi au haijakamilika.
Dhibiti matumizi ya data yako ya binafsi
Ni haki yako kuomba tuache kuchakata kabisa au kwa muda baadhi ya data yako au yote ya binafsi.
Pinga matumizi ya data yako ya binafsi
Ni haki yako kupinga tusichakate data yako ya binafsi wakati wowote, kwa misingi inayohusiana na hali yako mahususi.
Pinga matangazo ya kulenga
Ni haki yako kupinga data yako ya binafsi isichakatwe kwa madhumuni ya kuwezesha matangazo ya kulenga.
Pinga maamuzi yanayofanywa kiotomatiki
Ni haki yako kutoathiriwa na maamuzi yanayofanywa kiotomatiki pekee, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji kulingana na vigezo fulani, ambapo maamuzi yatakuwa na athari ya kisheria kwako au yawe na athari nyingine kubwa kama hiyo.
Hamisha data yako ya binafsi
Ni haki yako kutuma ombi la kupewa nakala ya data yako ya binafsi katika muundo wa kielektroniki na haki ya kutuma data hiyo ya binafsi kwa matumizi katika huduma ya wahusika wengine.
Futa data yako ya binafsi
Ni haki yako kuomba tufute data yako ya binafsi.
Kuondoa idhini yako
Ni haki yako kuondoa idhini yako ya kuturuhusu kukusanya au kutumia data yako ya binafsi.
Ninaweza kwenda wapi ili nidhibiti data ya binafsi inayotumiwa na Spotify?
- Ukurasa wa Mipangilio ya Faragha - dhibiti uchakataji wa data fulani ya binafsi, ikiwa ni pamoja na Matangazo Yanayolenga.
- Ukurasa wa Mipangilio ya Arifa - weka mawasiliano ya mauzo unayopata kutoka Spotify.
- Mipangilio (inayopatikana kwenye matoleo ya Kompyuta na Vifaa vya mkononi ya Spotify) - dhibiti vipengele fulani vya Huduma ya Spotify kama vile "Maudhui Dhahiri" au "Ya Kijamii". Kwenye mipangilio ya "Kijamii", unaweza:
- kuanzisha kipindi cha Faragha
- kuchagua iwapo utashiriki unachosikiliza kwenye Spotify na wanaokufuatilia, na
- kuchagua iwapo utaonyesha wasanii uliocheza kazi zao hivi karibuni kwenye wasifu wako wa ummapendekezo
Kwenye mipangilio ya "Maudhui Dhahiri" unaweza kudhibiti iwapo maudhui yaliyokadiriwa kuwa ni dhahiri yanaweza kuchezwa kwenye akaunti yako ya Spotify.
Sera Zetu
Katika Spotify tumejitolea kukupa hali bora zaidi ya matumizi. Zifuatazo hapa chini ni sera tunazotumia tunapokupa huduma hii.