Sera ya Faragha ya Spotify

Itatumika kuanzia tarehe 8 Juni 2022

1 Kuhusu Sera hii

2 Vidhibiti na haki za data yako ya binafsi

3 Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu

4 Kusudi letu la kutumia data yako ya binafsi

5 Kushiriki data yako ya binafsi

6 Ubakizaji wa data

7 Kuhamishia nchi zingine

8 Kutunza usalama wa data yako ya binafsi

9 Watoto

10 Mabadiliko kwenye Sera hii

11 Jinsi ya kuwasiliana nasi

1. Kuhusu Sera hii

Sera hii inafafanua jinsi tunavyoshughulikia data yako ya binafsi katika Spotify AB.

Inatumika kwenye matumizi yako ya:

 • huduma zote za utiririshaji za Spotify kama mtumiaji. Kwa mfano, hii ni pamoja na:
  • matumizi yako ya Spotify kwenye kifaa chochote
  • uwekeaji mapendeleo hali yako ya utumiaji
  • miundombinu inayohitajika ili kutoa huduma zetu
  • kuunganisha akaunti yako ya Spotify na programu nyingine
  • machaguo yetu mbili ya kutiririsha bure au kwa malipo (kila moja inaitwa 'Chaguo la Huduma')
 • huduma nyingine za Spotify zinazojumuisha kiungo kinachoelekeza kwenye Sera hii ya Faragha. Hizi ni pamoja na tovuti za Spotify, Huduma kwa Wateja na Tovuti ya Jumuiya

Kuanzia sasa, tutaita huduma hizi kwa pamoja 'Huduma ya Spotify'.

Mara kwa mara, tunaweza kubuni au kutambulisha huduma za ziada. Zitazingatia pia Sera hii, isipokuwa tubainishe vinginevyo tunapozitambulisha.

Sera hii si...

 • Masharti ya Kutumia Spotify , ambayo ni hati tofauti. Masharti ya Kutumia yanabainisha mkataba wa kisheria kati yako na Spotify kwa matumizi ya Huduma ya Spotify. Yanabainisha pia kanuni za Spotify na haki zako za mtumiaji
 • kuhusu matumizi yako ya huduma nyingine za Spotify ambazo zina sera yake ya faragha. Huduma nyingine za Spotify ni pamoja na Anchor, Soundtrap, Megaphone na programu ya Spotify Live

Nyenzo na mipangilio mingine

Maelezo muhimu kuhusu data yako ya binafsi yanapatikana hapa katika Sera hii. Hata hivyo, tunependekeza upitie vidhibiti na nyenzo zetu nyingine za faragha.

 • Kituo cha Faragha: Kituo kinachofaa watumiaji kilicho na muhtasari wa mada muhimu
 • Mipangilio ya Faragha: Dhibiti uchakataji wa data fulani ya binafsi, ikiwa ni pamoja na Matangazo ya Kulenga.
 • Mipangilio ya Arifa: Chagua mawasiliano ya mauzo unayopokea kutoka Spotify.
 • Mipangilio (inayopatikana kwenye matoleo ya Kompyuta na Vifaa vya mkononi ya Spotify): Dhibiti vipengele fulani vya Huduma ya Spotify kama vile 'Maudhui Dhahiri' au 'Ya Kijamii'. Kwenye mipangilio ya 'Kijamii', unaweza:
  • kuanzisha kipindi cha Faragha
  • kuchagua iwapo utashiriki unachosikiliza kwenye Spotify na wanaokufuatilia
  • kuchagua iwapo utaonyesha wasanii uliocheza kazi zao hivi karibuni kwenye wasifu wako wa umma

Kwenye mipangilio ya 'Maudhui Dhahiri' unaweza kudhibiti iwapo maudhui yaliyokadiriwa kuwa ni dhahiri yanaweza kuchezwa kwenye akaunti yako ya Spotify.

 • Sera ya Vidakuzi: Maelezo kuhusu jinsi ya kutumia vidakuzi na jinsi ya kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi. Vidakuzi ni faili zinazohifadhiwa kwenye simu, tableti au kompyuta yako unapotembelea tovuti.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

2. Vidhibiti na haki za data yako ya binafsi

Sheria za faragha, ikiwa ni pamoja na Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data ('GDPR'), zinatoa haki kwa watu binafsi juu ya data yao ya binafsi.

Baadhi ya haki zinatumika Spotify inapotumia 'misingi fulani ya kisheria' kuchakata data yako. Tunafafanua kila misingi ya kisheria na wakati ambapo Spotify inatumia kila mojawapo, katika Sehemu ya 4 'Kusudi letu la kutumia data yako ya binafsi'.

Jedwali hapa chini linafafanua:

 • haki zako
 • hali zinapotumika (kama vile kigezo cha kisheria kinachohitajika)
 • jinsi ya kuzitumia

Ni haki yako... Vipi?
Pata taarifa Pata taarifa kuhusu data ya binafsi tunayoichakata kukuhusu na jinsi tunavyoichakata. Tunakupa taarifa:
 • kupitia Sera hii ya Faragha
 • kupitia maelezo unayopewa unapotumia Huduma ya Spotify
 • kwa kujibu maswali na maombi mahususi unapowasiliana nasi
Idhini ya kufikia Omba idhini ya kufikia data ya binafsi tunayochakata kukuhusu.
Ili uombe nakala ya data yako ya binafsi kutoka Spotify, unaweza:
 • kutembelea Mipangilio ya Faragha ya akaunti yako. Huko, unaweza kupakua kiotomatiki data yako nyingi ya binafsi na kufahamu jinsi ya kuomba data ya ziada, au
 • kuwasilia nasi ili upate taarifa kamili tuliyonayo kukuhusu mara moja, bila kutumia zana ya kupakua kiotomatiki kwanza

Unapopakua data yako utapokea taarifa kuhusu data yako ambayo Spotify inapaswa kukupa kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha GDPR. Ikiwa unahitaji maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoshughulikia data yako ya binafsi, unaweza kuwasiliana nasi.
Urekebishaji Tuma ombi ili turekebishe au tusasishe data yako ya binafsi pale ambapo si sahihi au haijakamilika. Unaweza kubadilisha Data yako ya Mtumiaji chini ya ‘Badilisha wasifu’ katika akaunti yako au kwa kuwasiliana nasi.
Kufuta Tuma ombi ili tufute baadhi ya data yako ya binafsi.
Kwa mfano, unaweza kutuomba tufute data yako ya binafsi:
 • ambayo hatuihitaji tena kwa ajili ya kusudi lililotufanya tuikusanye
 • tunayochakata kulingana na misingi ya sheria ya idhini, na uondoe idhini yako
 • unapopinga (angalia sehemu ya 'Pingamizi' hapa chini) na
  • unapotoa pingamizi la haki, au
  • unapopinga matangazo ya moja kwa moja

Kuna hali ambapo Spotify haiwezi kufuta data yako, kwa mfano wakati:
 • bado tunahitaji kuchakata data kwa ajili ya kusudi lililotufanya tuikusanye
 • hitaji la Spotify la kutumia data linapewa kipaumbele ikilinganishwa na hitaji lako la kuifuta. Kwa mfano, pale tunapohitaji data kwa ajili ya kulinda huduma zetu dhidi ya ulaghai
 • Spotify ina wajibu wa kisheria wa kuhifadhi data, au
 • Spotify inahitaji data ili kuanzisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria. Kwa mfano, ikiwa kuna tatizo ambalo halijatatuliwa linalohusiana na akaunti yako
Kuna njia kadhaa unazoweza kutumia kufuta data ya binafsi kutoka Spotify:
 • unaweza kuondoa maudhui ya sauti kwenye wasifu wako kwa kuteua maudhui husika na kuchagua kuyaondoa. Kwa mfano, unaweza kuondoa orodha za kucheza kwenye wasifu wako, au kuondoa wimbo kwenye orodha yako ya kucheza
 • ili uombe tufute data yako ya binafsi kwenye Spotify, fuata hatua zilizo kwenye ukurasa wetu wa usaidizi. Data hii ni pamoja na Data ya Mtumiaji, Data ya Matumizi na data nyingine iliyoorodheshwa katika Sehemu ya 3 ‘Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu
 • unaweza pia kuwasiliana nasi moja kwa moja ili uombe tufute data
Vikwazo Tuma ombi ili tuache kuchakata baadhi au data yako yote ya binafsi.
Unaweza kufanya hivi ikiwa:
 • data yako ya binafsi si sahihi
 • uchakataji wetu ni kinyume cha sheria
 • hatuhitaji maelezo yako kwa kusudi mahususi, au
 • unapinga uchakataji wetu na tunatathmini ombi lako la pingamizi. Angalia sehemu ya 'Pingamizi' hapa chini

Unaweza kuomba kuwa tusitishe uchakatakaji huu kwa muda au kabisa.
Unaweza kutekeleza haki yako ya kuweka vikwazo kwa kuwasiliana nasi.
Pingamizi Weka pingamizi ili tuache kuchakata data yako ya binafsi.
Unaweza kufanya hivi ikiwa:
 • Spotify inachakata data yako ya binafsi kwa misingi ya kisheria ya maslahi halali, au
 • Spotify inachakata data yako ya binafsi kwa matangazo ya moja kwa moja
Ili utekeleze haki yako ya kupinga:
 • unaweza kutumia vidhibiti kwenye Huduma ya Spotify ili kuzima au kurekebisha baadhi ya vipengele vinavyochakata data yako ya binafsi. Kwa mfano, unaweza kuzima ‘Matangazo Yanayolengwa’ katika Mipangilio yako ya Faragha
 • pale ambapo Spotify haitoi kidhibiti, wasiliana nasi ili upinge
Uhamishaji wa data Tuma ombi la kupewa nakala ya data yako ya binafsi katika muundo wa kielektroniki na haki ya kutuma data hiyo ya binafsi kwa matumizi katika huduma ya watoaji wengine.
Unaweza kutuomba tutume data yako wakati tunachakata data yako ya binafsi kwa misingi ya idhini ya kisheria au utendaji wa mkataba. Hata hivyo Spotify bado itajaribu kutii ombi lolote kwa kadri inavyowezekana.
Kwa maelezo kuhusu namna ya kutekeleza haki ya kuhamisha, tafadhali angalia 'Idhini ya kufikia' hapo juu.
Usiathiriwe na maamuzi yanayofanywa kiotomatiki Usiathiriwe na maamuzi yanayofanywa kiotomatiki pekee (maamuzi yasiyo na mchango wa mtu), ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji kulingana na vigezo fulani, ambapo maamuzi yatakuwa na athari ya kisheria kwako au yawe na athari nyingine kubwa kama hiyo. Spotify haitekelezi aina hii ya maamuzi ya kiotomatiki kwenye Huduma ya Spotify.
Kuondoa idhini Ondoa idhini yako inayoturuhusu kukusanya au kutumia data yako ya binafsi.
Unaweza kufanya hivi ikiwa Spotify inachakata data yako ya binafsi kwa idhini ya misingi ya kisheria.
Ili uondoe idhini yako, unaweza:
Haki ya kuwasilisha malalamiko Wasiliana na Mamlaka ya Ulinzi wa Faragha ya nchini Uswidi au mamlaka ya ulinzi wa data ya mahali ulipo kuhusu maswali au hoja zozote. Unaweza kupata maelezo kuhusu Mamlaka ya Uswidi hapa, au uende kwenye tovuti ya mamlaka ya ulinzi wa data ya mahali ulipo.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

3. Data ya binafsi tunatokusanya kukuhusu

Majedwali haya yanabainisha aina za data ya binafsi tunayokusanya na kutumia.

Inayokusanywa unapojisajili kwenye Huduma ya Spotify au unaposasisha akaunti yako
Aina Maelezo
Data ya Mtumiaji Data ya binafsi tunayohitaji ili kufungua akaunti yako ya Spotify na inayokuruhusu kutumia Huduma ya Spotify.
Aina ya data inayokusanywa na kutumiwa inategemea aina ya Chaguo la Huduma ulilonalo. Inategemea pia jinsi unavyofungua akaunti yako, nchi unakoishi na matumizi yako ya huduma za wengine kuingia katika akaunti. Hii inaweza kuwa ni pamoja na:

 • jina la wasifu
 • anwani ya barua pepe
 • nambari ya simu
 • tarehe ya kuzaliwa
 • jinsia
 • anwani ya mtaa (angalia maelezo zaidi hapa chini)
 • nchi

Tunapata baadhi ya data hii kutoka kwako k.m. kutoka kwenye fomu ya kujisajili au ukurasa wa akaunti.
Pia tunakusanya baadhi ya data hii kutoka kwenye kifaa chako k.m. nchi au eneo. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data hii, angalia 'Eneo lako la jumla (lisilo mahususi)' katika aina ya Data ya Matumizi.
Data ya Anwani ya Mtaa Tunaweza kuomba na kuchakata anwani yako ya mtaa kwa sababu zifuatazo:
 • ili kuhakikisha umetimiza masharti ya kupata Chaguo la Huduma
 • ili kutoa ilani zinazohitajika kisheria
 • ili kutoa machaguo ya usaidizi
 • kwa usimamizi wa bili na ushuru
 • ili kukufikishia bidhaa au zawadi halisi ambazo umeagiza

Katika baadhi ya matukio, tunaweza kutumia programu ya wengine ili kukusaidia kuthibitisha anwani yako, kama vile Ramani za Google.
Yanayokusanywa kupitia matumizi yako ya Huduma ya Spotify
Aina Maelezo
Data ya Matumizi
Data ya binafsi inayokusanywa na kuchakatwa kukuhusu unapofikia au kutumia Huduma ya Spotify.
Kuna aina chache za maelezo yanayojumuishwa katika hili, yaliyoorodheshwa katika sehemu zinazofuata.
Maelezo kuhusu matumizi yako ya Spotify
Mifano ni pamoja na:
 • maelezo kuhusu Chaguo lako la Huduma ya Spotify
 • vitendo vyako katika Huduma ya Spotify (ikiwa ni pamoja na tarehe na saa), kama vile:
  • hoja za utafutaji
  • historia ya utiririshaji
  • orodha za kucheza unazounda
  • maktaba yako
  • historia ya kuvinjari
  • mipangilio ya akaunti
  • mtagusano na watumiaji wengine wa Spotify
  • matumizi yako ya huduma, vifaa na programu za wengine yanayohusiana na Huduma ya Spotify
 • makisio (yaani, uelewa wetu) ya mambo yanayokuvutia na mapendeleo yako kulingana na matumizi yetu ya Huduma ya Spotify
 • maudhui unayotoa wakati unashiriki kwenye ofa za Spotify, kama vile mashindano au bahati nasibu
 • maudhui unayochapisha kwenye sehemu yoyote ya Huduma ya Spotify. Kwa mfano: picha, sauti, maandishi, vichwa, maelezo, mawasiliano na aina nyingine ya maudhui

Data yako ya kiufundi
Mifano ni pamoja na:
 • Maelezo ya URL
 • vitambulishi vya mtandaoni kama vile data ya vidakuzi na anwani za IP
 • maelezo kuhusu vifaa unavyotumia kama vile:
  • Vitambulisho vya vifaa
  • aina ya muunganisho wa mtandao (k.m. wifi, 4G, LTE, Bluetooth)
  • mtoa huduma
  • utendaji wa mtandao na kifaa
  • aina ya kivinjari
  • lugha
  • maelezo yanayowezesha udhibiti wa haki za dijitali
  • mfumo wa uendeshaji
  • Toleo la programu ya Spotify
 • maelezo yanayotuwezesha kugundua na kuunganisha kwenye programu na vifaa vya wahusika wengine. Mifano ya maelezo haya ni jina la kifaa, vitambulishi vya kifaa, chapa na toleo. Mifano ya programu na vifaa vya wengine ni:
  • vifaa kwenye mtandao wako wa wifi (kama vile spika) ambavyo vinaweza kuunganisha kwenye Huduma ya Spotify
  • vifaa vinavyopatikana kupitia mfumo wako wa uendeshaji unapounganisha kupitia Bluetooth, programu jalizi na usakinishaji
  • Programu za washirika wa Spotify ili kubaini iwapo programu imesakinishwa kwenye kifaa chako

Eneo lako la jumla (lisilo mahususi)
Eneo lako la jumla ni pamoja na nchi, eneo au jimbo. Tunaweza kupata maelezo haya kutoka kwenye data ya kiufundi (k.m. anwani yako ya IP, mipangilio ya lugha kwenye kifaa chako) au sarafu ya malipo.
Tunahitaji maelezo haya:
 • ili kukidhi mahitaji ya kijiografia katika makubaliano yetu na wamiliki wa maudhui kwenye Huduma ya Spotify
 • ili kukupa maudhui na matangazo yanayokufaa

Data ya kihisi cha kifaa chako
Data ya kihisi cha kifaa cha mkononi inayotokana na mwendo au mkao (k.m. kipima kasi au gurudumu tuzi) ikiwa inahitajika ili kutoa vipengele vya Huduma ya Spotify vinavyohitaji data hii.
Data ya ziada unayoamua kutupatia
Aina Maelezo
Data ya Sauti
Ikiwa vipengele vya sauti vinapatikana katika soko lako na eneo ambako umechagua kutumia kipengele cha sauti, tutakusanya na kuchakata data ya sauti. Data ya sauti inamaanisha rekodi za sauti za sauti yako na manukuu ya rekodi hizo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi vipengele tofauti vya sauti vinavyofanya kazi, na jinsi unavyoweza kuvidhibiti na kuvizima, angalia Sera yetu ya Udhibiti wa Sauti.
Data ya Malipo na Ununuzi Ukifanya ununuzi wowote kutoka Spotify au ujisajili ili ufanye jaribio, tutahitaji kuchakata data yako ya malipo. Hii inajumuisha ukinunua Chaguo la Huduma inayolipiwa.
Data mahususi ya binafsi inayokusanywa na kutumiwa itatofautiana kwa kutegemea njia ya kulipa. Itajumuisha maelezo kama vile:
 • jina
 • tarehe ya kuzaliwa
 • aina ya njia ya malipo (k.m. kadi ya mikopo au ya malipo)
 • ikiwa unatumia kadi ya malipo au ya mikopo, aina ya kadi, tarehe ya mwisho ya matumizi na tarakimu fulani za nambari ya kadi yakoKumbuka: Kwa usalama, huwa hatuhifadhi nambari yako kamili ya kadi
 • ZIP/msimbo wa posta
 • nambari ya simu ya mkononi
 • maelezo ya ununuzi na historia ya malipo yako
Data ya Tafiti na Utafiti Unaposhiriki katika utafiti wa mtumiaji au kujibu tafiti, tunakusanya na kutumia data ya binafsi unayotoa.
Vyanzo vingine ambako tunakusanya data yako
Aina ya wahusika wengine Maelezo
Washirika wa uthibitishaji Ukijisajili au kuingia katika akaunti ya Huduma ya Spotify ukitumia huduma nyingine, tutapokea maelezo yako kutoka kwa mhusika huyo ili kukusaidia kufungua akaunti katika huduma yetu.
Programu, huduma na vifaa vya wengine unavyounganisha kwenye akaunti yako ya Spotify Ukiunganisha akaunti yako ya Spotify kwenye programu, huduma au vifaa vya wengine, tunaweza kukusanya na kutumia taarifa fulani kutoka kwa mhusika huyo ili kuwezesha ujumuishaji.
Programu, huduma na vifaa hivi vya wengine vinaweza kuwa ni pamoja na:
 • mitandao ya kijamii
 • vifaa ikiwa ni pamoja na:
  • sauti (k.m. spika na vipokea sauti vya kichwani)
  • saa mahiri
  • televisheni
  • simu za mkononi na tableti
  • motokaa (k.m. magari
  • vifaa vya michezo ya video
 • huduma au mifumo kama vile programu za kuratibu kwa sauti
Tutaomba ruhusa yako kabla hatujakusanya taarifa yako kutoka kwa wahusika fulani.
Washirika wa huduma za kiufundi Tunafanya kazi na washirika wa huduma za kiufundi wanaotupa data fulani. Hii ni pamoja na kuweka anwani za IP kwenye data isiyo mahususi ya mahali (k.m. nchi au eneo, jiji, jimbo).
Hii huwezesha Spotify kutoa Huduma ya Spotify, maudhui na vipengele.
Washirika wa malipo na Wauzaji Ukichagua kulipa kupitia wahusika wengine (k.m. watoa huduma za simu) au kupitia ankara, huenda tukapata data kutoka kwa washirika wetu wa malipo.
Hii huturuhusu:
 • kukutumia ankara
 • kuchakata malipo yako
 • kukupa ulichonunua

Tukikuelekeza kwa muuzaji, tunapokea data kutoka kwa muuzaji huyo inayohusiana na ununuzi wako. Kwa mfano, tunaweza kukuelekeza kwenye duka la bidhaa za msanii katika mfumo wa mhusika mwingine au tovuti ya tiketi ya mhusika mwingine.
Kupokea data hii huturuhusu:
 • kukokotoa asilimia yoyote ya mauzo tunayodai
 • kuchambua ufanisi wa ushirikiano wetu na washirika hawa wa mauzo
 • kuelewa mambo yanayokuvutia
Washirika wa matangazo na masoko Kutoka kwa washirika fulani wa utangazaji au matangazo, tunapokea makisio (yaani uelewa wake) wa mambo yanayokuvutia na mapendeleo yako.
Hii hutuwezesha kutoa matangazo yanayofaa zaidi.

Ukipakua programu ya vifaa vya mkononi ya Spotify na ujaribu kutumia Spotify ukiwa hujaingia katika akaunti, tutakusanya taarifa chache kuhusu matumizi yako ya Huduma ya Spotify, ikiwa ni pamoja na Data ya Matumizi. Tunafanya hivi ili kuelewa jinsi unavyofikia na kutumia Huduma yetu. Tunafanya hivi pia ili kuhakikisha tunatoa hali inayokufaa ya matumizi, kwa mfano kulingana na nchi au eneo lako. Ukiamua kufungua akaunti ya Spotify ili ufurahie huduma yetu kikamilifu, basi tutaunganisha data hii na data ya akaunti yako ya Spotify.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

4. Kusudi letu la kutumia data yako ya binafsi

Jedwali lililo hapa chini linafafanua:

 • kusudi letu la kuchakata data yako ya binafsi
 • uhalali wetu wa kisheria (unaojulikana kama 'misingi ya kisheria') chini ya sheria ya ulinzi wa data, kwa kila kusudi
 • aina za data ya binafsi tunazotumia kwa kila kusudi. Angalia maelezo zaidi kuhusu aina hizi katika Sehemu ya 3 'Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu'

Haya ni maelezo ya jumla kuhusu kila 'misingi ya kisheria' ili kukusaidia uelewe jedwali:

 • Utekelezaji wa Mkataba: Wakati kuna umuhimu wa Spotify (au mhusika mwingine) kuchakata data yako ya binafsi ili:
  • kutii wajibu uliobainishwa katika mkataba nawe. Hii ni pamoja na wajibu wa Spotify chini ya Masharti ya Kutumia ili kukupa Huduma ya Spotify, au
  • kuthibitisha maelezo kabla mkataba mpya na wewe haujaanza kutekelezwa.
 • Maslahi Halali: Wakati Spotify au mhusika mwingine anahitaji kutumia data yako ya binafsi kwa njia fulani, ambayo ni muhimu na ina sababu mahususi ikizingatiwa hatari yoyote kwako na watumiaji wengine wa Spotify. Kwa mfano, kutumia Data ya Matumizi ili kuboresha Huduma ya Spotify kwa watumiaji wote. Wasiliana nasi ikiwa ungependa kuelewa sababu maalum.
 • Idhini: Spotify inapokuomba uonyeshe dhahiri kukubali kwako matumizi ya Spotify ya data yako ya binafsi kwa kusudi fulani.
 • Kutii Wajibu wa Kisheria: Wakati Spotify inapaswa kuchakata data yako ya binafsi ili kutii sheria.
Kusudi la kuchakata data yako Misingi ya kisheria inayoruhusu kusudi Aina za data ya binafsi zilizotumika kwa ajili ya kusudi
Ili kutoa Huduma ya Spotify (kama ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya 1 ‘Kuhusu Sera hii’.)
 • Utekelezaji wa Mkataba
 • Maslahi Halali
 • Idhini

 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili kuelewa, kuchunguza, kutatua na kurekebisha hitilafu katika Huduma ya Spotify.
 • Utekelezaji wa Mkataba

 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
Ili kutathimini na kutengeneza vipengele vipya, teknolojia na maboresho katika Huduma ya Spotify.
 • Maslahi Halali

 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
Kwa matangazo au utangazaji ambapo sheria inatutaka tupate idhini yako.
Kwa mfano, tunapotumia vidakuzi kuelewa mambo yanayokuvutia au sheria inahitaji tupate idhini kwa ajili ya utangazaji kupitia barua pepe.
 • Idhini
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Kwa makusudi mengine ya utangazaji, ukuzaji na matangazo ambapo sheria haihitaji idhini.
Kwa mfano, tunapotumia data yako ya binafsi kufanya matangazo yakufae kulingana na mambo yanayokuvutia.
 • Maslahi Halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Ili kutii wajibu wa kisheria ambao tunazingatia.
Hii inaweza kuwa:
 • wajibu chini ya sheria ya nchi/eneo ulipo
 • Sheria ya Uswidi (kwa sababu makao yetu makuu yapo Uswidi), au
 • Sheria ya Umoja wa Ulaya tunayoizingatia
 • Kutii wajibu wa kisheria

 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Ili kutii ombi la mamlaka ya sheria.
Hii itatumika wakati mamlaka husika ya kisheria inapowasiliana nasi. Hii ni pamoja na polisi, mahakama au magereza.
 • Kutii wajibu wa kisheria
 • Maslahi halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Ili kutimiza wajibu wa kimkataba na wahusika wengine. Kwa mfano, makubaliano yetu na wamiliki wa maudhui kwenye Huduma ya Spotify.

 • Maslahi halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili kuchukua hatua zinazofaa kuhusu ripoti za ukiukaji wa hakimiliki na maudhui yasiyofaa.
 • Maslahi halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili kuanzisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria.
 • Maslahi halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Ili kuweka mipango ya biashara, kuripoti na kutabiri.
 • Maslahi Halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili kuchakata malipo yako
 • Utekelezaji wa Mkataba


 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili kutambua na kuzuia ulaghai. Kwa mfano, malipo ya ulaghai na matumizi ya ulaghai ya Huduma ya Spotify.
 • Maslahi Halali
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili kufanya utafiti na tafiti.
 • Maslahi Halali


 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Tafiti na Utafiti

Katika maeneo ya mamlaka ambapo maslahi halali hayatambuliki kwa misingi ya kisheria, tunategemea kigezo cha kimkataba au idhini.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

5. Kushiriki data yako ya binafsi

Sehemu hii inafafanua aina za wapokeaji wa data ya binafsi inayokusanywa au kuzalishwa kutokana na matumizi yako ya Huduma ya Spotify.

Maelezo yanapokatikana kwa umma

Data ya binafsi ifuatayo daima itapatikana kwa umma kwenye Huduma ya Spotify:

 • jina lako la wasifu
 • picha yako ya wasifu
 • orodha zako za kucheza za umma
 • maudhui mengine unayochapisha kwenye Huduma ya Spotify, na vichwa, maelezo na picha zozote zinazohusiana
 • unayefuatilia kwenye Huduma ya Spotify
 • anayekufuatilia kwenye Huduma ya Spotify (unaweza kuwazuia wanaokufuatilia)

Wewe au mtumiaji mwingine mnaweza kushiriki maelezo fulani kwenye huduma za wahusika wengine, kama vile mitandao jamii au mifumo ya ujumbe. Hii ni pamoja na:

 • wasifu wako
 • maudhui yoyote unayochapisha kwenye Spotify na maelezo kuhusu maudhui hayo
 • orodha zako za kucheza za umma

Data hii inaposhirikiwa, huduma ya wengine inaweza kuhifadhi nakala ili kuwezesha vipengele vyake.

Data ya binafsi unayoamua kushiriki

Tutashiriki data ya binafsi ifuatayo na walioorodheshwa katika jedwali lililo hapa chini pekee:

 • tunapohitaji kushiriki data ya binafsi kwa ajili ya matumizi ya kipengele cha Huduma ya Spotify, au programu, huduma au kifaa cha wengine ambacho umechagua kutumia, au
 • ukitupa vinginevyo idhini ya kushiriki data ya binafsi. Kwa mfano, unaweza kufanya hivyo kwa kuchagua mipangilio inayofaa katika Huduma ya Spotify au kwa kutoa idhini yako
Aina za wapokeaji Aina za data unayoweza kuchagua kushiriki Sababu ya kushiriki
Programu, huduma na vifaa vya wengine unavyounganisha kwenye Akaunti yako ya Spotify
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi

Ili kuunganisha akaunti yako ya Spotify, ama kukuruhusu utumie Huduma ya Spotify kuunganisha na programu, huduma au vifaa vya wengine.
Mifano ya programu, huduma na vifaa vya wengine ni kama vile:
 • programu za mitandao ya kijamii
 • vifaa vya spika
 • televisheni
 • mifumo ya motokaa
 • programu za kuratibu kwa sauti

Unaweza kuona na kuondoa miunganisho mingi ya washirika wengine chini ya 'Programu' katika akaunti yako.
Jumuiya ya usaidizi
 • Data ya Mtumiaji
Ili uweze kutumia huduma ya Jumuiya ya Usaidizi ya Spotify.
Unapojisajili ili kufungua akaunti kwenye Jumuiya ya Usaidizi ya Spotify, tutakuomba uweke jina la wasifu. Jina hili litaonyeshwa hadharani kwa mtu yeyote anayetumia Jumuiya ya Usaidizi ya Spotify. Tutaonyesha pia maswali au maoni yoyote utakayochapisha.
Watumiaji wengine wa Spotify
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
Ili ushiriki maelezo kuhusu matumizi yako ya Huduma ya Spotify na watumiaji wengine wa Spotify. Hawa wanaweza kuwa ni pamoja na wanaokufuatilia kwenye Spotify.
Kwa mfano, chini ya mipangilio ya 'Kijamii' unaweza kuchagua kushiriki wasanii uliocheza kazi zao hivi karibuni na orodha zako za kucheza kwenye wasifu wako. Unaweza pia kuchagua kuunda au kujiunga kwenye orodha ya kucheza inayoshirikiwa na watumiaji wengine. Orodha za kucheza zilizoshirikiwa hukupa mapendekezo ya kijamii kulingana na shughuli yako ya kusikiliza.
Wasanii na kampuni za kurekodi
 • Data ya Mtumiaji
Ili upokee habari au ofa za matangazo kutoka kwa wasanii, kampuni za kurekodi au washirika wengine.
Unaweza kuchagua kushiriki Data yako ya Mtumiaji kwa kusudi hili. Utaweza kuchagua kubadilisha mawazo yako na kuondoa idhini yako wakati wowote.

Maelezo tunayoweza kushiriki

Angalia jedwali hili la maelezo kuhusu tunayeshiriki naye na kwa nini.

Aina za wapokeaji Aina za data Sababu ya kushiriki
Watoa huduma
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Ili waweze kutoa huduma zao kwa Spotify.
Watoa huduma hawa ni pamoja na wale tunaowakodisha ili:
 • watoe usaidizi kwa wateja
 • waendeshe miundombinu ya kiufundi tunayohitaji ili kutoa Huduma ya Spotify
 • kusaidia katika kulinda mifumo na huduma zetu (k.m. reCAPTCHA ya Google)
 • kusaidia kutangaza bidhaa, huduma, matukio na ofa za Spotify (na washirika wetu)
Washirika wa malipo
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Malipo na Ununuzi
Ili waweze kuchakata malipo yako, kwa kusudi la kuepuka ulaghai.
Washirika wa matangazo
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
Ili waweze kutusaidia kukuonyesha matangazo yanayofaa zaidi kwenye Huduma ya Spotify na kusaidia kupima ufanisi wa matangazo.
Kwa mfano, washirika wetu wa matangazo hutusaidia kufanikisha matangazo yanayolengwa.
Matangazo yanayolengwa ni nini?
 • Hii hali ni wakati tunatumia maelezo ya wengine ili kufanya matangazo yakufae zaidi. Hali hii inajulikana pia kama utangazaji unaolingana na mambo yanayokuvutia.
 • Mfano wa tangazo linalolengwa ni pale ambapo mshirika wa tangazo anapokuwa na maelezo yanayoonyesha kuwa unapenda magari. Maelezo haya yanaweza kutusaidia kukuonyesha matangazo kuhusu magari.

Jinsi ya kudhibiti matangazo yanayolengwa:
 • Unaweza kudhibiti matangazo yanayolengwa katika Mipangilio ya Faragha ya akaunti chini ya ‘Matangazo Yanayolengwa’.
 • Unaweza pia kudhibiti matangazo yanayolengwa kwa baadhi ya podikasti ukitumia kiungo kilicho katika maelezo ya kipindi cha onyesho. Hii inatumika pale ambapo mtoa maudhui anafadhili podkasti yake kwa kuweka matangazo yanayolengwa au matangazo yanayotegemea maudhui katika podikasti yenyewe. Vidhibiti hivi husimamiwa na mpangishaji wa podikasti, ambaye huenda asiwe Spotify.

'Ukiondolewa' ili usipate Matangazo Yanayokulenga katika Mipangilio ya Faragha, bado huenda ukapata matangazo katika huduma zinazofadhiliwa kwa matangazo (k.m. podikasti au Chaguo la Huduma Bila Malipo). Utangazaji kama huo unatokana na maelezo yako ya usajili na maudhui unayotiririsha kwa sasa kwenye huduma zetu. Kwa mfano, ikiwa unasikiliza podikasti ya mapishi, unaweza kusikia tangazo kuhusu kichakataji chakula.
Washirika wa Matangazo
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
Ili kutangaza Spotify na washirika wetu. Huwa tunashiriki baadhi ya Data ya Mtumiaji na Data ya Matumizi na washirika hawa panapohitajika ili:
 • kukuwezesha ushiriki katika ofa za Spotify, ikiwa ni pamoja na majaribio au ofa nyingine zilizounganishwa
 • ili kutangaza Spotify katika maudhui na matangazo yanayochapishwa kwenye huduma nyingine za mtandaoni
 • kutusaidia sisi na washirika wetu kupima ufanisi wa ofa za Spotify

Mifano ya washirika ni pamoja na:
 • washiriki wa masoko au udhamini
 • tovuti na programu za vifaa vya mkononi zinazotuuzia nafasi ya kutangaza kwenye huduma zao
 • washirika wa kifaa, programu na vifaa vya mkononi wanaotoa pia ofa za Spotify

Washirika wetu wanaweza pia kuunganisha data ya binafsi tunayoshiriki nao na data nyingine wanayokusanya kukuhusu, k.m. matumizi yako ya huduma zao. Sisi na washirika wetu tunaweza kutumia maelezo haya kukupa ofa, matangazo au shughuli nyingine za utangazaji ambazo tunaamini zitakufaa.
Mifumo ya Kupangisha
 • Data ya Matumizi
Mifumo ya kupangisha hupangisha podikasti ili ziweze kukufikia. Tunashiriki data fulani, kama vile anwani yako ya IP, na mifumo ya kupangisha unapocheza podikasti. Spotify inamiliki mifumo miwili ya kupangisha, Megaphone na Anchor. Tunakuruhusu pia kutiririsha podikasti zinazopatikana kwenye mifumo mingine ya kupangisha isiyomilikiwa na Spotify.

Watoa huduma za podikasti wanapaswa kufafanua katika onyesho au kipindi mfumo upi unapangisha podikasti. Tafadhali angalia sera ya faragha ya mfumo wa kupangisha ili uone jinsi wanavyotumia data inayoshirikiwa nao.
Kushiriki na washirika wengine
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Ili kutusaidia kuelewa na kuboresha utendaji wa ushirikiano na huduma zetu.
Unaweza kuona na kuondoa miunganisho mingi ya washirika chini ya 'Programu' katika akaunti yako.
Watafiti wa kitaaluma
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
Kwa shughuli kama vile uchambuzi wa takwimu na masomo ya kitaaluma, lakini katika muundo wa utambulisho bandia pekee. Data iliyoficha utambuzi ni pale ambapo data inatambulishwa kwa msimbo badala ya jina lako au maelezo mengine yoyote yanayokutambulisha moja kwa moja.
Kampuni za Kupima za Spotify
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
Tunashiriki data na kampuni zifuatazo za Spotify ili kupima ufanisi wa kampeni za matangazo tunayoonyesha kwenye Huduma ya Spotify:
 • In Defense of Growth Incorporated d/b/a Podsights
 • Chartable Holding, Inc.
Kampuni nyingine za kikundi cha Spotify
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
 • Data ya Tafiti na Utafiti

Ili kutekeleza shughuli zetu za kila siku za biashara na ili tuweze kudumisha na kukupa Huduma ya Spotify.
Mamlaka za kisheria na mamlaka zingine
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Matumizi
Wakati tunaamini kwa nia njema kuwa ni muhimu kwetu kufanya hivyo, kwa mfano:
 • ili kutii wajibu wa kisheria
 • ili kushughulikia mchakato halali wa kisheria (kama vile kibali cha utafutaji, amri ya mahakama au wito wa mahakama)
 • kwa maslahi halali ya wahusika wengine au yetu wenyewe, yanayohusiana na:
  • usalama wa taifa
  • utekelezaji wa sheria
  • kesi (kesi mahakamani)
  • uchunguzi wa kosa la jinai
  • kulinda usalama wa mtu
  • kuzuia kifo au hatari iliyopo ya kujidhuru
Wanunuzi wa biashara yetu
 • Data ya Mtumiaji
 • Data ya Anwani ya Mtaa
 • Data ya Matumizi
 • Data ya Sauti
 • Data ya Malipo na Ununuzi
 • Data ya Tafiti na Utafiti
Iwapo tungeuza au tungejadiliana kuuza biashara yetu kwa mnunuzi au mnunuzi mtarajiwa.
Katika hali hii, tunaweza kuhamishia data yako ya binafsi kwa mrithi au mshirika kama sehemu ya mchakato huo.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

6. Ubakizaji wa data

Tunahifadhi data yako ya binafsi kadri tunavyoihitaji ili kukupa Huduma ya Spotify na kwa makusudi halali ya Spotify na michakato muhimu ya biashara, kama vile:

 • kudumisha utendaji wa Huduma ya Spotify
 • kufanya maamuzi ya biashara yanayotokana na data kuhusu ofa na vipengele vipya
 • kutii wajibu wetu wa kisheria
 • kutatua migogoro

Vigezo vinavyotumika kubainisha vipindi vya uhifadhi ni pamoja na:

 • Tunaweza kupunguzaje kipindi cha kuhifadhi data? Mifumo yetu imeundwa ili kuondoa data ya binafsi baada ya siku 90, isipokuwa kipindi kingine kikichaguliwa kwa sababu halali za kibiashara.
 • Je, tunahitaji kuhifadhi data ili kuhakikisha tunatoa huduma ambayo wateja wanatarajia? Tunahifadhi data ya binafsi kwa kipindi kinachofaa ili kutoa huduma zinazowafaa watumiaji wetu. Kwa kawaida huwa tunahifadhi historia ya kutiririsha kwa kipindi chote cha akaunti, kwa mfano, ili kutoa orodha za kucheza zinazofanana na zile ambazo watumiaji walifurahia awali zinazowafurahisha watumiaji (k.m. Kumbusho Lako la Likizo na kampeni ya Muhtasari ya mwisho wa mwaka) na mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo kulingana na mazoea ya sasa ya usikilizaji.
 • Je, watumiaji wanaweza kusasisha au kufuta data inayowahusu? Pale ambapo watumiaji wanaweza kuona na kusasisha data ya binafsi inayowahusu, tunahifadhi data hiyo kwa kadri mtumiaji anavyochagua kuihifadhi. Kwa mfano, tunahifadhi anwani yako ya barua pepe ya Spotify na maelezo mengine ya wasifu hadi utakapochagua kuyabadilisha au kuyafuta wewe mwenyewe.
 • Je, tunahitaji kuhifadhi data ili kudumisha sheria zetu na kutunza usalama wa huduma yetu? Ili kusaidia kuhakikisha usalama wa mtumiaji, kulinda dhidi ya maudhui hatari kwenye mfumo wetu na kushugulikia ripoti za ukiukaji wa hakimiliki, tunaweza kuhifadhi data iliyoondolewa kwenye Huduma ya Spotify kwa kipindi kifupi. Hii hutusaidia kuchunguza ukiukaji unaoshukiwa wa Mwongozo wetu wa Watumiaji na Sheria za Mfumo.
 • Je, Spotify ina wajibu wa kisheria au kimkataba kuhifadhi au kufuta data? Mifano ni pamoja na sheria za lazima za kuhifadhi data, amri za serikali za kuhifadhi data inayohusiana na uchunguzi au data inayohifadhiwa kwa kusudi la madai mahakamani. Kinyume cha hapo, tutaondoa maudhui yasiyo halali kisheria ikiwa sheria itatuhitaji tufanye hivyo.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

7. Kuhamishia nchi zingine

Kwa sababu ya hali ya kimataifa ya biashara yetu, Spotify hushiriki data ya binafsi kimataifa na kampuni za Spotify, wakandarasi wadogo na washirika ili kukupa Huduma ya Spotify. Wanaweza kuchakata data yako katika nchi ambako sheria zake za ulinzi wa data hazichukuliwi kuwa ni thabiti kama zilivyo sheria za Umoja wa Ulaya au sheria zinazotumika unakoishi. Kwa mfano, huenda wasikupe haki sawa kuhusu data yako.

Kila tunapohamisha data ya binafsi kimataifa, tunatumia zana:

 • kuhakikisha uhamishaji wa data unatii sheria inayotumika
 • kusaidia kuipa data yako kiwango sawa cha ulinzi kama ilivyo katika Umoja wa Ulaya

Ili kuhakikisha kila utumaji wa data unatii sheria zinazotumika katika Umoja wa Ulaya, tunatumia mbinu za kisheria zifuatazo:

 • Vifungu vya Kawaida vya Mikataba ('SCCs'). Vifungu hivi vinahitaji mhusika mwingine alinde data yako na akupe ulinzi na haki za kiwango cha Umoja wa Ulaya. Kwa mfano, tunatumia SCC kuhamisha data ya binafsi iliyofafanuliwa katika Sehemu ya 3 'Data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu' kwenda kwa watoa huduma wetu wa kupangisha wanaotumia seva zao zilizo Marekani. Unaweza kutekeleza haki zako chini ya Vifungu vya Kawaida vya Mikataba kwa kuwasiliana nasi au mhusika mwingine anayechakata data yako ya binafsi.
 • Maamuzi ya Kutosheleza. Hii inamaanisha kuwa tunatuma data ya binafsi katika nchi zilizo nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya ambazo zina sheria zinazojitosheleza za kulinda data ya binafsi, kama inavyofafanuliwa na Tume ya Ulaya. Kwa mfano, tunatuma data ya binafsi iliyofafanuliwa katika Sehemu ya 3 'Data ya binafsi tunayokusanya ' kwa washirika walio nchini Uingereza, Kanada, Japani, Jamhuri ya Korea na Uswisi.

Tunatambua pia na kutumia ulinzi wa ziada kama unavyohitajika kwa kila uhamishaji wa data. Kwa mfano, tunatumia:

 • ulinzi wa kiufundi, kama vile usimbaji fiche na utambulisho bandia
 • sera au michakato ya kupinga maombi ya mamlaka ya serikali yasiyo na uwiano au yaliyo kinyume cha sheria

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

8. Kutunza usalama wa data yako ya binafsi

Tumejitolea kulinda data ya binafsi ya watumiaji wetu. Tumeweka hatua zinazofaa za kiufundi na mipango ili kulinda usalama wa data yako ya binafsi. Hata hivyo, fahamu kuwa hamna mfumo ambao ni salama kabisa daima.

Tumetekeleza mbinu mbalimbali za kulinda dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa na uhifadhi usiohitajika wa data ya binafsi kwenye mifumo yetu. Hizi ni pamoja na utambulisho bandia, usimbaji fiche, ufikiaji na sera za utunzaji.

Ili kulinda akaunti yako ya mtumiaji, tunakuhimiza:

 • tumia nenosiri thabiti ambalo unatumia tu kwenye akaunti yako ya Spotify
 • usiwahi kushiriki nenosiri lako na mtu yeyote
 • dhibiti ufikiaji wa komyuta na kivinjari chako
 • ondoka katika akaunti mara tu unapomaliza kutumia Huduma ya Spotify kwenye kifaa kinachoshirikiwa
 • soma maelezo zaidi kuhusu kulinda akaunti yako

Unaweza kuondoka katika akaunti ya Spotify kwenye maeneo mengi kwa wakati mmoja kwa kutumia kipengele cha 'Ondoka katika akaunti kila mahali' kwenye ukurasa wa akaunti yako.

Ikiwa watu wengine wana idhini ya kufikia akaunti yako ya Spotify (kwa mfano iwapo umewapa ruhusa ya kutumia akaunti yako kwenye kifaa kinachoshirikiwa), basi wanaweza kufikia data yako ya binafsi, vidhibiti na Huduma ya Spotify inayopatikana kwenye akaunti yako.

Ni wajibu wako kuwapa ruhusa watu ambao huna wasiwasi kushiriki nao data hii ya binafsi ili wafikie akaunti yako. Matumizi ya akaunti yako ya Spotify na mtu mwingine yeyote kunaweza kuathiri mapendekezo yako ya binafsi na kujumuishwa katika data yako unayopakua.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

9. Watoto

Kumbuka: Sera hii haitumiki kwenye Spotify ya Watoto isipokuwa Sera ya Faragha ya Spotify ya Watoto iseme hivyo. Spotify ya Watoto ni programu tofauti ya Spotify.

Huduma ya Spotify ina kiwango cha chini cha 'Kikomo cha Umri' katika kila nchi au eneo. Huduma ya Spotify hailengi watoto ambao umri wao:

 • ni chini ya umri wa miaka 13, au
 • unafanya kuwa haramu kuchakata data yao ya binafsi, au
 • unahitaji idhini ya mzazi ili kuchakata data yao ya binafsi

Hatukusanyi au kutumia kwa makusudi data ya binafsi kutoka kwa watoto walio chini ya Kikomo cha Umri kinachoruhusiwa. Ikiwa uko chini ya Kikomo cha Umri, tafadhali usitumie Huduma ya Spotify, na usitupe data yoyote ya binafsi. Badala yake, tunapendekeza utumie akaunti ya Spotify ya Watoto.

Ikiwa wewe ni mzazi wa mtoto aliye na umri wa chini ya Kikomo cha Umri na umegundua mtoto wako ametoa data ya binafsi kwa Spotify, tafadhali wasiliana nasi.

Tukigundua kuwa tumekusanya data ya binafsi ya mtoto aliye na umri wa chini ya Kikomo cha Umri, tutachukua hatua zinazofaa kufuta data hiyo ya binafsi. Hatua hii inaweza kutuhitaji kufuta akaunti ya Spotify ya mtoto huyo.

Unapotumia kifaa kinachoshikiriwa kwenye Huduma kuu ya Spotify, unapaswa kuwa mwangalifu kuhusu kucheza au kupendekeza maudhui yoyote kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 18 ambayo huenda yasiwafae.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

10. Mabadiliko ya Sera hii

Huenda tukafanya mabadiliko katika Sera hii mara kwa mara.

Tunapofanya mabadiliko ya msingi kwenye Sera hii, tutakupa ilani dhahiri kama inavyotupasa kufanya katika hali hiyo. Kwa mfano, tunaweza kuonyesha ilani dhahiri ndani ya Huduma ya Spotify au kukutumia barua pepe au arifa kwenye kifaa.

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑

11. Jinsi ya kuwasiliana nasi

Kwa maswali au hoja zozote kuhusu sera hii, wasiliana na Afisa wetu wa Ulinzi wa Data kupitia mojawapo ya njia hizi:

 • barua pepe privacy@spotify.com
 • tuandikie kupitia: Spotify AB, Regeringsgatan 19, 111 53 Stockholm, Uswidi

Spotify AB ndiye mdhibiti wa data ya binafsi inayochakatwa chini ya Sera hii.

© Spotify AB

Sehemu ya juu ya ukurasa ↑