Sera ya Vidakuzi ya Spotify

Kuanza kufanya kazi tarehe 16/11/2021

1 Je, vidakuzi ni nini na teknolojia nyingine kama hizo?

2 Je, ni jinsi gani ambavyo Spotify inatumia vidakuzi?

3 Jinsi ya kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi

4 Masasisho ya Sera hii

5 Jinsi ya kuwasiliana nasi

Hujambo na karibu kwenye Sera ya Vidakuzi ya Spotify ("Sera").

Lengo la Sera hii ni kukupa wewe, kama mtumiaji wa huduma za Spotify, taarifa kamili na zinazofikiwa kuhusu vidakuzi ambavyo Spotify hutumia, jukumu ambalo vinatekeleza katika kutusaidia kutoa tukio bora iwezekanavyo kwako na machaguo uliyo nayo kuhusiana na mipangilio ya vidakuzi.

1. Je, vidakuzi ni nini na teknolojia nyingine kama hizo?

Vidakuzi ni faili za matini ambazo zinapakuliwa kwenye kifaa chako wakati unapotembelea tovuti. Ni muhimu kwa sababu huruhusu tovuti kutambua kifaa cha mtumiaji. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu vidakuzi kwenye: www.allaboutcookies.org au www.youronlinechoices.eu.

Neno kidakuzi hasa huelezea teknolojia nyingi, kwa kujumuisha:

  • vitambulisho vya pikseli (picha wazi za michoro zinazowekwa kwenye ukurasa wa tovuti au kwenye baruapepe, zinazoonyesha kwamba ukurasa au baruapepe imetazamwa),
  • vitambulisho vya kifaa cha mkononi na
  • hifadhi ya tovuti inayotumika na programu za tarakilishi au vifaa vya simu.

Tutatumia neno kidakuzi katika Sera hii kuelezea teknolojia hizi zote, lakini tutahakikisha kwamba tutakupa maelezo ya kutosha kuvihusu ili ufanye maamuzi mazuri kuhusu mipangilio yako ya vidakuzi.

Vidakuzi hufanya kazi mbalimbali, kama vile kukuwezesha kuvinjari kwenye kurasa kifanisi, kukumbuka mapendeleo yako, na kijumla kuboresha tukio lako la mtumiaji. Pia vinaweza kusaidia kuhakikisha kwamba matangazo unayoyaona mtandaoni ni ya kukufaa zaidi na ya mapendeleo yako.

Kuna kategoria chache tofauti za vidakuzi, kwa kujumuisha:

Vidakuzi vya Kipindi na vya Msisitizo

  • Vidakuzi vya Kipindi - hivi ni vidakuzi vinavyoisha kutumika mara unapofunga kivinjari chako cha tovuti; na
  • Vidakuzi vya Msisitizo - hivi ni vidakuzi vinavyodumu kwenye kifaa chako kwa muda fulani au hadi uvifute.

Vidakuzi vya Mhusika wa Kwanza na wa Tatu

  • Vidakuzi vya mhusika wa kwanza - hivi ni vidakuzi vinavyopangiliwa na tovuti unayotembelea wakati huo, nasi, au na mhusika wa tatu kwa ombi letu;;
  • Vidakuzi vya mhusika wa tatu - hivi ni vidakuzi vinavyopangiliwa na mtu kando na tovuti unayotembelea. Ikiwa unatembelea tovuti ya Spotify au unatumia Huduma ya Spotify Service na mtu mwingine anapangilia kidakuzi kupitia kwenye tovuti, hiki kitakuwa kidakuzi cha mhusika wa tatu.

Vidakuzi pia hutofautiana kulingana na lengo ambalo vinatumika, kwa kujumuisha:

Aina ya Kidakuzi Lengo
Vidakuzi Vinavyohitajika Kabisa Vidakuzi hivi ni muhimu ili kukuwezesha kutumia vipengee vya huduma zetu, kama vile kudumisha orodha ya muziki wako. Bila vidakuzi hivi, huduma unazoomba k.v., bili ya mtandaoni, haziwezi kutolewa.
Kwa muhtasari, vidakuzi hivi huwezesha huduma ambazo hasa umeomba na hufanya uwezekano wa kutumia huduma zetu.
Vidakuzi vya Utendaji Vidakuzi hivi hukusanya taarifa kuhusu jinsi wageni hutumia huduma zetu, kwa mfano ni kurasa gani wageni hutembelea sana, na ikiwa wanapata ujumbe wa makosa kutoka kwenye kurasa za tovuti. Vidakuzi hivi hukusanya taarifa za bila majina kwenye kurasa zinazotembelewa. Taarifa zote ambazo vidakuzi hivi hukusanya ni za jumla na hivyo bila majina. Hutumika tu kuboresha jinsi huduma zetu zinafanya kazi.
Uchambuzi wa tovuti unaotumia vidakuzi kukusanya data ili kuwezesha utendaji wa tovuti unapatikana katika kategoria hii. Kwa mfano, vinaweza kutumika kujaribu miundo na kuhakikisha mfanano mmoja na wa hisia moja unadumishwa kwa mtumiaji. Kategoria hii haijumuishi vidakuzi vinavyotumika kwa mitandao ya matangazo yanayolenga/ya tabia.
Vidakuzi vya Utandaji Kazi Vidakuzi hivi huwezesha tovuti kukumbuka maamuzi unayofanya (kama vile jina la mtumiaji, lugha au eneo ambalo upo) na hutoa vipengee vya binafsi vinavyofanya kazi vyema. Vidakuzi hivi pia vinaweza kutumika kukumbuka mabadiliko ambayo umefanya kwa ukuba wa matini, fonti na sehemu nyingine za kurasa za tovuti ambazo unaweza kupangilia. Taarifa ambazo vidakuzi hivi hukusanya zinaweza kutowekwa majina na haziwezi kufuatilia shughuli yako ya kuvinjari kwenye tovuti nyingine.
Vidakuzi hivi hukumbuka maamuzi unayofanya ili kuboresha tukio lako.
Ikiwa kidakuzi kimoja kinatumika kwa kulenga tena ni lazima vijumuishwe katika kategoria ya 'Vidakuzi vya kulenga/vya matangazo’ pia. Pia inaweza kujumuisha vidakuzi vinavyotumika kufanya kazi maalum, lakini mahali kazi hiyo inajumuisha vidakuzi vinavyotumika katika mitandao ya matangazo ya kulenga/ya tabia lazima vijumuishwe kwenye kategoria ya ‘Vidakuzi vya kulenga au vya maatangazo’ pia kama kategoria hii.
Vidakuzi vya kulenga au vya matangazo Vidakuzi hivi vinatumika kutoa matangazo yanayofaa kwako na kwa mapendeleo yako. Pia vinatumika kupunguza idadi ya muda unaoona tangazo pamoja na kusaidia kupima ufanisi wa kampeni za matangazo. awaida huwekwa na mitandao ya matangazo kwa idhini ya mmiliki wa tovuti. Hukumbuka kwamba umetembelea tovuti na taarifa hii inashirikiwa na mashirika mengine kama watangazaji. Mara nyingi vidakuzi vya kulenga au vya matangazo vitaunganishwa kwa utenda kazi wa tovuti inayotolewa na mashirika mengine.
Vidakuzi hivi hukusanya taarifa kuhusu tabia zako za kuvinjari ili kutengeneza matangazo mwafaka kwako na kwa mapendeleo yako.

2. Je, ni jinsi gani ambavyo Spotify hutumia vidakuzi?

Spotify, au watoaji huduma wanaofanya kazi kwa niaba yetu, hutumia aina ya vidakuzi vilivyotajwa kwenye Sehemu ya 1 hapo juu kwa njia zifuatazo:

Aina ya Kidakuzi Lengo
Vinavyohitajika Kabisa Vidakuzi hivi ni muhimu ili kutuwezesha kuiendesha Huduma ya Spotify jinsi ulivyoomba. Kwa mfano, hutufanya kukutambua wewe ni msajili wa aina gani na kisha kukupa huduma ipasavyo.
Utendakazi / Uchambuzi Tunatumia vidakuzi na teknolojia kama hizo kuchambua jinsi ambavyo Huduma ya Spotify hufikiwa, hutumiwa, au inafanya kazi. Tunatumia taarifa hii kudumisha, kuendesha, na kuendelea kuboresha Huduma ya Spotify. Pia tunaweza kupata taarifa kutoka kwenye majarida ya baruapepe au mawasiliano mengine tunayokutumia, kwa kujumuisha ikiwa uliyafungua au ulipitisha magazeti au ulibofya kwenye maudhui yake yoyote. Taarifa hii hutufahamish kuhusu ufanisi wa majarida yetu na hutusaidia kuhakikisha kwamba tunatoa taarifa unazofurahia.
Vinavyofanya kazi Vidakuzi hivi hutuwezesha kuendesha Huduma ya Spotify kulingana na mapendeleo yako. Kwa mfano, wakati unapoendelea kutumia kurejelea Huduma ya Spotify, tunaweza kukupa huduma zetu kulingana na taarifa unayotoa kwetu, kama vile kukumbuka jina lako la mtumiaji, jinsi ambavyo umepangilia huduma zetu kukufaa, na kukumbusha kuhusu maudhui uliyoyafurahia au uliyoyasikiza kwenye huduma hapo awali.
Matangazo ya Kulenga Tunavitumia vidakuzi hivi na teknolojia nyingine kama hizo kukupa matangazo yanayoweza kuwa mwafaka kwako na kwa mapendeleo yako, kwa kujumuisha matangazo ya kimapendeleo. Taarifa pia zinaweza kutumika kurekodi ni mara ngapi umepewa matangazo ya aina fulani na kuhakikisha hatuonyeshi matangazo yayo hayo kwako kwa kurudia, na vinginevyo kutusaidia kupima ufanisi wake.
Mhusika wa Tatu Tunaweza kuwaruhusu Wabia wetu wa Kibiashara kutumia vidakuzi au teknolojia nyingine kama hizo kwenye au nje ya Huduma ya Spotify Service kwa malengo yayo hayo yaliyotajwa hapo juu, kwa kujumuisha kukusanya taarifa kuhusu shughuli zako za mtandaoni kwa muda na kwenye tovuti tofauti, maombi, na/au vifaa.
Matangazo ya Spotify Tunafanya kazi pamoja na wachapishaji wa tovuti, waundaji wa maombi, mitandao ya matangazo, na watoaji wa huduma ili kutoa matangazo na maudhui mengine yanayoikuza Spotify kwenye tovuti na huduma nyingine. Vidakuzi na teknolojia nyingine kama hizo zinaweza kutumika kukupa matangazo yanayoweza kuwa mwafaka kwako na kwa mapendeleo yako kwenye tovuti nyingine, maombi, na vifaa, na kudhibiti matangazo unayopokea na kupima ufanisi wake.

3. Jinsi ya kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi

Vidakuzi vya Kivinjari

Unaweza kuondoa au kuboresha idhini yako kwa utumiaji wetu wa vidakuzi wakati wowote. Ikiwa hutaki tena kupokea vidakuzi unaweza kutumia mipangilio ya kivinjari cha tovuti kukubali, kukataa na kufuta vidakuzi. Tafadhali fanya hili, fuata maagizo yaliyotolewa na kivinjari chako (kawaida hupatikana chini ya mipangilio ya "Msaada", "Vifaa" au "Hariri").

Tafadhali fahamu kwamba ukipangilia kivinjari chako kukataa vidakuzi, hutaweza kutumia vipengee vyote vya tovuti ya Spotify. Ili kupata taarifa zaidi, unaweza kutembelea www.allaboutcookies.org.

Vitambuzi vya Simu

Kwenye kifaa chako cha simu, mfumo wako wa uendeshaji unaweza kukupa machaguo ya ziada ya kuondoa matangazo ya kimapendeleo au vinginevyo kupangilia tena vitambuzi vya simu yako. Kwa mfano, unaweza kutumia mpangilio wa "Zuia Ufuatiliaji wa Matangazo" (kwenye vifaa vya iOS) au mpangilio kwa "Ondoka kwenye Matangazo ya Kimapendeleo" (kwenye Android) unaokuwezesha kuzuia utumiaji wa taarifa kuhusu utumiaji wako wa programu kwa malengo ya kutoa matangazo yanayolenga mapendeleo yako.

Vidakuzi kwenye Programu ya Tarakilishi ya Spotify

Unaweza kuondoa idhini yako kwa utumiaji wetu wa vidakuzi kwenye programu ya tarakilishi ya Spotify wakati wowote. Ikiwa hutaki tena kupokea vidakuzi, vinjari hadi kwenye ukurasa wa Mipangilio ya Akaunti yako na uwashe kipengee cha Kuondoka kwenye Vidakuzi vya Tarakilishi. Wakati kipengee kimewashwa, kitazuia vidakuzi katika usakinishaji wa programu ya tarakilishi ya Spotify kwenye tarakilishi hiyo; ikiwa umesakinisha Spotify kwenye zaidi ya mashine moja, au ikiwa unasakinisha upya programu, basi utahitaji kuwasha kipengee katika kila usakinishaji. Utahitaji kuanzisha upya programu ili kipengee hiki kianze kufanya kazi.

Tafadhali fahamu kwamba ukipangilia programu yako ya tarakilishi kukataa vidakuzi, basi tukio lako la Spotify litaathirika.

Matangazo ya Kimapendeleo

Matangazo fulani ya kulenga ambayo sisi (au mtoaji huduma anayefanya kazi kwa niaba yetu) hukuonyesha kulingana na taarifa kuhusu shughuli zako za mtandani kwenye tovuti na vifaa vingine vinavyoendeshwa na wahusika wa tatu yanaweza kujumuisha ikoni ya "Machaguo ya Matangazo" au namna nyingine ya kuondoka katika kupokea matangazo ya kimapendeleo. Unaweza kubofya kwenye ikoni ya AdChoices au tembelea www.aboutads.info ili kupata taarifa zaidi kuhusu ukusanyaji na utumiaji wa taarifa kuhusu shughuli zako za mtandaoni kwa matangazo ya kimapendeleo au kujifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumiaji wa data kwa matangazo ya kimapendeleo na kampuni zinazoshiriki katika Digital Advertising Alliance (DAA).

  • Watumiaji wa Kanada pia wanaweza kutembelea www.youradchoices.ca.
  • Watumiaji wa Ulaya pia wanaweza kutembelea www.youronlinechoices.com ili kujifunza jinsi ya kuondoka kwenye data inayotumika kwa matangazo ya kimapendeleo na kampini zinazoshiriki katika European Interactive Digital Advertising Alliance (EDAA).
  • Zana ya Kuondoka ya Network Advertising Initiative's (NAI) kwenye www.networkadvertising.org/choices hukuwezesha kuondoka kwenye utumiaji wa taarifa kuhusu shughuli zako za mtandaoni kwa matangazo ya kimapendeleo katika kampuni za NAI.

Tafadhali fahamu kwamba ikiwa unaondoka kwa kutuia mbinu zilizo hapo juu, bado unaweza kupokea matangazo wakati unapotumia Huduma ya Spotify.

4. Masasisho ya Sera hii

Tunaweza kufanya mabadiliko kwenye Sera hii mara mojamoja.

Wakati tukifanya mabadiliko makuu kwa Sera hii, tutakupa notisi k.v., kuonyesha notisi ndani ya Huduma ya Spotify au kwa kukutumia baruapepe. Tunaweza kukutaarifu mapema.

Ikiwa unataka kufahamu mengi kuhusu Sera hii ya Vidakuzi na jinsi ambavyo Spotify hutumia data yako ya binafsi, tafadhali tembele Kituo cha Faragha ili kufahamu mengi.

5. Jinsi ya kuwasiliana nasi

Asante kwa kusoma Sera yetu ya Vidakuzi. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Vidakuzi, tafadhali wasiliana na Ofisa wetu wa Ulinzi wa Data kwa kutumia fomu ya 'Wasiliana Nasi' kwenye Kituo cha Faragha au kwa kututumia barua kupitia anwani ifuatayo:

Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501

© Spotify AB.